Kuna shida gani mkoa wa Pwani?

mwanyaluke

JF-Expert Member
Jan 22, 2015
473
1,448
Nilikuwa Pwani, Wilaya ya Mkuranga, nimetembea vijiji vingi Hadi Kijiji kinaitwa mwanzenga (nimeambiwa ni Kijiji Cha wasanii).

Kilichonishangaza ni maeneo mengi ya mkuranga ni potential sana Kwa ufugaji na ujenzi wa viwanda.

Kilichonichosha ni population ndogo na wenyeji wanaishi maisha magumu , na kutoka mwanzenga to mbagala sio mbali , watu wamerundamana mbagala halafu pembeni kidogo pana maeneo mazuri ya kuanzisha makazi, shida ni ipi watu hawataki kuhamia huko?
 
Nilikuwa pwani, Wilaya ya Mkuranga , nimetembea vijiji vingi Hadi Kijiji kinaitwa mwanzenga (nimeambiwa ni Kijiji Cha wasanii).

Kilichonishangaza ni maeneo mengi ya mkuranga ni potential sana Kwa ufugaji na ujenzi wa viwanda.

Kilichonichosha ni population ndogo na wenyeji wanaishi maisha magumu , na kutoka mwanzenga to mbagala sio mbali , watu wamerundamana mbagala halafu pembeni kidogo pana maeneo mazuri ya kuanzisha makazi, shida ni ipi watu hawataki kuhamia huko ?
Sasa unailaumu Pwani au Mbagala ?
 
Wakazi wengi ni makabila ya pwani kama vile wazaramo. Nafikkri unafahamu wazaramo walivyo wao ni ngoma tu kwenda mbele maendeleo wanasubiri wachaga, waha na wakinga waje waanze kuwatoa.

Kuna mashamba makubwa sana na ardhi yenye rutuba ila hakuna kjtu kinaendelea.

Kuna mzee mmoja ni mzaramo yeye waliachiwa hekari300 maana wazee wao walikuwa wanapeana kutokana na koo, yule mzee yupo yupo tu chanika hapo yale mashamba anayakata kwa wasukuma na wamasai wanafuga huko.

Nilkfika sehemu moja kabla ya kufika jaribu mpakani asee kuna mtu kafuga nyuki eneo zuri halafu mto unapita kati kati humo shambani na analima mahindi na mihogo.

Fursa zipo bongo sema ndio hivyo vijana hata pesa tu za mitaji bado kwetu changamoto tunaendelea jitafuta
 
Wakazi wengi ni makabila ya pwani kama vile wazaramo. Nafikkri unafahamu wazaramo walivyo wao ni ngoma tu kwenda mbele maendeleo wanasubiri wachaga, waha na wakinga waje waanze kuwatoa...
Watu wanafuata fursa lazima waende kweny fursa mzee ....Pwani wabongo hawana uwezo wa kufungua viwanda.

Dar ,Dodoma , mwanza na Arusha kuna fursa huko ndio serikali imeweka nguvu...Hao waha si wangefanya hiyo kigoma kuwa Paris ,tumia akili acha kukariri hayo makabali wangefanya mikoa yao iwe kama Dubai.

Watu wanaenda sehemu ambayo kuna huduma za muhimu ,kikubwa kujitafuta tu ...
 
Mkuu soma tena.
Rudia kusoma then soma mtoa mada ,akiwa na maana hao wamejazana huku Mbagala ...Watu wana mishe zake ukitaka kila mtu arudi mkoa wake hapo Dar hata watu million moja hawafiki...Mtu mishe zake zipo hapo kuna haja gani ya kukaaa huko pwani.

Mikoa ya Moro & pwani maendeleo yao yanaathiriwa sana na Dar .
 
Wakazi wengi ni makabila ya pwani kama vile wazaramo. Nafikkri unafahamu wazaramo walivyo wao ni ngoma tu kwenda mbele maendeleo wanasubiri wachaga, waha na wakinga waje waanze kuwatoa...
Haya masuala ya ukabila nchi hii yatakuja kuisha lini?

Biashara ni Karama ya mtu husika wala haina uhusiano na ukabila.

Mtoa mada acha kukariri.
 
Haya masuala ya ukabila nchi hii yatakuja kuisha lini?
Biashara ni Karama ya mtu husika wala haina uhusiano na ukabila.
Mtoa mada acha kukariri.
Ndo tatizo la wabongo.

Ukweli ndio huo wazaramo wengi hawapendi jishugulisha ndio maana sahivi wapo mwisho huko chanika kutoka katikati ya mji wao.

Ni wavivu na hata wakifanya biashara pesa zao zinaishia kwenye ngoma zile ndio tamaduni zao zilivyo.

Hata elimu pia hawapendi na mm mfano wangu pia nimetolea huko sababu wakazi wengi ni wazaramo
 
Back
Top Bottom