Makosa 99 Yaliyokuwepo Kwenye Talaka niliyompa Mke wangu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
HAYA NDIYO MAKOSA 99 YALIYOKUWEPO KWENYE TALAKA NILIYOMPA MKE WANGU.

Na, Robert Heriel

TAIKON WA FASIHI
ROBERT HERIEL
S.L.P
TIBELI

YAH: SABABU 99 YA KUMPA TALAKA MKE WANGU

Kichwa cha habari hapo juu cha husika.

Miaka kadhaa nyuma nilifunga ndoa na mke wangu niliyempenda kwa dhati yote, sikubakiza hata chembe ya upendo wangu kwake. Nilifuata taratibu zote za kimila, kidini na kiserikali kuhakikisha anakuwa Mke wangu. Kama hamtajali niruhusuni nitaje taratibu kadhaa nilizozifanya mpaka kufikia kufunga ndoa na Mke wangu Kipenzi;
1. Kuchumbia, hapa nilimtongoza mke wangu
2. Kukaa uchumba takriban miaka miwili (courtship)
3. Kujitokeza na kutoa mahari ukweni
4. Matangazo ya ndoa yetu.
Tulitangaza ndoa yetu katika maeneo mbalimbali na majukwaa mbalimbali. Tulitangaza kanisani, misikitini, kwenye magazeti, redioni, Luningani, pia tulichapisha matangazo ya karatasi tukabandika kwenye nguzo mji mzima. Pia tuliweka matangazo makaburini kwani kuna ndugu, jamaa na marafiki waliokuwa wametangulia mbele za haki lengo ni kuwajulisha hata kama wamekufa.
5. Hatimaye Tulifunga Ndoa takatifu ambayo ilihudhuriwa na watu wengi bila shaka ni kutokana na matangazo tuliyoyafanya. Harusi yetu ilikuwa mubashara kabisa kwenye Redio na luninga.
6. Tukala fungate kwa siku saba
7. Tukazaa watoto

NImeona nikumbushe taratibu hizo ili huko mbele nisijeonekana mimi ndiye mgomvi. Taikon ni Mtu wa itifaki, mtu wa kufuata taratibu Buana!

Maisha ya ndoa bila doa yalianza, tulifurahia maisha. Tulicheka tukacheka. Tulifurahi tukafurahi. Nyumba ilikuwa pepo yenye upepo mwanana wa fukweni. Nani mtaani ambaye hakujua mapenzi yetu, watu wote walitamani kuwa kama sisi, huku wenye vijicho na roho mbaya wakituombea dua mbaya ambayo tuliiona kama dua la kuku ambalo katu lisingetupa siye mwewe tuliokuwa tukikata anga la mapenzi kwa mbawa zetu mbili.

Huku na huku tukavunja chaga, watoto wakazaliwa wenye sura kama zetu. Hakika upendo wetu uliimarika maradufu, ikawa ndiyo turufu yetu.

Kufupisha hekaya hii, basi kizungumkuti kikaingia ndani ya nyumba yetu. Kasoro ya makusudi ya uchawi na ushetani iliyodhamiria kuvunja ndoa yetu ikatimua vumbi la uhaini.

Na hii ndio sababu muda huu unasoma waraka huu wa talaka kwa mke wangu. Sababu hizi 99 za kumpa talaka mke wangu ni muhtasari wa makosa yake yasiyopungua elfu moja. Nimeyafupisha kusudi yasiwachoshe ninyi ndugu zangu ninaowaheshimu. Makosa haya sio ya Martin Luther aliyoyaandika kulikosoa Kanisa la Roma ya wakati ule. Haya ni Makosa 99 ya ndoa yangu aliyoyafanya Mke wangu kipenzi.

Hakuna kosa hata moja nililomsingizia, yote ni Amini na kweli, shahidi ni mimi, yeye, watoto, baadhi ya ndugu, na majirani wakiwemo na marafiki.

Nakusudia Waraka huu wa Talaka ufuate itifaki ile ile ya ndoa yetu. Talaka hii itabandikwa kwenye nguzo za umeme kila mpita njia asome, itabandikwa Makaburini kusudi wale waliokufa nao wajulishwe kwani kuna waliokuwepo siku ya harusi yetu na sasa wamekufa, talaka hii itawekwa kwenye mfumo wa PDF na kurushwa mtandaoni ili waliombali waisome, itatangazwa kwenye Redio na luninga na kusomwa kila asubuhi na jioni walau makosa kumi kwa siku ili watu wayasikie, tayari nimeshalipia pesa kwa kazi hiyo, Talaka hii itasomwa Kanisani na Misikitini kila siku ya ibada ili waumini wasikie kwani isingefaa wasijue sababu, Pia itasomwa vilabuni na sehemu zote za starehe kwani nao wanapaswa kujua kuwa yule aliyewalewesha siku ya harusi ametokea talaka na watasomewa talaka hii.
Pia Waraka huu wa Talaka nimeshaupeleka Bungeni, ili usomwe kama hoja ya dhararu, ili wabunge na mawaziri na wafanyakazi wote wajue. Waraka huu pia nimeupeleka Mahakamani na Mahakimu, mawakili na wanasheria wameshindwa kujibu hoja zangu, hivyo wameipa talaka hii uhalali.
Waraka huu wa Talaka pia nimeupeleka katika vikozi na kambi zote za jeshini, kuanzia Lugalo, Monduli, Oljoro n.k kote huko

Nakusudia Talaka hii iwe kwa mfumo wa maandishi kama hivi, kisha nimeshaandaa wasanii watakaotungia nyimbo makosa haya na kuyaimba, napendekeza wimbo uende kwa jina la "Talaka ya Itifaki", pia Nimeandaa Malenga wa ushairi na Tenzi nao wataiweka Talaka hii kwa mfumo wa ushairi.

Sitarajii upatanisho wala kikao chochote ambacho lengo lake ni kusuluhisha na kuniweka pamoja na Mke wangu. Japo nafahamu heshima niliyonayo ni kubwa hivyo sitakataa kuitishwa kikaa kama wakubwa watataka, ila siku hiyo kila mmoja awe na nakala ya Waraka wa talaka hii yenye makosa 99, kisha mwendesha Kikao atafungua kikao baada ya kusoma agenda ya kikao, atataja hayo makosa 99 ili yajadiliwe moja baada ya jingine. Sitarajii hoja zilizopo kwenye talaka kupanguliwa kienyeji kwani mambo haya ni mazito.

Baada ya kukuchosha na maelezo haya, sasa niruhusu niyataje makosa 99 aliyoyatenda Mke wangu ambayo yamenifanya nimcharaze talaka hii;

MAKOSA 99 YA MKE WANGU ALIYONIKOSEA YALIYOMUONDOLEA NAFASI YA MKE NDANI YA NDOA TULIYOFUNGA MNAMO MIAKA KADHAA ILIYOPITA

1. Kupoteza pete ya ndoa
Mke wangu alipoteza pete ya ndoa nje ya nyumbani, niligundua baada ya kuifuma meseji ambayo alimtumia hawara wake. Kwa siri walichongesha Pete ingine iliofanana na ile niliyomvisha. Asijue pete halisi niliichukua siku ile waliokuwa wamelala Guest na huyo hawara kwani aliiacha bafuni.

2. Kuvalishwa Pete Bandia ya ndoa na mwanaume mwingine.
Baada ya pete kuchongwa, waliandaa sherehe katika fukwe maarufu hapa jijini Dar es salaam. Mke wangu akavalishwa huku baadhi ya wahusika wakimshangilia huku picha na video zikiwachukua

3. Kuwasiliana na Hawara mwingine kwa call na jumbe za mapenzi kwa siri
Vocha ninamuwekea mimi, simu nimemnunulia mimi. Lakini ajabu ni kuwa sms na clall nyingi anamtumia Hawara wake. Asijue kuwa simu ile nimemnunulia, hivyo niliiwekea ulinzi wa taarifa zote zitakazofanyika kwenye simu ile.

4. Kutuma Picha za uchi, na whatsApp call akiwa uchi.
Nilimia lakini acha niseme, mke wangu alikuwa anapiga picha na video zake za uchi na kumtumia hawara wake. Hata hivyo alikuwa akipigiwa WhatsApp Video call kisha huvua nguo zote na ndipo wanaongea.

5. Kumtumia Hawara wake pesa nilizompa.
Mke wangu alimtumia hawara wake shilingi milioni moja nilizompa kwa ajili ya kulipa ada ya watoto, kumbe alinidanganya. Uhujumu uchumi wa familia mke wangu kaufanya sana. Niliomba muongozo kwa serikali inipe hukumu ya mhujumu uchumi wa nchi nikashangaa kwa nini wanapewa adhabu kali vile.

6. Kuvaa Nguo za Ndani alizonunuliwa na Hawara wake zilizoandikwa herufi iliyoanzia jina la Hawara wake.
Siku moja Mke wangu alikuja na dozeni sita za nguo za ndani zenye rangi tofauti zote zikiwa na herufi ya mwanzo ya jina la hawara wake. Nilichunguza na kujua kuwa alizitoa kwa hawara wake. Ushahidi nitaambatanisha mwisho wa talaka hii

7. Kutoa Siri ya familia na kuudhalilisha Muungano
Mke wangu ameudhalilisha muungano na kutoa siri za familia ikiwa na kutoa mipango na mikakati yetu ya siri ya maendeleo kwa hawara wake. Kisha akatoa siri ya kuwa mimi nina kibamia, tena simfikishi kileleni. Nilipofika Lugalo nilimuuliza kamanda Mkuu kuwa, Hivi ninyi wanajeshi, mtu anayetoa siri zenu kwa adui mnamuitaje, akajibu 'msaliti' nilipoulizia adhabu ya msaliti niliamua kuondoka tuu.

8. Kuwatumia na Kuwafundisha watoto kufanya uovu wake.
Mke wangu amekuwa akiwafundisha watoto katika hila zake za umalaya. Amewafundisha watoto wangu uongo. Imefikia hatua watoto hata wasipoambiwa cha kusema na mama yao, sasa wame-master kubuni uongo kusudi kumtetea mama yako endapo nitakuwa sijamkuta nyumbani

9. Kumpenda Muigizaji wa filamu anayefanana na Hawara wake.
Mke wangu anapenda kuangalia tamthilia, sasa kuna tamthilia moja kuna muigizaji kafanana na hawara wake anampenda mno. Kabla sijajua mahusiano yake ya nje alikuwa akimpenda na kumsifia tuu bila sababu huyo muigizaji wa tamthilia pindi anapomuangalia. Mimi nilichukulia kawaida lakini kumbe alikuwa na jambo la siri lipo moyoni.

10. Kumpa Lift Hawara wake ndani ya Gari letu, kisha kufanya mapenzi.
Gari nimempa, nimenunua kwa hela zangu, kwa jasho lango. Leo anampakiza huyo Hawara wake, kisha anafanya mapenzi na kushikwa shikwa ndani ya gari langu. Akiii! Huyu mwanamke ni shetani. Ushahidi nimeuambatanisha,

11. Kumuingiza Hawara wake nyumbani kwangu.
Kipindi sijajua kuwa mke wangu anatoka na huyo hawara wake, kuna siku alikuja naye nyumbani akamtambulisha kuwa ni mfanyakazi mwenzake. Sikushtuka kitu, lakini nilipoingia ndani wakati narudi sebuleni nilishangaa kuona mkono wa huyo hawara ukimalizika ukiepa nisiuona ulivyokuwa unamshika mke wangu eneo la mapajani.
Nilipoenda hospitalini kuulizia kwa Daktari kuwa hivi, mtu anayechukua sindano yenye sumu kisha akaingiza kwenye mwili wako, anakusudia nini. Daktari akanijibu; anakusudia kukuua. Nikaondoka

12. Kuninyima Tendo la ndoa kwa mwezi mzima
Mke wangu ilifikia hatua akaninyima tendo la ndoa mwezi mzima kwa kisingizio amechoka, mara anaumwa yaani ilimradi. Wakati kwenye sms zake zinaonyesha kila baada ya siku tatu anampelekea hawara wake.

13. Kuwaletea watoto wangu zawadi alizopewa na Hawara wake
Mke wangu pia alianza tabia mbofu tena Mbovu. Hakuona aibu kuja na vijizawadi vyake kutoka kwa huyo hawara wake kisha akawapa watoto wangu. Hivi huyu mwanamke anaakili sawa sawa. Tangu lini adui yangu awe rafiki kwa watoto wangu.

14. Kufanya mapenzi Style mbaya zinazohatarisha uhai wake akiwa na hawara wake
Mke wangu akiwa na mimi anajifanya hapendi kufanya mapenzi kwa mitindo migumu anasema hajazoea tena nikijaribu ananambia anahisi roho yake inatoka. Lakini Ajabu ni kuwa akiwa na hawara wake anafanya style hizo hizo tena moja sikuwahi kuiona wala kuijua. Nilipofuatilia nikaambiwa inaitwa "POPO KANYEA MBINGU" Dooh! Ushahidi ninao, hivyo kwenye kikao hatutajadili maneno matupu, tutaona mambo live na hakuna kukatisha ushahidi. Vinginevyo kama nilivyosema pasiwepo na kikao, muiridhie hii Talaka.

15. Kufanya Mapenzi Kinyume na Maumbile
Mpaka nasikia kulia, usiniulize nalia nini, naumia, najua sio mwili wangu lakini ni Mke wangu huyu. Kwa macho yangu wlaa si kuhadithiwa. Hawara mshenzi mkubwa yule, hivi ni wakumharibu mke wangu. Lakini ndio nimeshatoa Talaka sasa, wakafanye uchafu wao

16. Kumtelekeza Mtoto Saluni kisha yeye kutokomea kwa hawara wake.
Siku fulani ya Wikiendi tukiwa nyumbani, Mke wangu aliniaga anaenda Saluni, nikamwambia aende na yule mtoto mdogo wa miaka mitatu unusu. Asimtelekeze Saluni, sasa mimi nikiwa naondoka nyumbani na watoto wengine nampitishia funguo ili niwapeleke watoto kufurahi, nafika saluni simkuti, nampigia simu, ananiambia yupo saluni, namwambia mpe G niongee naye ananikaripia. Nilichokifanya sikumwambia chochote, nilimchukua G pale saluni nakuenda nae sehemu ya watoto kufurahi. Kilichotokea baadaya yeye kurudi ni uongo uongo tuu.

17. Kugugumia na kulalama kwa mahaba wakati akifanya mapenzi na hawara wake.
Akifanya na mimi kimya kama maiti. wala hatoi mguno, yaani kimya kama sanamu. Lakini akiwa na hawara wake anavyolalama daah! Basi Taikon naumia sana. Kwa nini alalame vile wakati kwangu halalami.

18. Hawara wake Kutumia Puturu au Mundende
Haiwezekani mtu afanye mapenzi masaa manne unstopable. Hiyo haipo, hata nilipomuuliza Mwl. Kashasha kuwa mpira unadakika ngapi alinambia ni dakika 90 ambazo zinamapumziko. Sasa kwa nini Hawara yule amfanyie Mke wangu ukatili ule. Kwa nini atumie Puturu, tena apake Mundende. Kama asingekuwa amepaka huenda nisingemuacha mke wangu.

19. Kumuendea Kwa mganga hawara wake asimuache
Kwanza nilishawahi kumuambia Mke wangu, makosa mawili yatakufanya nikupe talaka bila kikao na mtu yeyote, mosi, Nikikukuta ugoni, pili, nikikukuta na uchawi au ushirikina. Lakini mke wangu ni sikio la kufa. Tena angalau angeniendea mimi kwa Mganga ili nizidi kumpenda japo ningemfukuza lakini ningemuelewa, lakini mtu anaenda kwa mganga kisa asiachwe na hawara mshenzi, hakika sitomsamehe ng'oo!

20. Kwenda Kilabuni na kwenye kumbi za Starehe na Hawara wake.
Kuna siku nilisafiri kikazi kwenda mkoani, Mke wangu asiende kwenye kumbi za starehe na huyo hawara wake, wakitumia gari langu, wakitumia pesa yangu, jamani! Jamani! Huko kilabuni walikunywa wakawa njii! Wamelewa kazi kufanya upuuzi. Nilipokwenda kilabuni kuulizia walevi kuwa je ni halali kwa mtu kuchukua mke asiyewake na kuchukua mke wa mtu kwenda naye kilabuni. Wakanijibu "nani kamwaga pombe yangu?"

Kwa Leo tuishie Makosa 20, kesho nitaendelea makosa ishirini mengine.

Nakala ifikie watu hawa;
1. Ukweni
2. Familia yetu
3. Viongozi wa Kanisa na Msikiti niliofungia ndoa
4. Mahakama
5. Ndugu, Jamaa, na Marafiki

Talaka hii imefuata itifaki, na imeandikwa kusudi watu wajue sababu za Taikon kumuacha mke wake. Wasiniulize ulize kila wanionapo.

Bajeti ya Talaka hii ni milioni 10 ambazo zitaelekezwa kwenye matangazo, uandishi, wasanii.

Ulikuwa nami, Mtoa Talaka. Uliza Swali lolote, utajibiwa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Namba 14 na 18 ulijuaje


Ila kwa makosa uliyoyairodhesha

Inaelekea hawara wa mke ana Game la hatari.....yaani mkeo kafikishwa mount evarest aisee...utasubiri sana heri umpe talaka tu

Cha kusikitisha kama ni mario sasa hivi mkeo ataachwa akatafutwe mwenye pesa
 
Back
Top Bottom