MgosiMnubi
JF-Expert Member
- Dec 6, 2022
- 464
- 685
Mininayo mkuu nipatie io laki nikuachie chap.NIKO SERIOUS😎Habari za majukumu wakuu.
Naimani mmeamka salama!
Tanzania nchi yangu kuna nini kinaendelea, kila siku jambo jipya.
Kujielekeza kwenye hoja
Kumezuka suala la watu kuzitafuta sana noti za Shilingi 500 tena wanaspecify ziwe na kichwa cha Hayati Nyerere na nyoka.
Sizikumbuki vizuri tofauti ya hizo noti kipindi zikiwa bado hazijatoweka sokoni.
Tena wako radhi kuzinunua kwa pesa kubwa kuanzia 50,000 mpaka 100,000 kwa noti moja.
Kuna nini kinaendelea kwa wanaofahamu Wakuu??
Asanteni.