Sadio Mane wa Liverpool FC kuondoka

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
18,511
68,141
Ripoti mbalimbali toka viunga vya jiji la Liverpool zinabainisha mshambuliaji wao raia wa Senegal, Sadio Mane, ataondoka dirisha hili la kiangazi.

Habari hizo zinadai kwamba, Bayern Munich wamekuwa na makubaliano ya muda kumtaka Mane, na wakakubaliana wasubiri kwanza mpaka fainali ya UEFA iliyochezwa usiku wa jana ipite, ambapo Liverpool walifungwa 1-0 na Real Madrid ya Hispania.

Inajulikana wazi sababu za,Bayern kumtaka Mane ni kwa ajili ya kuziba pengo la mshambuliaji wao wa Poland, Robert Lewandoski, ambaye anataka kutimkia FC Barcelona ya Hispania majira haya ya kiangazi.

Kinachosubiriwa sasa ni kuona kama Liverpool FC, watakuwa tayari kumpoteza Mane aliyebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake unaoisha 2023, huku wakiwa bado hawajampata mbadala wake.

Swali la kujiuliza ni je; moto wa Liverpool utaendelea kuwepo bila Sadio Mane pale mbele akishirikiana na Mo Salah?
 
Pamoja na mane kukiwasha na kuisaidia Liverpool...

Lakin ni mchezaji ambaye alikuwa analipwa mshahara mdogo zaidi ,Hadi kilaza Henderson alikuwa anamzidi mshahara ....

£100k per week

Na walikuwa hawawezi kumpa mkataba zaidi ya hio .... liverpool ni wanyonyaji tu
 
duh!, nilisikia analipwa 200,000 kwa wiki.
 
PESA PESA FWEZA.
Looserfully wanakomaa waendelee kumlipa euro laki moja wakati bayern watampa euro laki mbili kwa week.
Salah naye anaenda madrid tuone wachovu looserfully na van daiki ma alison beka watafanya nini?
Salah alikuwa anatingisha kiberiti, lakini kabka ya ile fainali akaja kuwaambia ana amini msimu ujao atakuwepo Liverpool akimaanisha atabaki.
 
Huyu mwamba ni mpambanaji san
Licha ya kuwa mim sio shabik wa liverpool ila nataman san niendelee kumuon Epl.Anajua kuipambania timu
Kila la kher kwako
 
Liver mafala Sana ,na kama mo Salah asingekuwa na uroho kwenye finl na Madrid Mane alikuwa na chance nzuri ya kuscore kuliko Salah ambaye alikuwa anapambana kufunga mwenyewe bila mafanikio...mshikaji asepe tuu
 
Pamoja na mane kukiwasha na kuisaidia Liverpool...

Lakin ni mchezaji ambaye alikuwa analipwa mshahara mdogo zaidi ,Hadi kilaza Henderson alikuwa anamzidi mshahara ....

£100k per week

Na walikuwa hawawezi kumpa mkataba zaidi ya hio .... liverpool ni wanyonyaji tu
Hata kama unalipwa 50K una miaka 6 utaendelea lipwa hyo hadi mkataba uishe ndo utaongezewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom