Kuna kama mlipuko wa homa na mafua dsm

Kuna kama mlipuko wa homa na mafua dsm

Mimi navyojua ni majuzi tu hapa kulikuwa na joto kali, kwa mvua zilizonyesha na kubadili hali ya hewa lazma magonjwa ya kawaida kama kikohozi na mafua ambayo mara nyingi husindikizwa na homa lazma viwapate watu. Malaria pia sababu ya kuongezeka kwa mazalia ya mbu, Hiki kitu pia si kwa dar tu ni mikoa mingi, hali ya hewa ikibadilika mfano kipindi cha jua kali utakuta watu wana mafua sana na vikohozi sababu ya vumbi au kipindi cha mvua, waathirika wa malaria wanaongezeka. NI magonjwa ya msimu tu sidhani kama ni issue kubwa kama inavyokuzwa humu
 
Kwa Dar hilo ni jambo la kawaida,muda mwingi Dar huwa kuna joto,hizi mvua zilizoanza wiki iliopita tayari zimebadili hali ya hewa,kwahiyo lazima kuwe na magonjwa kama hayo ili mwili ujiweke sawa,cha muhimu tusiache kuchukua tahadhari ya Covid...
 
Dooh kumbe tuko wengi, weekend hii ilikuwa pata shika, joto limepanda panadol haijafua dafu, J3 nauliza walevi wenzangu walikulaje bata kila mmoja anasema alikuwa anaumwa homa /mafua mkali.
Mungu ni mwema itapita tu
Aise ilinitandika kunywa panadol na mseto siku tatu nikapata nafuu na wikiendi nikapiga vyombo hadi asubuhi.

Na sasa niko fiti kama ndio OMICRON ishagonga mwamba tayari
 
Ndio ngoma inarudi hio!! 3rd wave Omicron. Sema hii haitishi sana. Wameteleza kwenye formula.

Nakumbuka 2019 miezi ya mwishoni Kama hiihii zilikuja post kama hizi hizi humu JF kabla mamlaka zozote Afrika hazijajua chochote kuhusu Corona.


Nikiwa kama mtaalam wa magonjwa ambukizi niliona JF ilitisha sana na vyombo yetu vya ku monitor AFYA ya jamii ni vya hovyo kabisa.

Mkuu unakumbukumbu sana tena hiyo kipindi kimara hadi mbezi watu walikuwa wanalalamika sana wakienda hosp hamna ugonjwa acha kabisa kipindi hicho..nilipigwa homa moja matata pamoja na mafua mmh acha kama ilikuwa ni covid basi mungu ndio aliingilia kati
 
Ni hali ya kawaida maana binadamu huwezi kukaa kwa utimamu 100% kikubwa tule vizuri, zoezi, tujikinge na magonjwa yote ambukizwa.
 
Hivi mmeliona hilo?Kuna hali fulani kama mlipuko wa homa na mafuta kila mahali katika jiji la Dar es Sallam
Acha tu, naugulia kitandan, ile nimepiga pen V Na pain killer naona nimekaa sawa
 
kuna dr mmoja anasema omicron ina mutation ambayo ni kipande cha vinasaba kutoka kwenye kirusi cha mafua.......hii mutation imekifanya kirusi kuwa butu kwenye kusababisha maafa lakini imeifanya kuwa na uwezo wa kuambukiza zaidi na hivo ukiugua omicron utaweza kuwaambukiza wengine kwa haraka zaidi lakini usitegemee kupata dalili za kupumua kwa shida,moyo kwenda mbio nk......... fungua link hapo chini👇
covid vs omicron
 
Mgeni karudi tena. Nchi hii bahati mbaya hatupimi. Na hata tukipima, hatuambiani ukweli. Waziri Mkuu amekwishasema Tanzania hakuna hata mgonjwa mmoja wa corona kwa sasa lakini watu wanaumwa mtaani na hospitali. Sasa ni daktari gani atasimama kupingana na PM? Ni linchi la hovyo kabisa. Huko India waliwakuta wasafiri waliotoka Tanzania na Omicron.
 
Back
Top Bottom