Kuna haja ya kuchangia hela ya mafuta ukiwa unapewa lifti ya gari kila siku?

Naomba kuuliza kwa Wadau.

Hivi kuna haja ya mtu anayekupa lift (Msaada wa usafiri kwenye gari) kila siku kuchangia mafuta kwenye gari lake, ..!?

Au unatakiwa uuchune uwe Shock absorber tu kwenye gari la watu..!!
Mwanaume usipende kusaidiwa kila siku kama kiwete.
Siku moja moja ukimsapoti hata lita 2 jamaa atakuona wa muhimu
 
Naomba kuuliza kwa Wadau.

Hivi kuna haja ya mtu anayekupa lift (Msaada wa usafiri kwenye gari) kila siku kuchangia mafuta kwenye gari lake, ..!?

Au unatakiwa uuchune uwe Shock absorber tu kwenye gari la watu..!!
Inategemea kama ni msaada ukianza kuchangia inakuwa ni kama Taksi (yaani jamaa anakuwa na obligation hata ukichelewa anakusuburi) after all kuna kitu umempa; otherwise anakuwa na uhuru wa akikuona anasema twende..., Ukianza kuchangia huchelewi kuanza kumfokea kwamba kwanini anachelewa kupita na gari lenu...
 
Naomba kuuliza kwa Wadau.

Hivi kuna haja ya mtu anayekupa lift (Msaada wa usafiri kwenye gari) kila siku kuchangia mafuta kwenye gari lake, ..!?

Au unatakiwa uuchune uwe Shock absorber tu kwenye gari la watu..!!
Ukitaka upate jibu sahihi, jitutimue ununue hilo gari! Halafu fanya huo utafiti wa kuwapa watu lifti, ili uone kama ni sahihi mtu kupanda tu bure! Au anatakiwa na yeye kujiongeza kuchangia mafuta.
 
Usipende kitonga mkuu unataka lift mnaenda ofisini mda wa chai we unaagiza supu kidali na chapati Pepsi baridi jamaa mwenye gari ana kunywa chai rangi na andazi anabana pesa aweke mafuta we umeshashiba unasubiri lift ukasinzie kwenye gari yake acha dharau kasinzie kwenye daladala
Bro kama ulikuwepo asee na ndio anafanya hivyo
 
Roho mbaya hiyo,hatufanani kama alama za vidole
Acha kupenda vya dezo lift upande tuuuuuuuuu... fahamu tu ninapoisho hatupmbani lift Kila mtu anaweza yake.

Nimetoa sana enzi za masomo kwa wanafunzi wa shule au maeneo ya karibu na shule.. Wala hawakutoa kitu..

Nasisitiza acha kupenda vya dezo.. na wewe na wenzako muwe na aibu na kazini mnakwenda..
 
Hatuachi,tutabana apo apo,kipare tunasema don't loose your self,trie to hold into someone else
Kesho nitapita mitaa yako ya osterbay kuVizia lift
 
Kwamba upande lift siku tano za kazi na huchangii hata mia? Mkuu panda daladala....

Wanawake(baadhi) ndio wanajizima akili, wanaweza kupanda hata mwaka na mia hawachangii
 
Naomba kuuliza kwa Wadau.

Hivi kuna haja ya mtu anayekupa lift (Msaada wa usafiri kwenye gari) kila siku kuchangia mafuta kwenye gari lake, ..!?

Au unatakiwa uuchune uwe Shock absorber tu kwenye gari la watu..!!
Hii falsafa kuwa hata usipochangia, lazima niweke mafuta kufika ninakoenda, ni falsafa ya kimaskini na inaongelewa na wasio na magari. Tambua, gari ukiibebesha mzigo zaidi, engine inatumia nguvu zaidi kusukuma gari, na hivyo ulaji wa mafuta unaongezeka.
Kama ni mshikaji wa kweli, changia siku moja moja
 
Bora nipande daladala, lifti kinyonge Sana mwenye gari mshabiki wa Simba mimi Yanga sasa inabidi kusapoti ujinga wake kwa jina la Uzalendo, kama kesho ataishabikia draw yake kishenzi... sio kinyonge kihivyo kesho napanda Nyoka Gomz Mnazi nipaishane sauti na wanazi kwenye Treni
 
Kama wote walevi au wazinzi,af familia zenu zipo karibu,kausha. Maana mnafichiana siri nyingi,na kwenye maovu hayo mnaenda wote. Sasa,kama hilo ni tofauti,panda tu daladala. Maana lift hiyo unapanda kwa sababu uwezo huna. Kwa wiki kama ungepandia elfu 5, kumuwekea mafuta utalipa si chini ya 15 elfu. Hiyo hasara sasa. Labda kama we mwanamke,utakuwa unajikalisha huko mbele,upandishe kidogo misketi labda aafishe tu macho
 
Kwanini upewe lift kila siku!? Kuna watu hamna mshipa wa aibu, au wewe ni ke?
 
Back
Top Bottom