Kuna haja ya kuboresha kitabu cha 'wageni' gesti

Kuna haja ya kuboresha kitabu cha 'wageni' gesti

Pamoja na hilo wawe pia na vitambulisho ili jina lihakikiwe kuwa lililoandikwa ndio hilo lipo kwenye kitambulisho
Pamoja na picha yake halisi iwepo kwenye kitambulisho.

Hata kama akiwa na kitambulisho fake chenye jina fake, picha yake halisi itasaidia maana muhudumu lazima ajiridhishe kulingana na picha kuwa huyu ndio mgeni husika.
 
Njia ya kupata taarifa sahihi, ni kuomba kitambulishi tu. MTU kama hana kitambulisho hapati chumba.
kama hapati chumba maana yake hakuna biashara kama chumba ni 15k imepotea hivyo, mmiliki gani wa guest house atakubali hilo???

wamiliki wanataka pesa watumiaji wanataka siri/udanganyifu
 
Wahudumu wa Nyumba za Wageni ni miongoni mwa ajira dhariri kabisa hapa nchini, na kimsingi malipo ya Short Time ndo yanawaweka mjini. Katika mazingira ya aina hii unategemea kupata taarifa sahihi kweli. ? Mshana my Brother!!
Sio short time ni kwa wale walalaji[emoji19]

Jr[emoji769]
 
Unaweza kunishangaa kwa mada kama hii na kufikiri nimewaza nini.. Lakini kama hili likifanikiwa tutakuwa tumesaidia kutatua tatizo kubwa sana
Wote tunatambua kwamba guest house ama nyumba za wageni kwa zaidi ya asilimia 80 zinatumika ndivyo sivyo... Kwa asilimia zote hizo huko ni machimbo ya ufuska, umalaya na ngono kwa wanafunzi, wamaume na wanawake wasio waaminifu kwenye ndoa zao, ma bar maid, beki tatu nknk
Ni kwa asilimia chache sana nyumba hizi hutumika kwa usahihi... Kwamba mtu ni mgeni kweli wa hilo eneo na hana ndugu au jamaa au rafiki, ama jamaa yake kutokana na ufinyu wa nyumba yake basi akuchukulie chumba gesti.. Na ni kwa asilimia chache zaidi mtu kuchukua chumba na kulala peke yake[emoji30][emoji848][emoji144]
Mapato ya hizi nyumba hutegemea 'wageni ' wa muda mfupi maarufu kama short time
Sasa basi kwa wale wanaolala kwa sababu zozote zile maranyingi hujaza kumbukumbu za uongo kwenye kitabu husika, kuanzia jina, kabila, mawasiliano mahali atokapo nknk.. Hili huwa gumu mara litokeapo tatizo kwa mgeni
Hivyo basi ni vema kwenye kile kitabu kikaongezwa kipengele cha MAWASILIANO YA MTU WA KARIBU ama msiri in case of emergency.. Pindi likitokea tatizo lolote hasa la ugonjwa ama kifo ni rahisi kwa wanaokujua kupata taarifa mapema na kutafuta msaada wa haraka.. Unaweza kufia gesti na mtu uliyekuwa naye akasepa kisha ukaishia mochwari na baadae kuzikwa na manispaa


Jr[emoji769]
Yanakuhusu nini wewe maisha ya wengine?
 
Ukisema tuweke mawasiliano ya wandani wetu wa karibu, bado tunaweza tukaweka zile namba za matapeli wa kwenye mitandao.

Labda kuwe na utaratibu wa kufunga kamera za ulinzi kwenye nyumba zote za wageni halafu kila ifikapo mwisho wa wiki, balozi na mwenyekiti wa mtaa waitwe na wamiliki kwenda kuwatambua wageni wote waliolala kwenye gesti husika kwa huo muda wote wa wiki nzima. Hakika tutaanza kwenda vichakani na maporini.
Hapana iko hivi... Ukilala na kuamka salama hakuna shida kabisa... Ishu inakuja pale unapozidiwa chumbani peke yako ama ukaaga dunia mazima[emoji24][emoji24][emoji24]

Jr[emoji769]
 
Nilikua Makete, Mwakauta, miaka ya 2013. Lile eneo ngono inafanyika sana msituni na vichakani kwakua gesti ipo kilomita tano kutoka kijiji na inamilikiwa na kanisa ili uingie utatoa vitambulisho hadi utakoma.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Back
Top Bottom