Kuna kama mlipuko wa homa na mafua dsm

Kuna kama mlipuko wa homa na mafua dsm

Mimi azuma niliacha nikameza antibiotics maana nilivokuwa Sina nguvu plus hyo azuma huchosha zaidi Sasa hivi nadunda ingawa nakunywa sana tangawizi nyingi kwenye chai na asali, nimeanza kufikiria tu kupata hyo chanjo ingawa kirusi kina change.
Azuma ni antibiotic pia mkuu.
 
Aisee yaani yamenishika hadi maskioni naskia mingurumo tu
 
Mimi azuma niliacha nikameza antibiotics maana nilivokuwa Sina nguvu plus hyo azuma huchosha zaidi Sasa hivi nadunda ingawa nakunywa sana tangawizi nyingi kwenye chai na asali, nimeanza kufikiria tu kupata hyo chanjo ingawa kirusi kina change.
dah,Mimi mwenyewe nasubiria mwili upate nguvu nikachanje, Kuna ndugu jamaa wamechanja,wao siwasikii kabisa kulalamika na hii hali
 
Kweli na mimi hoi homa, kichwa na mafua makali tangu jumamosi. Yaani kchwa hakiskii panadol. Nashukuru naendelea vizuri.
Hatari Sana mkuu, mi Hadi nilipiga simu kwa babu katavi, nikajua hiki kichwa itakuwa jirani yangu ambae tuna mgogoro wa mipaka kanitupia jini "
 
Ni kweli kabisa mkuu, na hospitali zimefurika wagonjwa, jana nimeenda hospitali mbili hivi mmh!
Mi ndio sikutaka kabisa kwenda hospital,nilijua kwa jinsi nilivyokuwa nachemka mwili,ningeambiwa nna covid19
 
Mimi navyojua ni majuzi tu hapa kulikuwa na joto kali, kwa mvua zilizonyesha na kubadili hali ya hewa lazma magonjwa ya kawaida kama kikohozi na mafua ambayo mara nyingi husindikizwa na homa lazma viwapate watu. Malaria pia sababu ya kuongezeka kwa mazalia ya mbu, Hiki kitu pia si kwa dar tu ni mikoa mingi, hali ya hewa ikibadilika mfano kipindi cha jua kali utakuta watu wana mafua sana na vikohozi sababu ya vumbi au kipindi cha mvua, waathirika wa malaria wanaongezeka. NI magonjwa ya msimu tu sidhani kama ni issue kubwa kama inavyokuzwa humu
Omicron hako ila hakana nguvu sana japo kinaenea sana juzi bibi mkubwa kaumwa tumepima vyote hakuna kitu tukajuwa kidudu kimevamia ila tujihadhari tu hakitishi sana kama lile baba lao la mwaka 2020.
 
Ni kweli kabisa! Binafsi tangu juzi nina homa kali pamoja na wanafamilia wawili na majirani kama watatu wote tunauguza homa
 
dah,Mimi mwenyewe nasubiria mwili upate nguvu nikachanje, Kuna ndugu jamaa wamechanja,wao siwasikii kabisa kulalamika na hii hali
Hata mimi inabidi tu nikachanjwe maana kubanwa kifua si mchezo aisee,
 
Mi nashindwa kuelewa hizi waves zinavyojitokeza...mara utaskia delta force mara omicro...hii inamaana ile corona Og washaimaliza na vimebakia vimelea vichache tu vya virus au zote zipo uwanja zinaupiga mwingi?
 
Ndio ngoma inarudi hio!! 3rd wave Omicron. Sema hii haitishi sana. Wameteleza kwenye formula.

Nakumbuka 2019 miezi ya mwishoni Kama hiihii zilikuja post kama hizi hizi humu JF kabla mamlaka zozote Afrika hazijajua chochote kuhusu Corona.

Nikiwa kama mtaalam wa magonjwa ambukizi niliona JF ilitisha sana na vyombo yetu vya ku monitor AFYA ya jamii ni vya hovyo kabisa.
2019 ilianza hivi hivi, wakadai upepo mbaya,, kufikia march watu wakatafutana, makaburi yalichimbwa hadi basi,
Vaeni barakoa, epukeni msongamano piga nyungu, choma chanjo,
Hiyo homa unayoipata ni intro tu,
 
Nilitegemea koment hii
Hii homa ya juzi jaaman tuache utani, mi mpaka nikajihisi nina ngoma au nina ugonjwa gan wa ajab? nilitetemeka siku nzima na nikawa sina mood ya msos plus kuvuja jasho ovyo ovyo. Hii inawezekana ni Omicron imenisalimia na kwenda zake, nimebakiwa na mafua tu yanaishia
 
Ndio ngoma inarudi hio!! 3rd wave Omicron. Sema hii haitishi sana. Wameteleza kwenye formula.

Nakumbuka 2019 miezi ya mwishoni Kama hiihii zilikuja post kama hizi hizi humu JF kabla mamlaka zozote Afrika hazijajua chochote kuhusu Corona.

Nikiwa kama mtaalam wa magonjwa ambukizi niliona JF ilitisha sana na vyombo yetu vya ku monitor AFYA ya jamii ni vya hovyo kabisa.
2019 December ndugu yangu alifariki kwa covid akitokea congo akazidiwa mbeya akafariki, wakati huo bado mambo ya covid africa hakuna taarifa kama ugonjwa upo tayari.
 
Mimi jumanne niliamka mapema kwa ajili ya majukumu ya kila siku,katika hali nisiyotarajia mwili ulikuwa unauma utadhani nimepigwa na magongo.
Nikashindwa kutokea kibaruani, kuna mnoko alitaka kujua kulikoni,nikamjibu "achana na mimi" [emoji28][emoji28]
Leo angalau nina "afueni" ingawa koo bado linakwaruza na kuwasha. Homa imekwisha.
 
Ya kwanza walitukosa sasa Billget kaingia chimbo tena na hiyo ndo aliyokuja nayo hatutoki hii,hata wanangu flan hapo 254 wamenambia na huko Nairobi kuna iyo hali pia homa na mafua kwa kwenda mbele
 
Back
Top Bottom