Kuna jambo gani katika noti za Tsh 500? Mbona watu wapo radhi kuzinunua kwa gharama kubwa?

Hazina ya mjerumani, rupia, mia ya zamani, sijui shilingi nyerere kaangalia kushoto sijui kulia aisee ni yale yale sema yanakuja kwa njia tofauti tofauti tu.
 
tumetoka kwenye sarafu ya shilingi 20,rupia,na wenzake wengine,tukaja kwenye mercury na sasa tunahamia rasmi kwenye noti ya jero.

hii nchi ina pilika sana.
Halafu wajinga huwa hawaishi ndio mtaji wa hao matapeli.
Wanaanzisha biashara feki mara rupia,mara mia 5,mayai ya kware,mayai ya dudumizi ili kuwapiga.
 
Naona wadau mnampinga sana mleta mada kwa kudai kwamba hilo jambo si la kweli,,,,, binafsi ninao ushuhuda kuna dogo mmoja aliulizia hizo noti nikamwambia ninayo moja basi tangu siku hiyo alinikomalia sana nimuuzie kwa bei ya 3k tsh/= nikamtania kwamba anipe 5k/= akakubali nikamwachia ile hela coz skuona kazi yake,,,,,, kesho yake alirudi mwenzie akaniambia ile noti imeuzwa kwa mganga mmoja hivi huko bush kwa 30k tsh/=.
Nadhan hizo noti zitakuwa zina matumizi katka mambo ya kiganga,

NB; Wanatafuta jero za noti tu achana na hizi sa coins( sarafu).
 
Back
Top Bottom