Kuna Mlipuko wa Homa na Mafua makali jijini Dar

Kuna Mlipuko wa Homa na Mafua makali jijini Dar

Mie mwanangu kafariji kwa hali hii ya homa kali na mm pia nimeugua sana chafya za kutosha mwili kuchemka, kichwa kuuma, kikohozi na mafua na jointi kuuma. Mwanangu ameondoka na hali hii ya ugonjwa hapo mnazi mmoja hospital zanzibar majira ya jioni jana.
Dah pole mkuu
 
Ni vile tu ukweli hautaki kusemwa ila CORONAA IPOO..!!
 
Mimi hata Sasa nina mafua, yameanza usiku wa kuamkia leo. Lakini nahisi chanzo ni maji niliyokunywa juzi, yalikuwa yametokea kwenye friji moja kwa moja. I hope I am right.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi nipo kwenye sekta ya afya.

Kwa wiki tatu sasa kuanzia katikati ya November 2020 kumekuwa na mlipuko wa homa kali na mafua makali ambayo huambatana na kikohozi.

Kwa takwimu ndogo niliyochukua kutoka vituo mbalimbali vya afya ni kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa

1. Homa kali
2. Maumivu ya kichwa
3. Mafua makali
4. Mafindofindo

Ni wazi kuwa tunapitia katika kipindi kigumu cha magonjwa haya.

Wengi wa wagonjwa hupona katika kipindi cha siku nne mpaka 7.

Mmejiuliza pia sababu ya mlipuko huu?

Wagonjwa wengi wamepimwa malaria lakini hawana malaria.

Hivyo madaktari wengi wamewapa dawa za homa na kikohozi.

Hali ikoje huko kwenu?
Mpaka sasa naumwa mafua, nimemeza cold off, nimetulia siku moja, yamerudi tena kwa kasi. Naendelea kumeza cold off, natafuna tangawizi na vitunguu maji. Na wife naye mafua yamekaba
 
Ni mabadiliko ya tabia nchi hasa ukizingatie tuko kwenye msimu wa mvua.
Mwenyezi Mungu atatuvusha tu ni suala la muda.
Labda pengine ni silaha za kibaiolojia za mabeberu dhidi yetu kutokana na kasi ya ukuaji wa kiuchumi wa Taifa letu......
 
Huu uzi kama huu ulishaletwa hapa miaka kadhaa iliyopita ilipotokea mlipuko wa corona watu wakaufukua
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi nipo kwenye sekta ya afya.

Kwa wiki tatu sasa kuanzia katikati ya November 2020 kumekuwa na mlipuko wa homa kali na mafua makali ambayo huambatana na kikohozi.

Kwa takwimu ndogo niliyochukua kutoka vituo mbalimbali vya afya ni kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa

1. Homa kali
2. Maumivu ya kichwa
3. Mafua makali
4. Mafindofindo

Ni wazi kuwa tunapitia katika kipindi kigumu cha magonjwa haya.

Wengi wa wagonjwa hupona katika kipindi cha siku nne mpaka 7.

Mmejiuliza pia sababu ya mlipuko huu?

Wagonjwa wengi wamepimwa malaria lakini hawana malaria.

Hivyo madaktari wengi wamewapa dawa za homa na kikohozi.

Hali ikoje huko kwenu?

Ni kweli hata mimi siku 4 zilizopita nilibanwa na mafua makali kikohozi kikali na homa iliyoambatana na maumivu ya kichwa, hali hiyo nilidumu nayo kwq siku 3, nikitumia kidonge kimoja cha Coldruf.

Namshukuru Mungu nimepona sasa.

Huku Morogoro.
 
Chukua taadhari endelea kuwaamini wanasiasa. Sisi sio kisiwa. Kama ni kisiwa why tumekula hela za mabeberu.
 
Mi nilijihami kwa nyagi siku mbili mfululizo baada ya kuona koo limeanza kuwasha! Siku ya tatu nilikuwa fresh na kuendelea na kazi maka leo hamna kitu
 
Wewe si upo sekta ya afya sasa unatuuliza nini ambao ni wakulima wa nyanya, swali lako lijibu mwenyewe au nenda kwa bosi wako wa kitengo ukamuulize,huku unakokimbilia ni sehemu ya porojo tu,toka lini mitandao ya kijamii ikawa na majibu stahiki?acha ujinga bana,kaanze upya.
Yaani we ni mqundu aisee, lengo la mtoa post sio kuuliza ni kufanya watu wawe aware na situation ilivo.
 
Ni vile tu ukweli hautaki kusemwa ila CORONAA IPOO..!!
Yani mm nimeshindwa kuelewa, malaria gani isiyosikia dawa , sina aman moyoni tangu niondokewe na mpendwa wangu.Tuweni makin sana na watoto wa umri wa mika 7 kushuka chini
 
Mimi Jana nimeamua kutorudi katika Hospitali ya private. Nimekuwa nikisumbuliwa na homa Kali na mafua mahali sana. Dalili zote ni za malaria Lakini wananiambia Ati sina malaria. Wamenipa ammoksilin capsules Ati Nina U-T-I. Sasa ni wiki ya pili. Nimeyatupa kule, naenda piga nyungu pamoja tangawizi kwa zaidi . yawezekana ikawa ni ile timu inayoitwa "La Corunya".
 
Tunaumwa Corona lakini serikali yetu imepiga marufuku kutaja huo ugonjwa. Tutegemee kudra za Allah!
 
Back
Top Bottom