Kuna kama mlipuko wa homa na mafua dsm

Kuna kama mlipuko wa homa na mafua dsm

Chanjo inaweza isizuie kupata kirusi lakini inaweza kuokoa maisha yako kwa kufanya ugonjwa usiwe mkali unapoupata. Kumbuka Omicron ni tofauti sana na wengine waliotangulia na chanjo ilikuwa ya hao waliotangulia.
Hapa kwangu Mimi tu ndo nlipata chanjo ya Covid ya Jansen,mwanzoni kabisa,lakini Sasa muda huu Ni Mimi ndo Nina homa,wenzangu wote,wife na watoto hakuna mwenye homa yeyote
 
Omicron hako ila hakana nguvu sana japo kinaenea sana juzi bibi mkubwa kaumwa tumepima vyote hakuna kitu tukajuwa kidudu kimevamia ila tujihadhari tu hakitishi sana kama lile baba lao la mwaka 2020.

inawezekana pia mkuu
 
Chanjo inaweza isizuie kupata kirusi lakini inaweza kuokoa maisha yako kwa kufanya ugonjwa usiwe mkali unapoupata. Kumbuka Omicron ni tofauti sana na wengine waliotangulia na chanjo ilikuwa ya hao waliotangulia.

Mkuu naomba uzoefu wako ulitumia nini maana niko katika hali ngumu tangu jana jioni naumwa sana
Mafua makali
Kikohozi
Mwili unauma
Kichwa kinauma
Usiku nimetokwa jasho sana
Nameza paracetamol lakini zinanipa nafuu ya muda mfupi tu
Kwenda hospital naogopa nisijekubeba vingine kuleta nyumbani
 
Pole sana. Nililazwa hospitali kwa siku 12. Nilihitaji oxygen, dawa na uangalizi wa karibu. Kama ulimwona Mh Mpango, basi nilikuwa hivyo hivyo. Nilipewa dawa kibao kwa njia ya mshipa. Baadae nilipoendelea vizuri, nikapewa za kumeza. Na zaidi niliombewa sana na wapendwa kanisani. Wengine walifunga kwa ajili yangu. Mungu akupe wepesi.
Mkuu naomba uzoefu wako ulitumia nini maana niko katika hali ngumu tangu jana jioni naumwa sana
Mafua makali
Kikohozi
Mwili unauma
Kichwa kinauma
Usiku nimetokwa jasho sana
Nameza paracetamol lakini zinanipa nafuu ya muda mfupi tu
Kwenda hospital naogopa nisijekubeba vingine kuleta nyumbani
 
Nawacheki tu Hawa viongozi badala ya kufunga anga wanaendesha kupokea wageni time will tell itaondoka na kiongozi mmoja aliyechanja.

China alistahili kupigwa bomu la nuclear
 
Hapo kwenye ku sweat hapo. Upande niliokuwa nalalia kwenye kitanda ulikuwa unakuwa kama umemwagiwa maji... Sijawahi kuona kitu kama hicho tangu nizaliwe.
Ni hatari sana hii una swet mpaka nguo zinaloa kabisa
 
Hata mimi naona imenikamata kweli. Kichw kinauma, mafua makali na mwili nao unauma . Sio poa.
 
Mi nimepona siku 3 hizi tu, ila ilikuwa kupumua shida kwelikweli, hapa mtaani naona wengi wamepatwa na mafua makali. Kinachosaidia Afrika ni Joto tu, hivyo kutoathiri sana mfumo wa upumuaji.
 
Ni kweli hata mimi nimeugua hyo Hali na kubanwa kifua na mafua makali, thank God nimepona nilivoenda hospital nilivokuta Kuna wagonjwa wanashindwa kupumua niligeuza nduki nika ghairi kupima kabisa.
Umetumia dawa gani
 
Back
Top Bottom