Kuna kama mlipuko wa homa na mafua dsm

Kuna kama mlipuko wa homa na mafua dsm

Hivi mmeliona hilo?Kuna hali fulani kama mlipuko wa homa na mafuta kila mahali katika jiji la Dar es Sallam
nikweli, Mimi hapa nna mafua makali na home Kali, hapa natumia AZUMA,na naona pia wengi limewapata Hilo tatizo mtaani
 
😁😁😁
EUkTE.jpg
 
Inawezekana,kuna hospitali moja hapa kariakoo juzi kuna mzimbabwe amefariki hapo,
Inabidi tuchukue tahadhari
 
Aisee ni kweli nimekutana na jamaa walikuwa wanalalamika homa,namfua,kupiga chafya kwa nguvu sana hadi kustua watu.
Hii ya chafya ni jirani yangu mke wake amekuwa anapiga chafya sana hadi kustua na siyo kawaida yake.
Jamaa wanasema hali ya hewa imebadilika .
Mimi binafsi nipo fiti
 
Ndio ngoma inarudi hio!! 3rd wave Omicron. Sema hii haitishi sana. Wameteleza kwenye formula.

Nakumbuka 2019 miezi ya mwishoni Kama hiihii zilikuja post kama hizi hizi humu JF kabla mamlaka zozote Afrika hazijajua chochote kuhusu Corona.


Nikiwa kama mtaalam wa magonjwa ambukizi niliona JF ilitisha sana na vyombo yetu vya ku monitor AFYA ya jamii ni vya hovyo kabisa.
Hii nchi mfumo wa afya wa kusubiri wa gonjwa ndio wapate kutibu..hovyo kabisa..kinga wameitupilia mbali..uwekezaji mkubwa unafanywa kwenye tiba..ikimaanisha wanasubiri waugue watz ili wawatibu.

Ukijenga mahospitali mengi mana yake unawanachi wagonjwa wengi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Dar Kuna mvua mkuu, hafu haya mafua mabaya unabanwa kifua na homa kuwa Kali sana aisee na kulegea mwilini, nadhani huu ni upepo mchafu umepita
Ni hatari, Mimi Hadi nilihisi kifo kimekaribia, joto la mwili lilikuwa juu Sana,na kichwa kuuma, yaan mpaka leo Bado mwili hauna nguvu kabisa
 
Kiherehere Cha keyboard ku sense tu mwenyewe huyo kanishtua nilikuwa hata sijui[emoji23][emoji23]
Hahaha, waga keyboard ziko Sharp sana kuliko ata mtu anaefklia kitu cha kutype
 
Ni kweli hata mimi nimeugua hyo Hali na kubanwa kifua na mafua makali, thank God nimepona nilivoenda hospital nilivokuta Kuna wagonjwa wanashindwa kupumua niligeuza nduki nika ghairi kupima kabisa.
Yaani badala upime ukaamua kula kona!!!!!
 
MZIGO umeingia huoooo.,,[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Wahi nyungu, malimao na tangawizi.
Usisahau kuomba Mungu
 
Back
Top Bottom