Kuna Mkoa haujapata mafanikio ya Magufuli?

Kuna Mkoa haujapata mafanikio ya Magufuli?

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,119
Reaction score
31,639
Hili ni swali kwa wawakilishi wa wananchi na wananchi ili tuende sawa.

1. Kuna mkoa haujajengewa hospitali au kituo cha afya?

2. Kuna mkoa hauna mradi wa maji?

3. Kuna mkoa hauna mradi wa barabara?

4. Kuna mkoa hauna mradi wa umeme vijijini?

5. Kuna mkoa haujapata mradi wa ujenzi wa shule?

6. Kuna mkoa una machinga asiyetambuliwa?

7. Kuna mkoa haujengi viwanda?

8. Kuna mkoa haujapata pembejeo za kilimo?

9. Kuna mkoa haujapata fursa ya kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa?

10. Kuna mkoa hauna huduma bora za fedha?

Hayo ni maswali yangu machache kati ya mengi yenye kuhoji utekelezwaji wa Ilani ya CCM.

Tukumbuke kuwa wakati miradi kadhaa ikitekelezwa basi kuna miradi mikubwa na ya kimkakati inayoshika kasi tena kwa fedha za ndani.

1. Mradi wa SGR
2. Mradi wa kufua umeme
3. Manunuzi ya ndege
4. Mradi wa Maji
5. Ujenzi wa flyovers n.k

Rais Magufuli songa mbele wanafiki wanaombea uumwe!!
 
5-Ujenzi wa flyovers
13346561_1045891872161693_1872851944272501840_n.jpg
 
Marxlups na Jingalao mme-editi picha. Hata hivyo picha moja ambayo tena ni ya kuediti haitoi picha halisi ya Tanzania nzima. Ungeediti picha nyinginyingi.
 
Pwani.unajumuisha wilaya za
Mkuranga
Kibiti
Rufiji
Kisarawe
Bagamoyo
Kibaha
Mafia
 
Tazama stendi kuu ya mkoa wa kagera mjini bukoba.

Tangu Uhuru mkoa wa kagera( wenye watu zaidi ya million tatu na wa tatu Kwa idadi ya watu nchini) haujawahi kuwa na stendi inayoeleweka.



Halafu unasema???View attachment 1246574View attachment 1246576
Kuhusu sekta ya mawasiliano Kagera ni mji wenye maji kimawasiliani na Serikali ya Magufuli inalitambua hilo kwa kuwekeza katika ujenzi wa meli ya MV VICTORIA...Hakika Chuma anawapenda wote !!
 
Mradi wa maji ngapa huko lindi haujatekelezwa?kama bado Mheshimiwa Magufuli atasoma hapa
Hahah ule ambao maji hayatoki

Nilitegemea ulete lundo la miradi kama ya Chato. Hamna mradi Lindi nasubiri ahadi ya mheshimiwa ya ujenzi wa barabara ya Nachingwea. Maana ahadi zake kama hizi wale wa Arusha barabra ya mianzini hata cm moja haijajengwa. Au wale wa Kidawe to Nyakanazi mwaka juzi
 
Back
Top Bottom