Kikwete na mkapa ni mahasimu tangu mwaka 1995 pale mkapa alipokuwa mgombea Urais wakati kikwete ndiye alishinda kura za maoni, pamoja na hayo wakati mkapa anaondoka madarakani alikusudia kumuacha waziri mkuu wake ili maslahi yake yasivurugike,hivyo akawa anampigia debe Sumaye kwa kushirikiana na makada maarufu kama aki na mzee Steven Mashushanga alie kuwa mkuu wa mkoa wa morogoro.
Pamoja na jitihada za mkapa lkn Jakaya alishinda kwa kishindo kura za maoni mwaka 2005, na alipoingia madarakani. kitu cha kwanza kilikuwa kufuatilia kila uovu aliifanya Rais Mkapa,mfano ni ukamataji wa Fedha ambazo mkapa alificha uswis, inasemekana kuwa ndio yale mabilioni ya kikwete ambayo yalikuwa yanagawiwa kila mkoa.
Pia rais kikwete aliendelea kufuatilia mali za mkapa na kuzitaifisha,mfano ni ile nyumba ya mkapa yenye ghorofa zaidi ya ishirini ambayo ilijengwa Afrika ya kusini,nyumba hiyo hata mandela aligoma kuizindua kutokana na kujengwa na Fedha za ufisadi,
Pamoja na hayo ,watu walioliingiza hasara taifa kwa kushirikiana na Rais kikwete,kwa mfano,Mahalu Mgonja na Mramba,wote waliburuzwa mahakamani,lkn kila waoelekwapo mahakamani,ni mkapa anaeenda mahakamani na kuwa shahidi,rejea kesi ya mahalu.
Kutokana na hayo,mkapa amekuwa akitumia kila jinsi kuihujumu serikali ya rais Kikwete bila mafanikio,
Hivyo ni vigumu saaana kumkuta Rais Benjamin Mkapa akitoa ushirikiano kwa Kikwete.
Kwa misingi hiyo ndio maana Rais kikwete kafanya kila mbinu kuhakikisha Mkapa anaondolewa kamati kuu ili kupunguza nguvu yake ya kupandikiza Rais atakae kuja kulipiza kisasi.