Too much politics.
Mh JPM Wapambe hawana jema. Hawatakueleza kweli, na ukweli tutakueleza sisi wengine ambao hatusubiri mrija wa mnunurisho wa asali na maziwa.
Kwani kuna awamu miradi hiyo haikuwapo.
Na kama haikuwapo hakukuwa na Miradi mbadala.
Tatizo la msingi si miradi, tatizo ni consistance ya miradi. Lakini kubwa zaidi ni pesa inayopelekwa kwenye miradi ni asilimia ngapi.
Kwa miaka 3 mfululizo mizara na halmashauri zimepatiwa chini ya asilimia 30 ya makadirio yao, tena pesa yenyewe ni ya mkopo. Tunaweza tu kuwapongeza viongozi wetu kwa kutoogopa kukopa na pesa kupekekwa kwenye miradi kwa chini ya 30%.
Pamoja na kuwa kiongozi wetu ana uthubutu, tunahitaji mabadiliko ya sera zake kwani uchumi wa nchi hauendeshwi kwa kukopa na kwa kutoza kodi kubwa wawekezaji. Ukifanya hivyo wawekezaji watapunguza uwekezaji wao. Tunaona viwanda kama dangote, kwasasa vinazalisha chini ya asilimia 20. Ni juzi tu tumesikia kiwanda cha tumbaku kinafungasha virago morogoro. Sababu kubwa ni software zetu au sera zetu.
Tumetumia zaidi ya bilioni 571 za kitanzania kununua ndege hii ya Boeing 787, fedha za kodi zetu.. Nani alikueleza tunahitaji ndege? Wananchi gani huko kwenye ziara wanalilia ndege?
Wanakijiji wa kijiji cha Shuka, halmashauri ya Mtama, Lindi wanalalamika hawana maji ya kutumia, wanatumia maji na wanyama, maji ni kero kwao.
Mimi na wenzangu, kwetu huko Tarime, zahanati, vituo vya afya na hospitali ni kero kubwa, kata hazina vituo vya afya, hospital ya wilaya hakuna Vifaa tiba.
Needs vs Wants.. Mahitaji makuu sidhani kama ni hayo madege,.. Hizo ni 'wants' tu. Wananchi wa Mtama wanataka visima vya maji safi na salama sio ndege hizi .
Tatizo la wapambe ni hili hata Leo ukiamua kununua Lamborghini ,Ferrari, Porsche, Buggati,Bentley, Aston Martin, Jaguar, Rolls-Royce, Audi, Maserati wakati wa njaa kali nyumbani wapambe watakuimbia kwa mapambio, kuwa hayo hayakuwahi kufanywa huko nyuma.
Kuna upungufu wa vyumba vya madarasa kwa zaidi ya asilimia 50 kwa shule za msingi na sekondari..
Kuna upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo mashuleni kwa zaidi ya asilimia 40 shule za msingi na sekondari
Kuna upungufu wa walimu wa shule za msingi na sekondari nchi nzima kwa zaidi ya asilimia 30.
Vipi upungufu wa vifaa tiba na dawa Katika hospitali za serikali kwa zaidi ya 65%?
Upungufu wa madaktari na wauguzi Katika hospitali za umma nchi nzima kwa zaidi ya asilimia 45?
Mh JPM Wapambe hawana jema. Hawatakueleza kweli.
Courtesy
TUSIKASIRIKIANE! Rais wangu Magufuli: Trump atakuwa alicheka kwanini Profesa Kabudi alipaita UDSM ni jalalani, chuo kikuu cha kitaaluma na mashuhuri kusini mwa jangwa la sahara. Trump lazima ashangazwe na hili. Au labda Trump alishangaa ni kwa sababu gani mtu mwenye hadhi ya kuwa profesa...
www.jamiiforums.com