Kuna haja ya kuchangia hela ya mafuta ukiwa unapewa lifti ya gari kila siku?

Onyix

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
683
788
Naomba kuuliza kwa Wadau.

Hivi kuna haja ya mtu anayekupa lift (Msaada wa usafiri kwenye gari) kila siku kuchangia mafuta kwenye gari lake, ..!?

Au unatakiwa uuchune uwe Shock absorber tu kwenye gari la watu..!!
 
Jiongeze, siku mmeenda sheli akishaweka wese lipia wewe, fanya hivyo walau mara moja kwa week (unajua gharama za mafuta kwa safari yenu).

Hii itamfanya asikuchoke, hata wewe itakupa ahueni ya kujihisi mzigo sana(incase una mshipa wa aibu).

Ndio hata usipompa atanunua na ataenda safari hio, ila na wewe hufanyi kumlipa unafanya kama ka support flani hivii.

Hii sehemu Usiombee awe KE, hawa watu utawapa lift mwaka, hata kujigusa, Yeye anaona kila mwanaume anamchukulia kimawazo ya kike, Sio kila njemba ni inawaza uchi tuu, muda mwingine bora ME mwenzako maana unaelewa hustle, kuliko unajua kabisa huyu anataka Dezo...

Kuna muda inabidi, Ujiulize hivi huyu kichwani mwake ananiwaziaje mimi kila siku kupanda Bure?
Kama unaona anakuwazia mazuri, fresh kabisa tena akichelewa muulize kabisa mbona unanichelewesha? Hujui nachelewa majukumu yangu? Washa Gari haraka uniwahishe.
 
1-Amekupa lifti. Haujamuomba.
2-Ametaka/ameshauri uchangie?
3-Huwa anakupa lifti kiroho safi au anazungushazungusha maneno akitaka umchangie?
4-Wewe unajisikiaje na unafikiriaje kama asingekuwa anakupa lift?
5-Kumchangia mafuta mara mojamoja au mfululizo unaweza/unataka iwe hivyo?
6-Vipi kama usipomchangia, unaingiwa na hisia hasi?
 
Kama ni kila siku hebu jiongeze mkuu. KILA SIKU?
ila kama mwenye gari ni mtumishi wa taasisi ya serikali uchune.
 
Akienda peke yake inakuwaje?;Yaani kunipa lift mimi consumption ya mafuta inaongezeka!Anipe tuu lift nikinunua la kwangu nae nitampa lift.
Na wewe ukienda peke yako itakuwaje?
Vitu vingine ni kama ku mpush tuu,
Anakusaidia, na wewe unamsaidia, mnaishi kwa kusaidiana hamna anayeumia hamna anyeumiza, kwa kufanya hivyo Ukaribu utakua wa manufaa sio Uchawa.
½ + ½ = 1
 
Fanya hivyo, mwingine anashundwa kukuambia ila hafurahii, halafu sio kama hafurahii sababu anaingia gharama, Hafurahii sbb kwa nini huyu hajiongezi...

Ohooo utakuja Pelekewa Semi kwenge site we haya.
 
Back
Top Bottom