Kuna Mlipuko wa Homa na Mafua makali jijini Dar

Kuna Mlipuko wa Homa na Mafua makali jijini Dar

We acha tu cha kushangaza huu uzi ni wa mwaka jana lakini angalia ulivyovamiwa kama ni wa leo leo[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hii inaonyesha ni kweli ugonjwa huu wa mafua makali unaendelea kwa kasi sana.
Huu ni mlipuko mpya. Siyo ule wa mwaka jana. Huoni thread ni ya leo? Inaonyesha pengine kila mwezi November kunakuwa na hali ya hewa inayofanya vijidudu vya flu kusambaa kwa urahisi.
 
Ni kweli kabisa. Mimi ndio nimepona leo toka jumatatu.
Yaani nimekohoa mpaka misuli ya tumbo ikawa inauma kama mtu uliyefanya mazoezi ya kunyanyua kitu kizito ukiwa chali.
 
Na mimi nilikuwa nashangaa kwa mlipuko huu.

Hali ni mbaya ila uzuri ni kuwa huu ugonjwa huwa unaisha wenyewe.

Ila mlipuko upo tena wa kutosha.
Namimi nipo kwenye daraja la Kigamboni nashangaa na wakigamboni wananishangaa mimi.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi nipo kwenye sekta ya afya.

Kwa wiki tatu sasa kuanzia katikati ya November 2020 kumekuwa na mlipuko wa homa kali na mafua makali ambayo huambatana na kikohozi.

Kwa takwimu ndogo niliyochukua kutoka vituo mbalimbali vya afya ni kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa

1. Homa kali
2. Maumivu ya kichwa
3. Mafua makali
4. Mafindofindo

Ni wazi kuwa tunapitia katika kipindi kigumu cha magonjwa haya.

Wengi wa wagonjwa hupona katika kipindi cha siku nne mpaka 7.

Mmejiuliza pia sababu ya mlipuko huu?

Wagonjwa wengi wamepimwa malaria lakini hawana malaria.

Hivyo madaktari wengi wamewapa dawa za homa na kikohozi.

Hali ikoje huko kwenu?

Nina mafua yanayoendana na hizo tarehe na homa kali, nimeacha hangaika nayo yapone yenyewe, ila watoto hawana kabisa na wakipata wanapona haraka
 
Huenda corona imerudi I see, maana hata mi pia hapa nakohoa , famila nzima hivyohivyo, mafua makali naaumivu ya kichwa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mimi nipo kwenye sekta ya afya.

Kwa wiki tatu sasa kuanzia katikati ya November 2020 kumekuwa na mlipuko wa homa kali na mafua makali ambayo huambatana na kikohozi.

Kwa takwimu ndogo niliyochukua kutoka vituo mbalimbali vya afya ni kuwa kuna ongezeko la wagonjwa wa

1. Homa kali
2. Maumivu ya kichwa
3. Mafua makali
4. Mafindofindo

Ni wazi kuwa tunapitia katika kipindi kigumu cha magonjwa haya.

Wengi wa wagonjwa hupona katika kipindi cha siku nne mpaka 7.

Mmejiuliza pia sababu ya mlipuko huu?

Wagonjwa wengi wamepimwa malaria lakini hawana malaria.

Hivyo madaktari wengi wamewapa dawa za homa na kikohozi.

Hali ikoje huko kwenu?
Hizi dalili zinaendana sambamba Allergic Rhinitis lakini.... Inatia wasi wasi hasa unapotoa huduma,

Idara zinazohusika watuambie kinachoendelea, yameniweka nje ya ofisi hii siku ya nne...

Dah
 
Ni kweli kwangu nyumba nzima kwa wiki nzima ilikuwa ni homa, kikohozi, maumivu ya kichwa, na kwenye joints wote watu 4... mama na watoto 2 pamoja na dada wa kazi... imetushangaza sana ila kwa sasa wote wanaendelea salama.. wamepima vipimo vyote negative ikabidi kutumia dawa za homa na kwa tahadhari wakatumia dawa za malaria
 
Hizi dalili zinaendana sambamba Allergic Rhinitis lakini.... Inatia wasi wasi hasa unapotoa huduma,

Idara zinazohusika watuambie kinachoendelea, yameniweka nje ya ofisi hii siku ya nne...

Dah
Mimi nina hiyo Allergic Rhinitis, dawa zote ambazo nimetumia zimedunda, yaani sina amani, sina raha kabisa
 
Mimi nina hiyo Allergic Rhinitis, dawa zote ambazo nimetumia zimedunda, yaani sina amani, sina raha kabisa
Allergic rhinitis...... Mara nyingi haina matibabu ni mazoezi, kunywa maji mara kwa mara na kupata muda wa kupumzika

Ikizingua tafuta antihistamine, corticosteroids na analgesic

Utakula maisha
 
  • Thanks
Reactions: ram
Dawa gani mkuu, manake mateso ninayoyapata na haya mafua, sina hamu kabisa

Ascoril.d hii ni ya kifua maana nilikuwa nakohoa na pia nakunywa zile toff plus za chenga chenga ukipata za kenya itapendeza zaidi bila kusahau dicloper
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom