BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Posted Date::1/5/2008
Serikali bado yaiota Real Madrid
Na Vicky Kimaro
Mwananchi
SERIKALI bado inaiota ziara ya vigogo wa Hispania, Real Madrid, ambao walialikwa mwaka jana kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa Uwanja Mkuu wa Taifa, lakini hawakuja.
Rais Jakaya Kikwete alitoa mwaliko kwa mabingwa hao wa Hispania wakati aliposimama kwa muda jijini Madrid akiwa ziarani barani Ulaya na vigogo hao walitarajiwa kuja nchini Julai mwaka jana kwa ajili ya sherehe za ufunguzi, lakini ikashindikana.
Lakini jana, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Seif Khatib Muhammed, alisema serikali bado inaendelea na mipango ya kuileta timu hiyo, ambayo kama ingekuja mwaka jana ingecheza mechi tatu za kirafiki.
"Tunawasubiri wangalizi wao waje," alisema Khatib. "Hili suala sio kwamba limefutwa linafanyiwa kazi na litakapokamilika tutawajulisheni."
Real, ambayo Inaundwa na wachezaji wengi nyota duniani, ilikuwa inahitaji kitita cha shilingi bilioni 6.8 kwa ajili ya kulipia gharama za safari yao.
Ili kufanikisha ziara hiyo, serikali iliunda kamati chini ya mwenyekiti wa Baraza la Taifa (BMT), Idd Kipingu kushulikia safari hiyo.