Hii tabia ya kukarabati barabara muda mrefu ni kero sana

incredible terminator

JF-Expert Member
Aug 1, 2016
2,246
3,548
Wakuu habari,

Inasikitisha sana hawa wakandarasi wanaorekebisha barabara wanavyofanya kazi kimazoea na kusababisha kero kwa watumiaji.

Mimi ni mkazi wa Dodoma, ikiwa jiji hili lilipewa hadhi ya kuwa Mji Mkuu wa Tanzania, sijui kwanini wizara husika zinakubari Jiji hili kuchukuliwa poa.

Kuna vijitabia vinafanyika kimazoea jijini hapa kiasi kwamba hadi watu tunashindwa kuelewa kwamba hili taifa halina uongozi au nikuchukuliana poa?

Mfano barabara ya Bahi ambayo wengi huitamka kama byeroad, Mwanza road etc, kumekuwa na tabia ya barabara hii kujazwa kokoto, kutoka round about hadi Kizota Msikitini, pasipokuwepo na viashiria vyovyote vya tatizo katika barabara husika.

Kokoto hizo hujazwa na kusababisha kero kama vile vumbi pamoja na hatari ya utelezi kwa watumiaji wa barabara hii, pasipo sababu za kimsingi zozote zile.

Inaonekana kama ni bajeti za upigaji tu zinaratibiwa kwa kuwa barabara iko vizuri tu, chanzo cha kumwaga makokoto na kusababisha kero kwa watumiaji hakieleweki kabisa, maana hata mara baada ya kokoto hizo kuisha ndio husababisha mabonde na mitikisiko katika barabara.

Pili, Barabara ya Mbeya, tangu mwaka jana mkandarasi anaetengeneza barabara ya standard guage, au Barabara ya Treni ya umeme, waliharibu kipande cha barabara maeneo ya Mkonze, kutoka njia panda ya Hosptali ya Mkonze hadi maeneo ya White Rore, au Image Petrol Station, kwa ajili ya marekebisho ya barabara ya juu ya treni ya umeme, na baada ya kukamilisha zoezi lao.

Hadi sasa, kipande kile hakijafanyiwa marekebisho, na kimegeuka kero kubwa kwa watumiaji wa barabara ile, ukilinganisha barabara ile ni miongoni mwa barabara ambazo zinatumika sana kwa magari ya mizigo.

Kuna vumbi lisilokuwa la kawaida, tena kibaya ni vumbi lenye mchanganyiko wa cement, kitu ambacho ni hatari sana hata kwa afya za watumiaji wa barabara ile. Ila cha ajabu wizara ziko kimya, na njia hii inazidi kuwa hatarishi kwa kuwa kuna muda vumbi linafunika njia nzima na hata mtu asijue kipi kinakuja mbele yake kutokana na wingi wa vumbi.

Sijui kama ndio kuchukulia poa au wanajifanya hawaoni. Pia barabara hii hii ya Mbeya maeneo ya Matumbulu, Mpunguzi, hadi sasa barabara iko katika marekebisho ila mchepuko wa njia iliyoandaliwa ili kupisha marekebisho ya barabara haukidhi mahitaji kulingana na umhimu wa barabara husika na matumizi yake, na bado kasi inayotumika kutengeneza barabara ile ni taratibu sana, kiasi kwamba hadi sasa ni Mwezi wa Tatu unaelekea wa Nne tangu marekebisho yale yaanze kufanyika ila kazi inaonekana bado sana; kama ndio wameanza siku tatu!

Hapa tuaniomba serikali iingilie kati changamoto hizi, hasa kile kipande cha Mkonze kwani lile vumbi ni hatari kwa afya za watumiaji wa barabara ile.
 
Kuna wale wanakwangua lami halacu wanahitaji miezi minne kuweka lami upya, angalia barabara ya chalinze mlandizi
 
Kero sana huku Mbeya wilaya ya Rungwe Barabara Kutoka Suma kupitia Mpata kuelekea Kanyelele kwenda Rwangwa Kifusi kimemwagwa toka Mwezi Wa Pili Hadi Leo hakijasambazwa....
 
Kero sana huku Mbeya wilaya ya Rungwe Barabara Kutoka Suma kupitia Mpata kuelekea Kanyelele kwenda Rwangwa Kifusi kimemwagwa toka Mwezi Wa Pili Hadi Leo hakijasambazwa....
hili la kurundika vifusi ndio tatzo kubwa zaidi na sasa wananyanyasa madereva kuwafutia reseni kama kwamba reseni ndio hushikiria usukani wakisahau kuwa barabara wanazotumia madereva ni changamoto zaidi na hawazingatii
 
Hapa Zanzibar kuna kipande kidogo tu kama mita 100 na kinakarabatiwa karibu mwezi sasa, na ni njia anapita Rais kwenda Ikulu pamoja na ambulance za wagonjwa. Na ata dalili ya kumalizika hakuna. Kuna shida ya hawa wakandarasi wetu. Halafu huu ni wakati wa mvua wao ndo wameamua kufanya ukarabati
 
Hapa Zanzibar kuna kipande kidogo tu kama mita 100 na kinakarabatiwa karibu mwezi sasa, na ni njia anapita Rais kwenda Ikulu pamoja na ambulance za wagonjwa. Na ata dalili ya kumalizika hakuna. Kuna shida ya hawa wakandarasi wetu. Halafu huu ni wakati wa mvua wao ndo wameamua kufanya ukarabati
Tatizo haliwezi kuwa katika wakandarasi matatizo yapo katika serikali yetu,kwa kuwa mkandarasi hupokea maagizo kama sivyo itakuwa viongozi wana namna wanakubaliana na wakandarasi katika kazi kiasi kwamba hata wakashindwa kuwaamrisha kwa kuwa kuna makubaliano ya kimasrahi baina yao
 
Back
Top Bottom