Kuna haja ya kuboresha kitabu cha 'wageni' gesti

Kuna haja ya kuboresha kitabu cha 'wageni' gesti

Dawa ni kutembea na kitambulisho cha Taifa,mpiga kura au kitambulisho cha kazi au kadi za benki!

Hakuna mtu atakaye kubali kujaza accuracy details kwenye nyumbani ya wageni japo,wazo lako ni zur sana Mr.Mshana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisema tuweke mawasiliano ya wandani wetu wa karibu, bado tunaweza tukaweka zile namba za matapeli wa kwenye mitandao.

Labda kuwe na utaratibu wa kufunga kamera za ulinzi kwenye nyumba zote za wageni halafu kila ifikapo mwisho wa wiki, balozi na mwenyekiti wa mtaa waitwe na wamiliki kwenda kuwatambua wageni wote waliolala kwenye gesti husika kwa huo muda wote wa wiki nzima. Hakika tutaanza kwenda vichakani na maporini.
Hili halitawezekana mkuu kila MTU anahitaji privacy as long as hajavunja sharia ya nchi

CCTV camera ni kwaanili tu ya security surveillance na huwezi anza kupitisha kwa mjumbe,Mwenyekiti ili iweje

But kama kuna suspicion ya uhalifu hapo ndo zinaweza tumika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aje na kitambulisho cha taifa au mpiga kura au leseni yake ukijiandikisha mhudumu anajirisha kuwa ndie yeye kitambilisho kinapigwa photo copy inabaki guest kama ushahidi
 
Ha ha haaa hii umeiongea kama utani ila ina maana sana
Unaweza kunishangaa kwa mada kama hii na kufikiri nimewaza nini.. Lakini kama hili likifanikiwa tutakuwa tumesaidia kutatua tatizo kubwa sana

Wote tunatambua kwamba guest house ama nyumba za wageni kwa zaidi ya asilimia 80 zinatumika ndivyo sivyo... Kwa asilimia zote hizo huko ni machimbo ya ufuska, umalaya na ngono kwa wanafunzi, wamaume na wanawake wasio waaminifu kwenye ndoa zao, ma bar maid, beki tatu nknk

Ni kwa asilimia chache sana nyumba hizi hutumika kwa usahihi... Kwamba mtu ni mgeni kweli wa hilo eneo na hana ndugu au jamaa au rafiki, ama jamaa yake kutokana na ufinyu wa nyumba yake basi akuchukulie chumba gesti.. Na ni kwa asilimia chache zaidi mtu kuchukua chumba na kulala peke yake[emoji30][emoji848][emoji144]

Mapato ya hizi nyumba hutegemea 'wageni ' wa muda mfupi maarufu kama short time

Sasa basi kwa wale wanaolala kwa sababu zozote zile maranyingi hujaza kumbukumbu za uongo kwenye kitabu husika, kuanzia jina, kabila, mawasiliano mahali atokapo nknk.. Hili huwa gumu mara litokeapo tatizo kwa mgeni
Hivyo basi ni vema kwenye kile kitabu kikaongezwa kipengele cha MAWASILIANO YA MTU WA KARIBU ama msiri in case of emergency..

Pindi likitokea tatizo lolote hasa la ugonjwa ama kifo ni rahisi kwa wanaokujua kupata taarifa mapema na kutafuta msaada wa haraka.. Unaweza kufia gesti na mtu uliyekuwa naye akasepa kisha ukaishia mochwari na baadae kuzikwa na manispaa


Jr[emoji769]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawasiliano anayosema nikwamba kila MTU ana msiri wake hata akiwa na mchepuko anamtambulisha au akienda kwenye Mechi anajua
Ukisema tuweke mawasiliano ya wandani wetu wa karibu, bado tunaweza tukaweka zile namba za matapeli wa kwenye mitandao.

Labda kuwe na utaratibu wa kufunga kamera za ulinzi kwenye nyumba zote za wageni halafu kila ifikapo mwisho wa wiki, balozi na mwenyekiti wa mtaa waitwe na wamiliki kwenda kuwatambua wageni wote waliolala kwenye gesti husika kwa huo muda wote wa wiki nzima. Hakika tutaanza kwenda vichakani na maporini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi nilijua utasema

Atoe Kopi kitambulisho chake Cha uraia Cha mpiga kura

Aweke namba za Kiongozi wake wa Serikali ya mtaa anakotoka.


kumbe sivyo
 
Back
Top Bottom