Kuna Mkenya amepiga 180 KPH kwenye Nairobi expressway

Tony254

JF-Expert Member
May 11, 2017
16,017
16,427
Hii Nairobi expressway itatuonyesha mambo. Kuna huyu jamaa anapiga 180 kph kwenye Nairobi expressway.

Kwangu naona kama anahatarisha maisha yake na sioni kama ni sawa. Japo jamaa amenishangaza kwa ujasiri alionao. Amepiga Westlands hadi JKIA distance ya takriban 27 kilometres kwa dakika 7 tu.

inakushangaza hiyo?!? hapa bongo kuna watu wana gari za 280km/hr yanazimaliza zote!!!. umemsahau pascal mayala na mpikipiki wake???!!??
Bongo kuna gari inaeza shika hii GTR?
FB_IMG_1653938697554.jpg
 
Ha ha ha!! Wow.... tutayafanya sana haya ila mimi mwoga wa mwendo kasi.
Haya vijana mnaowahi uwanja wa ndege, mumeachiwa barabara ndio hiyo mjimwayi mwayi, haya mavitu mbona yalichelewa enzi za ujana wangu....
 
Mbona huku bongo kwenye hizi Barbara zetu za twende sote watu wanamaliza vibati!!

Lengo hapa LA mleta uzi ni Nairobi expressway na sio 180

Bongo wapi unapiga 180 mjini kati, hizo hata Kenya tunazipiga maporini kwenye barabara za mikoani, ila huyu kadhihirisha itakavyokua rahisi kukatiza mjini kati kwa dakika chache tu.
 
inakushangaza hiyo?!? hapa bongo kuna watu wana gari za 280km/hr yanazimaliza zote!!!. umemsahau pascal mayala na mpikipiki wake???!!??
Wacha ujinga. Bongo hamna expressway. Barabara zenu zina bumps. Pia barabara zenu hazina interchange katika kila junction kwa hivyo huwezi kupiga 180 kph katika barabara za Tanzania bila kuhatarisha maisha.
 
Enzi za ujana wangu.

I think nina miezi sasa sijagusa 180. For real
Wacha uongo. Bongo kuna barabara gani ambayo unaweza kupiga 180 kph? Kuna barabara gani ambayo haina bumps na ina interchanges katika kila junction? Bongo ukipiga 180 kph unahatarisha maisha.
 
Mbona huku bongo kwenye hizi Barbara zetu za twende sote watu wanamaliza vibati!!

Lengo hapa LA mleta uzi ni Nairobi expressway na sio 180
Sidhani kama kuna barabara yoyote ya Bongo ambayo gari inaweza kufika 180 kph bila kuhatarisha maisha.
 
Mtanzania mmoja aliyejaribu huo upuuzi wa kupiga 180 kph alikufa kwa ujinga wake. Barabara ambalo ni single-carriageway,lina round-abouts na lina bumps utakuwa zuzu kujaribu kupiga 180 kph pale.
 
Sidhani kama kuna barabara yoyote ya Bongo ambayo gari inaweza kufika 180 kph bila kuhatarisha maisha.
Popote pale 180km/h ni kuhatarisha maisha.
Hiyo 180 Mara kibao huku watu wanaifuta, wengine hatuna tabia ya kurekodi hizi mambo.
 
Wacha ujinga. Bongo hamna expressway. Barabara zenu zina bumps. Pia barabara zenu hazina interchange katika kila junction kwa hivyo huwezi kupiga 180 kph katika barabara za Tanzania bila kuhatarisha maisha.
Kwani huyo unaemshangilia hajahatarisha maisha hapo? Gari za kawaida sana 180kph inafika less than 30sec sasa jiaminishe hapa Dar hakuna hio stretch.
 
Mtanzania mmoja aliyejaribu huo upuuzi wa kupiga 180 kph alikufa kwa ujinga wake. Barabara ambalo ni single-carriageway,lina round-abouts na lina bumps utakuwa zuzu kujaribu kupiga 180 kph pale.

Usiongee usivyovijua. Hizo ni ajali mbili tofauti. Kwenye hio ajali walikufa watu watatu. Sio huyo mwehu aliojirekodi.
Btw speed kills.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom