Kuna hali ya kukata tamaa kwa vijana baada ya ajira mpya za walimu

msovero

JF-Expert Member
Jun 30, 2019
839
1,472
Baada ya ajira za ualimu kutangazwa vijana wengi wameonekana kukata tamaa huku mioyo yao ikifunikwa na wingu nzito la huzuni na majonzi yasiyoelezeka.

Miongoni mwa mambo yaliyochangia vijana kukata tamaa ni pamoja na Tamisemi kutumia suala la umri kama kipaumbele cha ajira. Kama tunavyofahamu serikali imekuwa ikisisitiza wazazi kusomesha watoto wao wakiwa na umri mdogo ili pindi wamalizapo masomo walitumikie Taifa kwa muda mrefu.

Leo watoto wamesoma wamemaliza vyuo wakiwa na umri wa miaka 20+ serikali inasema kigezo cha kuajiriwa ni miaka 40. Maana yake kama kijana amemaliza chuo na miaka 25 itamlazimu kukaa mtaani kwa miaka 15 ndipo aajiriwe. Kama amemaliza chuo akiwa na miaka 26 itamlazimu kukaa mtaani kwa miaka 14 ili afikishe miaka 40 ndipo aajiriwe.

Vile vile mtu mwingine anaweza kuwa na umri mkubwa lakini kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo kukariri madarasa miaka ya nyuma ikamlazimu kurudisha umri nyuma kwenye cheti chake cha kuzaliwa ili kukidhi vigezo vya kiserikali kupata elimu katika mfumo rasmi hususani katika ngazi ya vyuo ambako kigezo cha umri na mwaka wa kumaliza masomo kinazingatiwa.

Mathalani utakuta mtu kwenye cheti chake kinaonyesha ni mzaliwa labda wa 1994 lakini kiuhalisia anakuwa ni mzaliwa wa 1988. Kwa mtu kama huyu ukifuata umri wa kwenye cheti utamuona kama mdogo lakini kwa umri halisia ni mtu mzima na mtu kama huyu ukisema hadi afikishe miaka 40 ndipo umwajiri maana yake utakuja kumwajiri akiwa na miaka zaidi ya 50 kwa umri halisi. Hili kwakweli haliko sawa inabidi serikali ilitazame upya

Jambo lingine ni tamisemi kutozingatia mwaka wa kumaliza chuo kama walivyowaaminisha waombaji. Waziri ummy alisema watazingatia mwaka wa kumaliza chuo na kwamba wataajiri kwa series kwa kutoa kipaumbele kwa waliomaliza miaka ya nyuma lakini hata hiki kigezo nacho bado kimekiukwa.

Nasema kimekiukwa kwa sababu baadhi ya walimu waliomaliza 2017 na wengi wa 2018 wenye masomo yale yale wameachwa wakachukuliwa wa 2019. Maana yake utaratibu wa kuajiri kwa kufuata mtiririko wa miaka ya kumaliza chuo haujazingatiwa bali wameendelea na utaratibu wa kuajiri kwa kudonoa donoa ilimradi waombaji wote walioambiwa kuomba kazi ionekane wameajiriwa

Mengine yataongezewa na wadau....
 
Kigezo cha umri hakipo official mana wapo wengi wamechukuliwa wakiwa na miaka 25 had 24 na waliowazidi wameachwa.
 
Kwa kuongezea tu, ajira zilizotolewa ni pamoja na madaktari, wauguzi, wafamasia na wengine
Labda wamezingatia umri ili waweze kulipa madeni ya HESLB
 
Kigezo Cha umri kipo sahihi maana watu hao wamesota sana sasa wewe ni mtu gani usiye na huruma unaweza kuwahudumia watoto kweli unataka utoke shule na kuajiriwa wakati wenzio wamekaa sana mtaani
Kwa kuongezea tu, ajira zilizotolewa ni pamoja na madaktari, wauguzi, wafamasia na wengine
Labda wamezingatia umri ili waweze kulipa madeni ya HESLB
 
Umri unapewa kipaumbele maana watoto wanasumbua Sana kazini hawajielewi wanaendekeza mitandao ya kijamii muda wa kazi
 
Kigezo Cha umri kipo sahihi maana watu hao wamesota sana sasa wewe ni mtu gani usiye na huruma unaweza kuwahudumia watoto kweli unataka utoke shule na kuajiriwa wakati wenzio wamekaa sana mtaani
hao wenye umri mkubwa ndio wale waliokuwa wanapewa ajira kipindi cha kikwete, wanaenda kuripoti kazini wanauta pesa ya kujikimu then wanakimbia kazi

kilichofanyika ni siasa tupu
 
Mnategemea ajira za serikali!....kuna msenge mmoja amekaa kule kwenye kona serikalini amesubili mimi na wewe wenye madiploma na madigrii yetu tukate tamaa ya maisha au tupotee kabisa kwenye uso wa dunia.....ndugu zangu tusikubali ndoto za huyu 'msenge' zitimie...
 
Back
Top Bottom