Kuna haja ya kuboresha kitabu cha 'wageni' gesti

Kuna haja ya kuboresha kitabu cha 'wageni' gesti

Ila wadada wa guest wanapiga pesa bwana yani guest ikiwa na mzunguko mzuri zile short time kwa siku unakuta kabana mpaka 40,000/ tena kama mm sikumbuki ni lini mara ya mwisho niliandika kwenye kitabu.
Ndugu Gest za siku hizi hizi za kishua zinafungwa camera hakuna Cha kubana Wala nn
 
Sipendi kujaza taarifa zangu kwenye vitabu vya gesti. Yaani mtu mwenye nia ovu anaweza kutumia taarifa zako kukudhuru. Napenda kujaza fomu ambazo hakuna mtu ataona taarifa zangu isipokuwa muhudumu tu.
 
Unaweza kunishangaa kwa mada kama hii na kufikiri nimewaza nini.. Lakini kama hili likifanikiwa tutakuwa tumesaidia kutatua tatizo kubwa sana

Wote tunatambua kwamba guest house ama nyumba za wageni kwa zaidi ya asilimia 80 zinatumika ndivyo sivyo... Kwa asilimia zote hizo huko ni machimbo ya ufuska, umalaya na ngono kwa wanafunzi, wamaume na wanawake wasio waaminifu kwenye ndoa zao, ma bar maid, beki tatu nknk

Ni kwa asilimia chache sana nyumba hizi hutumika kwa usahihi... Kwamba mtu ni mgeni kweli wa hilo eneo na hana ndugu au jamaa au rafiki, ama jamaa yake kutokana na ufinyu wa nyumba yake basi akuchukulie chumba gesti.. Na ni kwa asilimia chache zaidi mtu kuchukua chumba na kulala peke yake[emoji30][emoji848][emoji144]

Mapato ya hizi nyumba hutegemea 'wageni ' wa muda mfupi maarufu kama short time

Sasa basi kwa wale wanaolala kwa sababu zozote zile maranyingi hujaza kumbukumbu za uongo kwenye kitabu husika, kuanzia jina, kabila, mawasiliano mahali atokapo nknk.. Hili huwa gumu mara litokeapo tatizo kwa mgeni
Hivyo basi ni vema kwenye kile kitabu kikaongezwa kipengele cha MAWASILIANO YA MTU WA KARIBU ama msiri in case of emergency..

Pindi likitokea tatizo lolote hasa la ugonjwa ama kifo ni rahisi kwa wanaokujua kupata taarifa mapema na kutafuta msaada wa haraka.. Unaweza kufia gesti na mtu uliyekuwa naye akasepa kisha ukaishia mochwari na baadae kuzikwa na manispaa

Jr[emoji769]
Wazo ni zuri sana nakumbuka iliwahi kunitokea kwenye Guest House moja Tabora niliambiwa nitoe namba za mtu wangu wa karibu,nikatoa ila niliona kama ni utaratibu mgeni kwangu ila ni mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kunishangaa kwa mada kama hii na kufikiri nimewaza nini.. Lakini kama hili likifanikiwa tutakuwa tumesaidia kutatua tatizo kubwa sana

Wote tunatambua kwamba guest house ama nyumba za wageni kwa zaidi ya asilimia 80 zinatumika ndivyo sivyo... Kwa asilimia zote hizo huko ni machimbo ya ufuska, umalaya na ngono kwa wanafunzi, wamaume na wanawake wasio waaminifu kwenye ndoa zao, ma bar maid, beki tatu nknk

Ni kwa asilimia chache sana nyumba hizi hutumika kwa usahihi... Kwamba mtu ni mgeni kweli wa hilo eneo na hana ndugu au jamaa au rafiki, ama jamaa yake kutokana na ufinyu wa nyumba yake basi akuchukulie chumba gesti.. Na ni kwa asilimia chache zaidi mtu kuchukua chumba na kulala peke yake[emoji30][emoji848][emoji144]

Mapato ya hizi nyumba hutegemea 'wageni ' wa muda mfupi maarufu kama short time

Sasa basi kwa wale wanaolala kwa sababu zozote zile maranyingi hujaza kumbukumbu za uongo kwenye kitabu husika, kuanzia jina, kabila, mawasiliano mahali atokapo nknk.. Hili huwa gumu mara litokeapo tatizo kwa mgeni
Hivyo basi ni vema kwenye kile kitabu kikaongezwa kipengele cha MAWASILIANO YA MTU WA KARIBU ama msiri in case of emergency..

Pindi likitokea tatizo lolote hasa la ugonjwa ama kifo ni rahisi kwa wanaokujua kupata taarifa mapema na kutafuta msaada wa haraka.. Unaweza kufia gesti na mtu uliyekuwa naye akasepa kisha ukaishia mochwari na baadae kuzikwa na manispaa

Jr[emoji769]
Kuna lodge moja nilienda maeneo ya Mbezi ya Kimara waliniomba namba ya simu ya mtu wa karibu [emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Solution ni moja tu kama inavyofanyika katika hotels. Kabla ya kupokelewa toa kitambulisho. Sasa wao wanachukua jina mle. Kama utaweza ongopa namba ya simu lakini jina wanalo.

Sent using my Nokia Torch
 
Waongze kitambulisho cha kupiga kura au leseni ya udereva au kitambuliaho cha mwanafunzi
 
Jazeni taarifa za kweli mkilala. Kuna siku walipita polisi wakachukua kitabu, wanakagua kila chumba na jina. Onesha kitambulisho, kama majina hayafanani unasanda.

Sent using my Nokia Torch
 
Waongze kitambulisho cha kupiga kura au leseni ya udereva au kitambuliaho cha mwanafunzi
 
Upo sahihi, na kipengele kingine ambacho sioni umuhimu wake ni kile cha "kazi yako" sasa nikiandika mhasibu au HR itasaidia nini? nafikiri ilitakiwa kuwa "Taasisi yako" au sehemu unapofanyia kazi. Hii ingeweza kusaidia au kurahisisha kuwapata wanaonifahamu endapo litatokea tatizo.

Kitu kingine ambacho nafikiri kingeongezwa ni, "Tatizo la kiafya" kama mtu analo ataje ili ikitokea wajue pakuanzia.

Mwisho nafikiri kulikuwa na haja ya kuweka kipengele cha "Dhehebu" mgeni ataje anaposali na lilipo kanisa lake au msikiti wake. Hii inaweza kusaidia upatikanaji wa taarifa za mgeni endapo tatizo litatokea.

NOTE: Hapa ninawaongelea wageni sio 'wageni'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mh...ila sometimes bora kuzikwa na manispaa kuliko aibu ya kufia gesti, maana kwa perception yetu sie wabongo wengi moja kwa moja tunaamini mtu kufia gest ni mambo ya uzinz

thanks to god the almighty
Kuzikwa na serikali kuna ubora/ sifa gani? Kwamba huna ndugu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom