Siku 60 za Rais Samia madarakani: Tunakushukuru sana kwa uongozi wako makini, hakika umerejesha tumaini na furaha

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,089
Mheshimiwa Rais.

Awali ya yote nakutakia Amani ya Mwenyezi Mungu BWANA wa Majeshi na Nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nipende kuchukua fursa hii kukupongeza kwa uchapakazi makini, kwa uongozi thabiti na serikali inayosikia na kuzingatia maoni, matakwa na maslahi ya wananchi. Kwa hakika uongozi wako umekuwa ni faraja kubwa na matumaini makubwa sana kwetu hasa ukizingatia aina ya utawala uliopita, utawala ambao haukujali vilio vya wananchi, utawala uliojaa uonevu, propaganda na matumizi mabaya kabisa ya madaraka.

Mheshimiwa Rais nafahamu kuwa haya unayoyatekeleza ni wajibu wako, lakini sisi Watanzania ni waungwana, kwa hiyo si vibaya kuonyesha uungwana wetu kwa kushukuru. Hata kwenye vitabu vitakatifu tumefundishwa kuwa kushukuru ni jambo zuri na hata Mwenyezi Mungu amesema kuwa Mwenye kumshukuru basi humuongezea. Kwa hiyo mheshimiwa rais tunashukuru kwa aina ya uongozi wako, uongozi uliojaa utu, huruma, uzalendo, haki na vision kubwa ya maendeleo

Tangu umechukua uongozi baada ya kifo cha rais aliyekutangulia Ndugu Magufuli yapata siku 60, lakini katika hizo siku umefanya mambo makubwa, yenye manufaa sana kwa nchi yetu na hapa chini nitaorodhesha machache

1. Ndani ya Siku 60 za uongozi wako, umeshawaondolea wananchi riba (retention fee) ya 6% kwenye mikopo yao ya elimu ya juu.
Mheshimiwa hili ulilolifanya ni jambo zuri mno, hii riba ndiyo iliyokuwa ikiwafanya watu walipe deni miaka na miaka lakini lisiishe maana deni lilikuwa inaendelea kujiaccumulate hata baada ya kulipunguza. Hakika tunakushukuru sana mheshimiwa rais kwa uamuzi huu wa busara

2. Umetangaza Ajira 40000 kwa mwaka huu, na umeshatoa kibali cha ajira takriban 10000 kwanza.

Mheshimiwa rais ubarikiwe sana, hili ni jambo kubwa, vijana wetu walikuwa wanatangatanga mitaani, ajira hakuna, mzigo wa kulea hawa watoto uliendelea kuwa mzigo kwa familia ambazo zimeshatumia kila senti na ndululu kuwasomesha lakini mwishowe wanakosa ajira. Hili suala kwa hakika lilikuwa linayafanya maisha yazidi kuwa magumu lakini umetusaidia sana, na nakuomba uendelee kutoa ajira kadri hali ya uchumi itakavyoboreka

3. Mheshimiwa rais, ndani ya siku 60, umetusaidia kuongeza umri wa mtoto kunufaika na NHIF kutoka miaka 18 hadi 21.
Hili jambo limekuwa msaada mkubwa kwetu wananchi, hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa vijana wa miaka 18 kimsingi wanakuwa bado hawajaanza kusimama vizuri kwa miguu yao, kwa hiyo zigo la matibabu yao lilikuwa linarudi tena kwa mzazi au mlezi, kitendo chako cha kuongeza umri wa kunufaika na Bima ya Afya hadi miaka 21 chini ya cover ya mzazi/mlezi kimeleta unafuu mkubwa kwa hawa vijana na familia zao kiujumla

4. Mheshimiwa ndani ya siku 60 umesaidia kurudisha bei za vifurushi vya internet kuwa angalau kama zamani, na umefungulia mitandao iwe huru.

Nikupongeze sana mheshimiwa rais kwa Intervention yako, Serikali iliyopita ya Magufuli ilituhadaa wananchi kuwa inakwenda kukaa na makampuni ya simu ili yashushe bei za vifurushi, kilichotokea hapo ni uwongo mtupu, bei zilipanda na sisi wananchi tukaumia sana, maana zilikuwa ni bei ambazo majority ya wananchi wasingeweza kuzimudu. Wewe umetusaidia kuzirudisha angalau kwa bei ya awali. Nafahamu kuwa licha ya kuwa yapo makampuni korofi yanajivutavuta, lakini hata yenyewe yameshusha kidogo, na yapo yaliyotii kabisa agizo lako, kwetu sisi wananchi tunasema hili si haba, na tunaomba hayo makampuni korofi yafuatiliwe bila kuathiri uwekezaji wao ili iwepo win-win.

Pia mheshimiwa rais, ndani ya siku zako 60, Umeachia mitandao iwe huru zaidi, Leo hii hatuhitaji rena VPN kuipata twitter, na wale waliokuwa na online TV umewaachia huru. Kwa hakika hii ni hatua muhimu sana ya kulinda demokrasia yetu na uhuru wa habari.

5.Mheshimiwa rais, ndani ya siku zako 60 Umeachia huru wafungwa wa waliobambikiziwa kesi.

Miongoni mwao wamo wale waliowekwa ndani kwa sababu za Kisiasa, mheshimiwa jana peke yake umeachia huru wafungwa takriban 147 ambao makosa yao yalikuwa ni ya kubumba, hawa walibambikiziwa kesi mbayambaya za uhujumu uchumi ili waozee jela kwa sababu za ajabuajabu kabisa ikiwemo ugomvi wa kisiasa tu.

6. Ndani ya siku 60, umeonyesha uongozi makini wenye kuzingatia sayansi kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa korona.

Kiukweli kabisa, Nchi yetu ilifanikiwa kupata mafanikio katika wimbi la kwanza kwa sababu tulipigana katika angle tatu, tulipambana kwa kufuata recommendations kadha wa kadha za kisayansi, pia tukawa tunatumia na njia zetu za asili bila kusahau spiritual front. Lakini kwenye wimbi la pili tukawa wabishi, sayansi tukaikataa, tukapromote njia zetu za asili peke yake na huku upande wa Spiritual tukawa wanafiki zaidi, Tukataka kulitumia Jina la Mungu kuficha kutowajibika kwetu, matokeo yake wimbi la pili likawa disaster sana.

Nakupongeza mheshimiwa raisi kwa kurudisha common sense kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huu, ba ushauri wangu ni kuwa lazima tuendelee kupambana na huu ugonjwa kisayansi, bila kusahau njia zetu za asili na bila kumsahau Mungu, na tuwe genuine kabisa, tusimtumie Mungu kisiasa ili kuficha kutowajibika kwetu. Nakupongeza kwa kupromote barakoa badala ya kuzibeza.

7. Ndani ya siku 60 umeshawezesha Mahindi yetu kuendelea kupata soko Kenya na Umeweza kuingia mkataba wa kujenga bomba la gesi ili tuwauzie Wakenya.

Mheshimiwa, wote tunajua kuwa Wakenya walikerwa na kauli ya rais Magufuli juu ya kuwakebehi kwa lockdown waliyoweka kwao, na Magufuli akajitapa kuwauzia chakula kwa bei ghali, kwa hiyo Wakenya wakafanya retaliation. Ila kutokana na uwezo wako mkubwa kwenye diplomasia umewezesha kutatua hilo tatizo na sasa mahindi yetu yanapata soko huko Kenya, wakulima wetu wananufaika.
Pia ndani ya siku 60 umetia saini mkataba wa kujenga bomba la gesi ili tuwauzie Wakenya gesi. Kwa hakika hili ni hambo kubwa kiuchumi, litakapokamilika litasaidia kukuza uchumi wetu.

8. Mheshimiwa, ndani ya siku 60 umeonyesha nia kuzungumza na wapinzani na kujenga mazibgira ya siasa za kuaminiana katika spirit ya kupingana bila kupigana.

Mheshimiwa rais, chini ya utawala wa Rais Magufuli, siasa za nchi hii zikitawaliwa na ubabe, uporaji wa haki ya wananchi kuchagua viongozi wao kwa haki(rejea chaguzi za serikali za mitaa), polisi kuvamia ofisi za wapinzani, kuvuruga mikutano yao hata ile ya ndani, kubambikiza kesi wapinzani na hata wengine kupigwa risasi mchana kweupe bila uchunguzi wowote. Mheshimiwa, sisi tunakupongeza kwa kutaka au kukubali mazungumzo na wapinzani, maana at the end of the day, hii nchi ni yetu sote na ni lazima kila chama kiwe na haki ya kuoperate nchini bila kufanyiana fujo na vurugu.

9. Ndani ya siku 60, umetuonyesha kuwa uko tayari kung'oa Washenzi na waonevu katika nyadhifa za utumishi.
Kitendo cha kumchunguza yule bwana wa bandari na yule kijana mkuu wa wilaya, ni message kali kwa viongozi wengine kuwa hauko tayari kuvumilia ushenzi. Nimependezwa na approach yako ya kuwachunguza na hatimaye kuchukua hatua, maana haitoshi tu kumtumbua mtu, bali atumbuliwe huku ukiwepo ushahidi wa kutosha kumfikisha katika mkono wa sheria, lakini pia inalinda haki yake kama labda anasingiziwa.

10. Mheshimiwa rais, ndani ya siku 60, umeagiza wale walikuwa na elimu ya darasa la saba waliofukuzwa kazi bila kulipwa stahiki zao walipwe

Mheshimiwa hili ni jambo zuri, ni jambo la haki, maana wale ni wanadamu, wana haki zao za msingi, kitendo cha wewe kuzitambua, ni jambo la faraja sana.

OMBI MAALUM KWAKO MHESHIMIWA RAIS
1. Mheshimiwa Rais, Mwenyezi Mungu amekuweka katika hiyo nafasi, basi tunaomba sisi wananchi utujengee MIFUMO mizuri ili kesho na keshokutwa upo au haupo tuweze kusema kuwa umetuacha tukiwa na HAKI zaidi katika nchi, tukiwa HURU zaidi katika nchi, Tukiweza KUWAWAJIBISHA Viongozi wetu zaidi katika nchi, TUKINUFAIKA na rasilimali zetu zaidi katika nchi.

Na hilo halitiwezekana chini ya katiba hii ya sasa, Hii ni katiba ya KIDIKTETA yaani hata wewe hapo mheshimiwa rais ukiamua kuwa Dikteta katiba hii inakupa ushirikiano mkubwa. Sasa tunaomba utupe MUAFAKA mzuri zaidi wa Kitaifa, na Muafaka huo ni Katiba mpya iliyo nzuri na bora. Mhwshimiwa hili ndo litatufanya tukukumbuke zaidi kuliko hata kama utaweka mabomba ya asali katika kila nyumba!.

2. Pili naomba wale waliovunjiwa nyumba zao Kimara-Mbezi, serikali yako iwaangalie, maana Serikali iliyopita ilionyesha ubaguzi kwenye kutekeleza zoezi la ubomoaji, wale wa Mwanza ilisema wasibomolewe eti kwa sababu walimpa kura Magufuli kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, ila wale wa Kimara-Mbezi serikali ikawabomolea bila kujali kuwa walikuwa na Stop order ya Mahakama kuzuia ubomoaji huo. Mheshimiwa Rais naomba uwape kifuta machozi wananchi wa Kimara Mbezi maana kuna ukatili mkubwa na double standard kubwa sana ilifanyika pale.

3. Tunaomba zile sheria za kidhalimu, zenye lengo la kuupalilia udikteta nchini zifanyiwe marekebisho au ziondolewe kabisa. Mheshimiwa rais tunaomba uondoe sheria inayowapa kinga Spika, Naibu wake na Waziri mkuu Kinga ya kutoshitakiwa, hawa wanataka wasishitakiwe kwa nini?, pia sheria za mitandao, vyombo vya habari na kanuni zake zibadirishwe. Hizo sheria siyo conducive kujenga Taifa la watu wenye FIKRA huru kutoa maoni yao kikamilifu, na hazilindi wala kupanua Demkrasia yetu.

4. Pia Mheshimiwa Rais, nchini katika majela yetu kumejaa Masheikh wengi ambao wamo ndani kwa kesi za kubambikiza ikiwemo Masheikh wa UAMSHO na wengine wengi nchini, hawa bado hawajaachiwa, nakuomba Masheikh hawa wasio na hatia nao waachiwe kama wafungwa wengine waliobambikiziwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kisiasa wanavyoachiwa.

Mwisho kabisa nimalize kwa kusema. Mheshimwa, Upo kwenye right track sana, yaani uongozi wako ni mzuri na makini mno endelea kuchapa kazi

Kazi iendelee!
 
Hiyo ndio maana halisi ya kauli ya "Nakwenda kuifungua nchi".

Mwalimu Nyerere alisema, "Kitendo chochote cha kujiongezea uhuru wako, japo hakikuongezei shibe wala afya, ni kitendo cha maendeleo"

Hatuna habari kama tupo uchumi wa kati, wa pembeni au wa chini bali Taifa linafurahia kwa kurejeshewa matumaini kadha wa kadha ikiwemo uhuru wa kua na maoni huru hata kama yanapingana na kiongozi/viongozi wakuu wa nchi

Kazi iendelee
 
Mheshimiwa Rais.
Awali ya yote nakutakia Amani ya Mwenyezi Mungu BWANA wa Majeshi na Nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nipende kuchukua fursa hii kukupongeza kwa uchapakazi makini, kwa uongozi thabiti na serikali inayosikia na kuzingatia maoni, matakwa na maslahi ya wananchi. Kwa hakika uongozi wako umekuwa ni faraja kubwa na matumaini makubwa sana kwetu hasa ukizingatia aina ya utawala uliopita, utawala ambao haukujali vilio vya wananchi, utawala uliojaa uonevu, propaganda na matumizi mabaya kabisa ya madaraka.

Mheshimiwa Rais nafahamu kuwa haya unayoyatekeleza ni wajibu wako, lakini sisi Watanzania ni waungwana, kwa hiyo si vibaya kuonyesha uungwana wetu kwa kushukuru. Hata kwenye vitabu vitakatifu tumefundishwa kuwa kushukuru ni jambo zuri na hata Mwenyezi Mungu amesema kuwa Mwenye kumshukuru basi humuongezea. Kwa hiyo mheshimiwa rais tunashukuru kwa aina ya uongozi wako, uongozi uliojaa utu, huruma, uzalendo na haki na vision kubwa ya maendeleo

Tangu umechukua uongozi baada ya kifo cha rais aliyekutangulia Ndugu Magufuli yapata siku 60, lakini katika hizo siku umefanya mambo makubwa, yenye manufaa sana kwa nchi yetu na hapa chini nitaorodhesha machache

1. Ndani ya Siku 60 za uongozi wako, umeshawaondolea riba(retention fee) wananchi ya 6% kwenye mikopo yao ya elimu ya juu.
Mheshimiwa hili ulilolifanya ni jambo zuri mno, hii riba ndiyo iliyokuwa ikiwafanya watu walipe deni miaka na miaka lakini lisiishe maana deni lilikuwa inaendelea kujiaccumulate hata baada ya kulipunguza. Hakika tunakushukuru sana mheshimiwa rais kwa uamuzi huu wa busara

2. Umetangaza Ajira 40000 kwa mwaka huu, na umeshatoa kibali cha ajira takriban 10000 kwanza.

Mheshimiwa rais ubarikiwe sana, hili ni jambo kubwa, vijana wetu walikuwa wanatangatanga mitaani, ajira hakuna, mzigo wa kulea hawa watoto uliendelea kuwa mzigo kwa familia ambazo zimeshatumia kila senti na ndululu kuwasomesha lakini mwishowe wanakosa ajira. Hili suala kwa hakika lilikuwa linayafanya maisha yazidi kuwa magumu lakini umetusaidia sana, na nakuomba uendelee kutoa ajira kadri hali ya uchumi itakavyoboreka

3.Mheshimiwa rais, ndani ya siku 60, umetusaidia kuongeza umri wa mtoto kunufaika na NHIF kutoka miaka 18 hadi 21.
Hili jambo limekuwa msaada mkubwa kwetu wananchi, hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa vijana wa miaka 18 kimsingi wanakuwa bado hawajaanza kusimama vizuri kwa miguu yao, kwa hiyo zigo la matibabu yao lilikuwa linarudi tena kwa mzazi au mlezi, kitendo chako cha kuongeza umri wa kunufaika na Bima ya Afya hadi miaka 21 chini ya cover ya mzazi/mlezi kimeleta unafuu mkubwa kwa hawa vijana na familia zao kiujumla

4. Mheshimiwa ndani ya siku 60 umesaidia kurudisha bei za vifurushi vya internet kuwa angalau kama zamani, na umefungulia mitandao iwe huru.

Nikupongeze sana mheshimiwa rais kwa Intervention yako, Serikali iliyopita ya Magufuli ilituhadaa wananchi kuwa inakwenda kukaa na makampuni ya simu ili yashushe bei za vifurushi, kilichotokea hapo ni uwongo mtupu, bei zilipanda na sisi wananchi tukaumia sana, maana zilikuwa ni bei ambazo majority ya wananchi wasingeweza kuzimudu. Wewe umetusaidia kuzirudisha angalau kwa bei ya awali. Nafahamu kuwa licha ya kuwa yapo makampuni korofi yanajivutavuta, lakini hata yenyewe yameshusha kidogo, na yapo yaliyotii kabisa agizo lako, kwetu sisi wananchi tunasema hili si haba, na tunaomba hayo makampuni korofi yafuatiliwe bila kuathiri uwekezaji wao ili iwepo win-win
Pia mheshimiwa rais, ndani ya siku zako 60, Umeachia mitandao iwe huru zaidi, Leo hii hatuhitaji rena VPN kuipata twitter, na wale waliokuwa na online TV umewaachia huru. Kwa hakika hii ni hatua muhimu sana ya kulinda demokrasia yetu na uhuru wa habari

5.Mheshimiwa rais, ndani ya siku zako 60 Umeachia huru wafungwa wa waliobambikiziwa kesi

Miongoni mwao wamo wale waliowekwa ndani kwa sababu za Kisiasa, mheshimiwa Jana peke yake umeachia huru wafungwa takriban 147 ambao makosa yao yalikuwa ni ya kubumba, hawa walibambikiziwa kesi mbayambaya za uhujumu uchumi ili waozee jela kwa sababu za ajabuajabu kabisa ikiwemo ugomvi wa kisiasa tu.

6. Ndani ya siku 60, umeonyesha uongozi makini wenye kuzingatia sayansi kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa korona.

Kiukweli kabisa, Nchi yetu ilifanikiwa kupata mafanikio katika wimbi la kwanza kwa sababu tulipigana katika angle tatu, tulipambana kwa kufuata recommendations kadha wa kadha za kisayansi, pia tukawa tunatumia na njia zetu za asili bila kusahau spiritual front. Lakini kwenye wimbi la pili tukawa wabishi, sayansi tukaikataa, tukapromote njia zetu za asili peke yake na huku upande wa Spiritual tukawa wanafiki zaidi, Tukataka kulitumia Jina la Mungu kuficha kutowajibika kwetu, matokeo yake wimbi la pili likawa disaster sana. Nakupongeza mheshimiwa raisi kwa kurudisha common sense kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huu, ba ushauri wangu ni kuwa lazima tuendelee kupambana na huu ugonjwa kisayansi, bila kusahau njia zetu za asili na bila kumsahau Mungu, na tuwe genuine kabisa, tusimtumie Mungu kisiasa ili kuficha kutowajibika kwetu. Nakupongeza kwa kupromote barakoa badala ya kuzibeza.

7. Ndani ya siku 60 umeshawezesha Mahindi yetu kuendelea kupata soko Kenya na Umeweza kuingia mkataba wa kujenga bomba la gesi ili tuwauzie Wakenya.

Mheshimiwa, wote tunajua kuwa Wakenya walikerwa na kauli ya rais Magufuli juu ya kuwakebehi kwa lockdown waliyoweka kwao, na Magufuli akajitapa kuwauzia chakula kwa bei ghali, kwa hiyo Wakenya wakafanya retaliation. Ila kutokana na uwezo wako mkubwa kwenye diplomasia umewezesha kutatua hilo tatizo na sasa mahindi yetu yanapata soko huko Kenya, wakulima wetu wananufaika.
Pia ndani ya siku 60 umetia saini mkataba wa kujenga bomba la gesi ili tuwauzie Wakenya gesi. Kwa hakika hili ni hambo kubwa kiuchumi, litakapokamilika litasaidia kukuza uchumi wetu

8. Mheshimiwa, ndani ya siku 60 umeonyesha nia kuzungumza na wapinzani na kujenga mazibgira ya siasa za kuaminiana katika spirit ya kupingana bila kupigana

Mheshimiwa rais, chini ya utawala wa Rais Magufuli, siasa za nchi hii zikitawaliwa na ubabe, uporaji wa haki ya wananchi kuchagua viongozi wao kwa haki(rejea chaguzi za serikali za mitaa), polisi kuvamia ofisi za wapinzani, kuvuruga mikutano yao hata ile ya ndani, kubambikiza kesi wapinzani na hata wengine kupigwa risasi mchana kweupe bila uchunguzi wowote. Mheshimiwa, sisi tunakupongeza kwa kutaka au kukubali mazungumzo na wapinzani, maana at the end of the day, hii nchi ni yetu sote na ni lazima kila chama kiwe na haki ya kuoperate nchini bila kufanyiana fujo na vurugu.

9. Ndani ya siku 60, umetuonyesha kuwa uko tayari kung'oa Washenzi na waonevu katika nyadhifa za utumishi.
Kitendo cha kumchunguza yule bwana wa bandari na yule kijana mkuu wa wilaya, ni message kali kwa viongozi wengine kuwa hauko tayari kuvumilia ushenzi. Nimependezwa na approach yako ya kuwachunguza na hatimaye kuchukua hatua, maana haitoshi tu kumtumbua mtu, bali atumbuliwe huku ukiwepo ushahidi wa kutosha kumfikisha katika mkono wa sheria, lakini pia inalinda haki yake kama labda anasingiziwa.

10. Mheshimiwa rais, ndani ya siku 60, umeagiza wale walikuwa na elimu ya darasa la saba waliofukuzwa kazi bila kulipwa stahiki zao walipwe

Mheshimiwa hili ni jambo zuri, ni jambo la haki, maana wale ni wanadamu, wana haki zao za msingi, kitendo cha wewe kuzitambua, ni jambo la faraja sana

OMBI MAALUM KWAKO MHESHIMIWA RAIS

1. Mheshimiwa Rais, Mwenyezi Mungu amekuweka katika hiyo nafasi, basi tunaomba sisi wananchi utujengee MIFUMO mizuri ili kesho na keshokutwa upo au haupo tuweze kusema kuwa umetuacha tukiwa na HAKI zaidi katika nchi, tukiwa HURU zaidi katika nchi, Tukiweza KUWAWAJIBISHA Viongozi wetu zaidi katika nchi, TUKINUFAIKA na rasilimali zetu zaidi katika nchi.

Na hilo halitiwezekana chini ya katiba hii ya sasa, Hii ni katiba ya KIDIKTETA yaani hata wewe hapo mheshimiwa rais ukiamua kuwa Dikteta katiba hii inakupa ushirikiano mkubwa. Sasa tunaomba utupe MUAFAKA mzuri zaidi wa Kitaifa, na Muafaka huo ni Katiba mpya iliyo nzuri na bora. Mhwshimiwa hili ndo litatufanya tukukumbuke zaidi kuliko hata kama utaweka mabomba ya asali katika kila nyumba!.

2. Pili naomba wale waliovunjiwa nyumba zao Kimara-Mbezi, serikali yako iwaangalie, maana Serikali iliyopita ilionyesha ubaguzi kwenye kutekeleza zoezi la ubomoaji, wale wa Mwanza ilisema wasibomolewe eti kwa sababu walimpa kura Magufuli kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, ila wale wa Kimara-Mbezi serikali ikawabomolea bila kujali kuwa walikuwa na Stop order ya Mahakama kuzuia ubomoaji huo. Mheshimiwa Rais naomba uwape kifuta machozi wananchi wa Kimara Mbezi maana kuna ukatili mkubwa na double standard kubwa sana ilifanyika pale.

3. Tunaomba zile sheria za kidhalimu, zenye lengo la kuupalilia udikteta nchini zifanyiwe marekebisho au ziondolewe kabisa. Mheshimiwa rais tunaomba uondoe sheria inayowapa kinga Spika, Naibu wake na Waziri mkuu Kinga ya kutoshitakiwa, hawa wanataka wasishitakiwe kwa nini?, pia sheria za mitandao, vyombo vya habari na kanuni zake zibadirishwe. Hizo sheria siyo conducive kujenga Taifa la watu wenye FIKRA huru kutoa maoni yao kikamilifu, na hazilindi wala kupanua Demkrasia yetu

4. Pia Mheshimiwa Rais, nchini katika majela yetu kumejaa Masheikh wengi ambao wamo ndani kwa kesi za kubambikiza ikiwemo Masheikh wa UAMSHO na wengine wengi nchini, hawa bado hawajaachiwa, nakuomba Masheikh hawa wasio na hatia nao waachiwe kama wafungwa wengine waliobambikiziwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kisiasa wanavyoachiwa.

Mwisho kabisa nimalize kwa kusema.
Mheshimwa, Upo kwenye right track sana, yaani uongozi wako ni mzuri na makini mno endelea kuchapa kazi

Kazi iendelee!
Kuna watu wanafyonza wakati wanasoma hili bandiko.. ila kwa kweli walau nchi imetulia tulia sasa looh !!
 
Atuletee Katiba Mpya hayo yote uliyoandika hayatajirudia, vinginevyo ataondoka yeye aje mwingine turudi tulipotoka.

Hao masheikh wenu nao iachieni mahakama ifanye kazi yake, sio kumtumia wa dini yenu awaachie huru hata kama walikuwa na hatia, hii nchi ina sheria zake ziheshimiwe.
 
Mheshimiwa Rais.

Awali ya yote nakutakia Amani ya Mwenyezi Mungu BWANA wa Majeshi na Nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nipende kuchukua fursa hii kukupongeza kwa uchapakazi makini, kwa uongozi thabiti na serikali inayosikia na kuzingatia maoni, matakwa na maslahi ya wananchi. Kwa hakika uongozi wako umekuwa ni faraja kubwa na matumaini makubwa sana kwetu hasa ukizingatia aina ya utawala uliopita, utawala ambao haukujali vilio vya wananchi, utawala uliojaa uonevu, propaganda na matumizi mabaya kabisa ya madaraka.

Mheshimiwa Rais nafahamu kuwa haya unayoyatekeleza ni wajibu wako, lakini sisi Watanzania ni waungwana, kwa hiyo si vibaya kuonyesha uungwana wetu kwa kushukuru. Hata kwenye vitabu vitakatifu tumefundishwa kuwa kushukuru ni jambo zuri na hata Mwenyezi Mungu amesema kuwa Mwenye kumshukuru basi humuongezea. Kwa hiyo mheshimiwa rais tunashukuru kwa aina ya uongozi wako, uongozi uliojaa utu, huruma, uzalendo, haki na vision kubwa ya maendeleo

Tangu umechukua uongozi baada ya kifo cha rais aliyekutangulia Ndugu Magufuli yapata siku 60, lakini katika hizo siku umefanya mambo makubwa, yenye manufaa sana kwa nchi yetu na hapa chini nitaorodhesha machache

1. Ndani ya Siku 60 za uongozi wako, umeshawaondolea wananchi riba(retention fee) ya 6% kwenye mikopo yao ya elimu ya juu.
Mheshimiwa hili ulilolifanya ni jambo zuri mno, hii riba ndiyo iliyokuwa ikiwafanya watu walipe deni miaka na miaka lakini lisiishe maana deni lilikuwa inaendelea kujiaccumulate hata baada ya kulipunguza. Hakika tunakushukuru sana mheshimiwa rais kwa uamuzi huu wa busara

2. Umetangaza Ajira 40000 kwa mwaka huu, na umeshatoa kibali cha ajira takriban 10000 kwanza.

Mheshimiwa rais ubarikiwe sana, hili ni jambo kubwa, vijana wetu walikuwa wanatangatanga mitaani, ajira hakuna, mzigo wa kulea hawa watoto uliendelea kuwa mzigo kwa familia ambazo zimeshatumia kila senti na ndululu kuwasomesha lakini mwishowe wanakosa ajira. Hili suala kwa hakika lilikuwa linayafanya maisha yazidi kuwa magumu lakini umetusaidia sana, na nakuomba uendelee kutoa ajira kadri hali ya uchumi itakavyoboreka

3.Mheshimiwa rais, ndani ya siku 60, umetusaidia kuongeza umri wa mtoto kunufaika na NHIF kutoka miaka 18 hadi 21.
Hili jambo limekuwa msaada mkubwa kwetu wananchi, hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa vijana wa miaka 18 kimsingi wanakuwa bado hawajaanza kusimama vizuri kwa miguu yao, kwa hiyo zigo la matibabu yao lilikuwa linarudi tena kwa mzazi au mlezi, kitendo chako cha kuongeza umri wa kunufaika na Bima ya Afya hadi miaka 21 chini ya cover ya mzazi/mlezi kimeleta unafuu mkubwa kwa hawa vijana na familia zao kiujumla

4. Mheshimiwa ndani ya siku 60 umesaidia kurudisha bei za vifurushi vya internet kuwa angalau kama zamani, na umefungulia mitandao iwe huru.

Nikupongeze sana mheshimiwa rais kwa Intervention yako, Serikali iliyopita ya Magufuli ilituhadaa wananchi kuwa inakwenda kukaa na makampuni ya simu ili yashushe bei za vifurushi, kilichotokea hapo ni uwongo mtupu, bei zilipanda na sisi wananchi tukaumia sana, maana zilikuwa ni bei ambazo majority ya wananchi wasingeweza kuzimudu. Wewe umetusaidia kuzirudisha angalau kwa bei ya awali. Nafahamu kuwa licha ya kuwa yapo makampuni korofi yanajivutavuta, lakini hata yenyewe yameshusha kidogo, na yapo yaliyotii kabisa agizo lako, kwetu sisi wananchi tunasema hili si haba, na tunaomba hayo makampuni korofi yafuatiliwe bila kuathiri uwekezaji wao ili iwepo win-win
Pia mheshimiwa rais, ndani ya siku zako 60, Umeachia mitandao iwe huru zaidi, Leo hii hatuhitaji rena VPN kuipata twitter, na wale waliokuwa na online TV umewaachia huru. Kwa hakika hii ni hatua muhimu sana ya kulinda demokrasia yetu na uhuru wa habari

5.Mheshimiwa rais, ndani ya siku zako 60 Umeachia huru wafungwa wa waliobambikiziwa kesi

Miongoni mwao wamo wale waliowekwa ndani kwa sababu za Kisiasa, mheshimiwa Jana peke yake umeachia huru wafungwa takriban 147 ambao makosa yao yalikuwa ni ya kubumba, hawa walibambikiziwa kesi mbayambaya za uhujumu uchumi ili waozee jela kwa sababu za ajabuajabu kabisa ikiwemo ugomvi wa kisiasa tu.

6. Ndani ya siku 60, umeonyesha uongozi makini wenye kuzingatia sayansi kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa korona.

Kiukweli kabisa, Nchi yetu ilifanikiwa kupata mafanikio katika wimbi la kwanza kwa sababu tulipigana katika angle tatu, tulipambana kwa kufuata recommendations kadha wa kadha za kisayansi, pia tukawa tunatumia na njia zetu za asili bila kusahau spiritual front. Lakini kwenye wimbi la pili tukawa wabishi, sayansi tukaikataa, tukapromote njia zetu za asili peke yake na huku upande wa Spiritual tukawa wanafiki zaidi, Tukataka kulitumia Jina la Mungu kuficha kutowajibika kwetu, matokeo yake wimbi la pili likawa disaster sana. Nakupongeza mheshimiwa raisi kwa kurudisha common sense kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huu, ba ushauri wangu ni kuwa lazima tuendelee kupambana na huu ugonjwa kisayansi, bila kusahau njia zetu za asili na bila kumsahau Mungu, na tuwe genuine kabisa, tusimtumie Mungu kisiasa ili kuficha kutowajibika kwetu. Nakupongeza kwa kupromote barakoa badala ya kuzibeza.

7. Ndani ya siku 60 umeshawezesha Mahindi yetu kuendelea kupata soko Kenya na Umeweza kuingia mkataba wa kujenga bomba la gesi ili tuwauzie Wakenya.

Mheshimiwa, wote tunajua kuwa Wakenya walikerwa na kauli ya rais Magufuli juu ya kuwakebehi kwa lockdown waliyoweka kwao, na Magufuli akajitapa kuwauzia chakula kwa bei ghali, kwa hiyo Wakenya wakafanya retaliation. Ila kutokana na uwezo wako mkubwa kwenye diplomasia umewezesha kutatua hilo tatizo na sasa mahindi yetu yanapata soko huko Kenya, wakulima wetu wananufaika.
Pia ndani ya siku 60 umetia saini mkataba wa kujenga bomba la gesi ili tuwauzie Wakenya gesi. Kwa hakika hili ni hambo kubwa kiuchumi, litakapokamilika litasaidia kukuza uchumi wetu

8. Mheshimiwa, ndani ya siku 60 umeonyesha nia kuzungumza na wapinzani na kujenga mazibgira ya siasa za kuaminiana katika spirit ya kupingana bila kupigana

Mheshimiwa rais, chini ya utawala wa Rais Magufuli, siasa za nchi hii zikitawaliwa na ubabe, uporaji wa haki ya wananchi kuchagua viongozi wao kwa haki(rejea chaguzi za serikali za mitaa), polisi kuvamia ofisi za wapinzani, kuvuruga mikutano yao hata ile ya ndani, kubambikiza kesi wapinzani na hata wengine kupigwa risasi mchana kweupe bila uchunguzi wowote. Mheshimiwa, sisi tunakupongeza kwa kutaka au kukubali mazungumzo na wapinzani, maana at the end of the day, hii nchi ni yetu sote na ni lazima kila chama kiwe na haki ya kuoperate nchini bila kufanyiana fujo na vurugu.

9. Ndani ya siku 60, umetuonyesha kuwa uko tayari kung'oa Washenzi na waonevu katika nyadhifa za utumishi.
Kitendo cha kumchunguza yule bwana wa bandari na yule kijana mkuu wa wilaya, ni message kali kwa viongozi wengine kuwa hauko tayari kuvumilia ushenzi. Nimependezwa na approach yako ya kuwachunguza na hatimaye kuchukua hatua, maana haitoshi tu kumtumbua mtu, bali atumbuliwe huku ukiwepo ushahidi wa kutosha kumfikisha katika mkono wa sheria, lakini pia inalinda haki yake kama labda anasingiziwa.

10. Mheshimiwa rais, ndani ya siku 60, umeagiza wale walikuwa na elimu ya darasa la saba waliofukuzwa kazi bila kulipwa stahiki zao walipwe

Mheshimiwa hili ni jambo zuri, ni jambo la haki, maana wale ni wanadamu, wana haki zao za msingi, kitendo cha wewe kuzitambua, ni jambo la faraja sana

OMBI MAALUM KWAKO MHESHIMIWA RAIS

1. Mheshimiwa Rais, Mwenyezi Mungu amekuweka katika hiyo nafasi, basi tunaomba sisi wananchi utujengee MIFUMO mizuri ili kesho na keshokutwa upo au haupo tuweze kusema kuwa umetuacha tukiwa na HAKI zaidi katika nchi, tukiwa HURU zaidi katika nchi, Tukiweza KUWAWAJIBISHA Viongozi wetu zaidi katika nchi, TUKINUFAIKA na rasilimali zetu zaidi katika nchi.

Na hilo halitiwezekana chini ya katiba hii ya sasa, Hii ni katiba ya KIDIKTETA yaani hata wewe hapo mheshimiwa rais ukiamua kuwa Dikteta katiba hii inakupa ushirikiano mkubwa. Sasa tunaomba utupe MUAFAKA mzuri zaidi wa Kitaifa, na Muafaka huo ni Katiba mpya iliyo nzuri na bora. Mhwshimiwa hili ndo litatufanya tukukumbuke zaidi kuliko hata kama utaweka mabomba ya asali katika kila nyumba!.

2. Pili naomba wale waliovunjiwa nyumba zao Kimara-Mbezi, serikali yako iwaangalie, maana Serikali iliyopita ilionyesha ubaguzi kwenye kutekeleza zoezi la ubomoaji, wale wa Mwanza ilisema wasibomolewe eti kwa sababu walimpa kura Magufuli kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, ila wale wa Kimara-Mbezi serikali ikawabomolea bila kujali kuwa walikuwa na Stop order ya Mahakama kuzuia ubomoaji huo. Mheshimiwa Rais naomba uwape kifuta machozi wananchi wa Kimara Mbezi maana kuna ukatili mkubwa na double standard kubwa sana ilifanyika pale.

3. Tunaomba zile sheria za kidhalimu, zenye lengo la kuupalilia udikteta nchini zifanyiwe marekebisho au ziondolewe kabisa. Mheshimiwa rais tunaomba uondoe sheria inayowapa kinga Spika, Naibu wake na Waziri mkuu Kinga ya kutoshitakiwa, hawa wanataka wasishitakiwe kwa nini?, pia sheria za mitandao, vyombo vya habari na kanuni zake zibadirishwe. Hizo sheria siyo conducive kujenga Taifa la watu wenye FIKRA huru kutoa maoni yao kikamilifu, na hazilindi wala kupanua Demkrasia yetu

4. Pia Mheshimiwa Rais, nchini katika majela yetu kumejaa Masheikh wengi ambao wamo ndani kwa kesi za kubambikiza ikiwemo Masheikh wa UAMSHO na wengine wengi nchini, hawa bado hawajaachiwa, nakuomba Masheikh hawa wasio na hatia nao waachiwe kama wafungwa wengine waliobambikiziwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kisiasa wanavyoachiwa.

Mwisho kabisa nimalize kwa kusema.
Mheshimwa, Upo kwenye right track sana, yaani uongozi wako ni mzuri na makini mno endelea kuchapa kazi

Kazi iendelee!
Mama tunamshukuru sana kwa hayo ila tunahitaji mabadiliko katika mfumo mzima wa elimu, Elimu ya Tz haina tija kabisa kwa wahitimu.
 
Huyu mama ni mzuri sana na anaenda vizuri, ila jambo la kuzingatia ni kwamba, mzazi mzuri ni yule anayetafuta suluhu ya matatizo ya watoto wake baada ya yeye kutokuwepo duniani.
 
Back
Top Bottom