Kuna haja Police General Orders (PGO) ziwekwe hadharani kwa matumizi ya umma

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,801
12,247
Mara nyingi watu hufanyiwa vitendo vya hovyo, udhalilishaji na kunyimwa haki zao za kisheria na kikatiba na polisi wetu kwa kukosa uelewa wa PGO. Hali hii hufanyika kwa makusudi na polisi ama kwa polisi kusahau au kutokuifahamu PGO.

Kwa wananchi kuifahamu vizuri PGO watakuwa katika nafasi nzuri ya kufahamu haki zao kisheria mara wanapowekwa chini ya ulinzi na polisi.

PGO iwekwe mitandaoni na hard copies ziwepo madukani ili wananchi wengi waweze kuzipata.
 
1694422778590.jpg
 
Ukitaka kujua ubabe wa polisi wa tz?wakuweke chini ya ulinzi halafu ujifanye unajua sana sheria?watakumalizia hasira za michepuko zao,hasira za makazi duni n.k
 
Ukitaka kujua ubabe wa polisi wa tz?wakuweke chini ya ulinzi halafu ujifanye unajua sana sheria?watakumalizia hasira za michepuko zao,hasira za makazi duni n.k
Mtaarifu mkuu wake wa kazi (OSS).
 
Tujitahid kupita kwenye maduka ya vitabu.
Tusiwe tunapenda kuandika na kumaliza kama jambo hatujui.
Tuulize kama kuna kitu hatujui.
 
PGO ipo mtandaoni.

lissu ama mwanaharakati yeyote ana nguvu na hari ya kupambana na PT kwa maneno na PGO sababu anajua anachosakamwa nacho kinapingana kabisa na sheria za haji jinai yaani SIASA tu.

vunja kwa watu iba TV wakija kukukamata waambie PGO inasema niwapekue kwanza kabla hamjanipekua halafu sisitiza wajitambulishe,utaamkia hospital uambie umelazwa toka january ukiwa huna fahamu .
 
Mara nyingi watu hufanyiwa vitendo vya hovyo, udhalilishaji na kunyimwa haki zao za kisheria na kikatiba na polisi wetu kwa kukosa uelewa wa PGO. Hali hii hufanyika kwa makusudi na polisi ama kwa polisi kusahau au kutokuifahamu PGO.

Kwa wananchi kuifahamu vizuri PGO watakuwa katika nafasi nzuri ya kufahamu haki zao kisheria mara wanapowekwa chini ya ulinzi na polisi.

PGO iwekwe mitandaoni na hard copies ziwepo madukani ili wananchi wengi waweze kuzipata.
mbona ipo mkuu mtandaoni
 
Hata ujue PGO na sheria zote duniani kwa Tz kama hujulikani au huna connection utanyimwa haki tu,tena ukijifanya unajua utawasikia wanaambiana linajifanya libush royal hili.
 
Nisingekuwa Mganga, ningekuwa Mwanasheria.

Ningekuwa upande wa Jamhuri, nisingetaka kuonana na Lissu.
 
Back
Top Bottom