Upo sahihi, na kipengele kingine ambacho sioni umuhimu wake ni kile cha "kazi yako" sasa nikiandika mhasibu au HR itasaidia nini? nafikiri ilitakiwa kuwa "Taasisi yako" au sehemu unapofanyia kazi. Hii ingeweza kusaidia au kurahisisha kuwapata wanaonifahamu endapo litatokea tatizo.
Kitu kingine ambacho nafikiri kingeongezwa ni, "Tatizo la kiafya" kama mtu analo ataje ili ikitokea wajue pakuanzia.
Mwisho nafikiri kulikuwa na haja ya kuweka kipengele cha "Dhehebu" mgeni ataje anaposali na lilipo kanisa lake au msikiti wake. Hii inaweza kusaidia upatikanaji wa taarifa za mgeni endapo tatizo litatokea.
NOTE: Hapa ninawaongelea wageni sio 'wageni'
Sent using
Jamii Forums mobile app