Kuna haja ya kutumia mabilioni ili kuileta hii timu?

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Posted Date::1/5/2008
Serikali bado yaiota Real Madrid
Na Vicky Kimaro
Mwananchi

SERIKALI bado inaiota ziara ya vigogo wa Hispania, Real Madrid, ambao walialikwa mwaka jana kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa Uwanja Mkuu wa Taifa, lakini hawakuja.

Rais Jakaya Kikwete alitoa mwaliko kwa mabingwa hao wa Hispania wakati aliposimama kwa muda jijini Madrid akiwa ziarani barani Ulaya na vigogo hao walitarajiwa kuja nchini Julai mwaka jana kwa ajili ya sherehe za ufunguzi, lakini ikashindikana.

Lakini jana, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Seif Khatib Muhammed, alisema serikali bado inaendelea na mipango ya kuileta timu hiyo, ambayo kama ingekuja mwaka jana ingecheza mechi tatu za kirafiki.

"Tunawasubiri wangalizi wao waje," alisema Khatib. "Hili suala sio kwamba limefutwa linafanyiwa kazi na litakapokamilika tutawajulisheni."

Real, ambayo Inaundwa na wachezaji wengi nyota duniani, ilikuwa inahitaji kitita cha shilingi bilioni 6.8 kwa ajili ya kulipia gharama za safari yao.

Ili kufanikisha ziara hiyo, serikali iliunda kamati chini ya mwenyekiti wa Baraza la Taifa (BMT), Idd Kipingu kushulikia safari hiyo.
 
Nchi ina matatizo mengi ambayo yanahitaji ufumbuzi. Badala yake Serikali inakimbilia kuleta timu na kutafuta sifa ambayo haimsaidii Mtanzania zaidi ya wachache ambao watawalaza Real Madrid, kuwalisha, na kuwaendesha wakifika Tanzania.

Na hao watakaofaidika wanaweza wasiwe Watanzania.
 
1. JK hili kuleta Real Madrid ni mambo ya cheap popularity- kama Tz we shall have to pay 6.8 Billions- ni sawa na budget ya Wizara ya EA!

2. Tunahitaji mjadala wa kitaifa on appripriate ways of setting priorities in the way we spend our resources! Sio tu raisi siku anajiskia anapitia Ulaya na kuwapa Walipa kodi mzigo mzito kila siku!

Hii nchi bado tuna matatizo- 6.8 billions zingeimashisha sana michezo shule za msingi- ili kutambua na kukuza vipaji! We dont need Real Madrid now!
 
1. Mishahara ya wafanya kazi iko chini!
2. Miundo mbinu ni mibovu, sehemu nyingi hazifikiki wakati wa masika!
3. Hospitali nyingi hazina madawa na vifaa vya ktolea huduma!
4. Shule hazitoshi!
5. Wanafunzi wa vyuo vikuu wanakosa mikopo kwani wizara haina hela
6. Wastaafu ya jumuiya ya EA hadi leo bado wanasota!
7. Wananchi wengi hawana maji safi!
8. ............

OOh Tanzania!
Hata wakija, sidhani kama gharama inaweza kurudishwa!

Tusikubali hiki kitu kifanyike, tusemae hapana! na tuwafanye wananchi wetu waseme HAPANA.

Tufanye compaign!! naamini tunaweza.
 
Yale yale ya misplaced priorities! hawa wataleta kikosi C, watatufunga mabao maengi na watarudi kwao wakisimulia jinsi walivyopambana na nyoka, mende hali kadhali katika makazi yao! Hatuwahitaji. Hatuwahitaji. We have better things to do.
 
Wanayoiona kwenye tv ikicheza ni wangapi na watakayoiona ikija hapa ni wangapi...
Mechi kama hii TFF watakwambia kiingilio ni laki mbili,na kiwango cha chini kabisa 50,000! Sasa sijui inakuwa ni kwa faida ya nani
 
Back
Top Bottom