Kuna Jambo Uongozi uliopo madarakani usipoangalia linaenda kutokea kama la 1992 kwa Jirani yetu

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,751
21,204
Amani muswano.

Tupo chungu cha tano leo ndugu zangu ni kasi ya ajabu sana hii.

Nafuatilia siasa za jirani zetu hapo Kenya, kuna mambo yanafanyika siyo ya kistaarabu kwa kweli.

Screenshot_2023_0327_172346.jpg

Naona huyu mujamaa makamu wa Rais ndg Rigathi Gachagua hana furaha anapoona wakenya wana amani.

Leo bana kuna shamba la miti lipo eneo la Northlands inasemekana ni la familiai ya Uhuru, sasa huyo makamu wa Rais katuma convoy ya watu wake na watu anaowajua yeye wamevamia na kuanza kukata ovyo miti.

IMG_20230327_173149.jpg
Hilo siyo jambo zuri kwa kiongozi mkubwa wa kitaifa kufanya ubaya unaoonekana kwa raia kuna baadhi ya wakenya wanasema huyu jamaa anataka kufanya kama mapigano ya kikabila ya mwaka 1992.

Kama jirani mwema tu hapa ambaye jeshi letu la police linasifiwa kwa kutenda wema likija kunikamata nasema ndg makamu wa Rais Gachagua hicho unachokifanya hakikubariki.

STOP IT!.
 
Wale walioshindwa watulie tu, wenzao wafanye kazi ya kuwaletea wakenya maendeleo. Walishindwa kwenye kura badala watulie wanaleta fujo, wakiumizwa wajilaumu wao.

Hapa kwetu bongo uchaguzi ulipoisha tu wapinzani walipumzishwa watulie mpaka juzikati waliporuhusiwa kufanya mambo yao kistaarabu bila ghasia.

Wapinzani wa bongo hawana munkari wa kuandamana andamana walishajifunza kufungiwa kwao. Hata hao wapinzani wa kenya wanatakiwa wafungiwe kwa muda watulie kuleta vurugu kwa wakenya wasifaidika na siasa za vurugu. Ruto piga marufuku hayo maandamano
 
Ile ya Rwanda sidhani kama itakuja kutokea tena, watu laki moja ndani ya siku 90 za hofu na mashaka.

Gachuma anafanya siasa za kishamba, , ni vile tu katiba imnampiga pini.

Naamini mahakama itafanya kazi yake vizuri , Kenya huo mhimili japo ni corrupt lakini upo huru.
 
Ile ya Rwanda sidhani kama itakuja kutokea tena, watu laki moja ndani ya siku 90 za hofu na mashaka.
Gachuma anafanya siasa za kishamba, , ni vile tu katiba imnampiga pini. Naamini mahakama itafanya kazi yake vizuri , Kenya huo mhimili japo ni corrupt lakini upo huru.
"Gachagua" kweli huyu mwamba ana roho mbaya sana na inasemekana ndiye alipanga uvamizi wa shamba la mstaafu Uhuru.

Nimeandika pale juu, ambapo kulitokea vita ya wenyewe kwa wenyewe ambapo ilileta msuguano sana, so hiki kinachotengenezwa na huu uongozi yetu macho!.
 
Ndo maana tunasisitiza katiba wazee, huyo makamu pamoja na Roho mbaya yake hawezi kufanya political damage akafanikiwa, mahakama itamnasq tu na atawajibika, ' Uhuru anaweza kuwa wa kwanza kumshitaki kwa hiyo misconduct aliyofanya..
 
Ile ya Rwanda sidhani kama itakuja kutokea tena, watu laki moja ndani ya siku 90 za hofu na mashaka.
Gachuma anafanya siasa za kishamba, , ni vile tu katiba imnampiga pini .
Naamini mahakama itafanya kazi yake vizuri , Kenya huo mhimili japo ni corrupt lakini upo huru.
Haya hayako mbali Sna na alicokua akifanya JIWE MAGU FOOL Ukabila ukabila mtupu unanukia hpo KENYA
 
Uchaguzi ulipofanyika kwa mbwembwe kedekede hadi tukaambiwa na kina Fatma Karume na Maria Sarungi kuwa kuna cha kujifunza Kenya…sikuwaelewa kipindi kile…kumbe haya ndo wanatamani yatokee huku
KATIBA NA MFUMO WETU UNATUFAA SANA TUSIDANGANYIKE, TUSIICHOKONOE KATIBA YETU HATA KIDOGO, TUTAKUJA WEKA VIFUNGU VIJE KUTUKOSTI NA TAIFA NA UTAIFA WETU NA MUUNGANO WETU USAMBARATIKE KIPUUZI KABISA!
 
Uchaguzi ulipofanyika kwa mbwembwe kedekede hadi tukaambiwa na kina Fatma Karume na Maria Sarungi kuwa kuna cha kujifunza Kenya…sikuwaelewa kipindi kile…kumbe haya ndo wanatamani yatokee huku
Mkuu uchaguzi ulikuwa muswano tatizo la Kenya ni ukabila, means kuna watu, majority power wakisema huyu hapana inakuwa kama ccm, so issue haikuwa iwe kubwa kiasi hiko endapo takwa la muzee RAO la kutaka saver ziwekwe wazi kama miaka mingine.
 
Sasa kumbe issue yao haikuwa katiba bali walipaswa watafute namna yakusort tatizo la ukabila kwanza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom