Kuna cha kujifunza toka Chile? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna cha kujifunza toka Chile?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyani Ngabu, Feb 28, 2010.

 1. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #1
  Feb 28, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,521
  Trophy Points: 280
  Tetemeko lililotokea jana huko Chile ni moja ya matetemeko makubwa sana kutokea duniani. Vipimo vyake vilikuwa 8.8 kwenye mzani wa Richter. Hakika hili lilikuwa kubwa zaidi kuliko lile la Haiti lililotokea mwezi uliopita ambalo vipimo vyake vilikuwa 7.0

  Cha kushangaza hili la Chile inaonekana maafa yake hayatakuwa makubwa sana ukilinganisha na lile la Haiti. Hii pengine ni kwa sababu Chile ilikuwa imejiandaa vya kutosha na janga kama hili kwa sababu ya uwepo wake kwenye ule ukanda wa ring of fire kwenye bahari ya Pacific ambako matetemeko mengi ya ardhi hutokea. Maandalizi hayo yanaelekea yameweza kuepusha maafa makubwa zaidi ya yaliyotokea.

  Mpaka sasa Chile hawajaomba msaada kutoka kwa yeyote yule, si Marekani wala majirani zao Argentina. Bila shaka wana uwezo na ujuzi wa kutosha kukabiliana na kilichotokea.

  Sasa nimekaa hapa nikakumbuka Mzee Mwanakijiji hupenda kusema taifa lisilojiandaa kwa majanga hujiandaa kwa maafa. Binafsi kwa kweli nimevutiwa na jinsi Chile walivyokabiliana na wanavyoendelea kukabiliana na janga hili. Inavyoelekea hata majengo yao yamejengwa imara kuweza kuhimili matetemeko makubwa kama hili la jana. Sasa sijui sisi kama taifa tumejifunza nini kutoka Chile jinsi ya kujiandaa na majanga haya ya asili.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,489
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Julius,'
  Kuna mengi ya kujifunza kutoka Chile. To always be ready for the emergency na spirit ya self reliance. Nimewakubali.
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  huyu ni julius au nyani ngabu.................... mbona mnachanganya watu????????????//.............
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Feb 28, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,521
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hata mimi jamaa nimewakubali. Wamenivutia sana.
   
 5. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,776
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ni kweli wamejiandaa ila kama sikosei hili tetemeko halijapita katikati ya mji na limepita pembezoni kidogo, hapo ni pa kumshukuru Mungu pia kama linge hit capital nadhani sasa ingekuwa habari nyingine!
   
 6. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  ha, mrembo, kumbe kwa analysis na wewe umo?................ angalau umeanalyse critically................ unajua niko well coversant na human settleent issues, sasa waliotangulia wameignore urban development and human settlement factors.............. kaazi kwelikweli............... kamata mvinyo hapo kwa afta yako...........
   
 7. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,776
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160

  Kidogo najaribu mwayego vipi ishu yako hujatupa feedback lol:rolleyes:
   
 8. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  feedback natundika kesho............... mbona wewe hukuapply na nilisema nitaruhusu kushea na jibwana jingine?....................
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  kiongozi mimi mambo ya chile siko deep...!ILA HILO JINA ULILORUDISHA NDO NIMEKUBALI NA NIMEHAMASIKA KUPOST SREDI:D:D
   
 10. O

  Ogah JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,233
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  My 50cents napendekeza Serikali yetu ijufunze yafuatayo:

  1.Physical Planning (both to urban and rural)
  2.Ku-enforce building code (kama ipo)
  3.Environment Protection (enforcement)
  4.Public Education and awareness campaign
  5.Kitengo/Kikosi cha maafa kiondolewe OPM.......Kiundwe Kikosi/Kitengo Maalum kitakachoshughulikia maafa (Kambi za JKT zaweza kutumika kama centres za vikosi hivyo).....Kikosi hicho kishughulikie ku-enforce hayo hapo juu
  6.Serikali Itenge resources kuhakikisha hayo hapo juu yanatimia ikishirikiana na private sectors
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,524
  Likes Received: 576
  Trophy Points: 280
  Nafikiri funga kazi ni Wajapan na hasa inapokuja maswala ya metetemeko ya ardhi. Hawa jamaa wamejizatit haswa na wametoa hadi shule kwa watu wao wafanye nini yakitokea.

  Hongera Chile.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Mar 1, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,301
  Likes Received: 1,059
  Trophy Points: 280
  Kuna mengi ya kujifunza siyo tu kutoka Chile bali hata kutoka Haiti kutokana na matetemeko haya. Kubwa ni kuwa tunatakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na plan B kutokana na ukweli kuwa maafa mengi ya asili kama vile matetemeko, mafuriko vimbunga, volcano na kadhakli hutokea bila kutoa taarifa.

  Hata hivyo madai yako kuwa tetemeko la Chile ambalo lilipima Richter 8.8 liltakiwa lilete madhara makubwa zaidi kuliko lile la Haiti ambalo lilikuwa Richter 7.0 siyo sahihi kabisa katika kupima madhara ya matetemeko. Hiyo Richter scale inayotumika kukokotoa nguvu ya tetemeko inaunganisha mambo mawili: urefu wa mtikisiko wa ardhi kwenda juu na chini (vertical amplitude) na urefu wa juu ya ardhi au ukubwa wa eneo lililotikisika. Inawezekana mtikisiko wa kwenda juu usiwe mkubwa lakini ukawa umetokea katika eneo kubwa sana hivyo Richter magnitude ikawa ni kubwa sana pia, na vile vile inawezekana mtikisiko ule ukawa ni mkubwa sana wa kutisha lakini ukawa umetokea eneo dogo tu hivyo Richter magnitude yake ikawa siyo kubwa sana. Kwa sasa hivi wataalamu wa seismology wanashughulika ili kuweka kipimo sahihi zaidi cha madhara ya tetemeko locally badala ya hiyo Richter ambayo inapima nguvu ya tetemeko katika eneo kubwa (distributed.)


  Pamoja na ubovu wa infrastructure na standards za majengo ya Haiti, kumbuka kuwa ile ikulu yao ilikuwa imejengwa imara sana kuhimiri matetemeko kwa standards za kisasa sawa na zinazutumika eneo lote lile including Chile. Hata hivyo Ikulu ile bado ilianguka wakati nyumba za aina hiyo huko Chile hazikuanguka. Tofauiti hapa ni kuwa mtikisiko wa Haiti ulikuwa ni wa nguvu sana kuliko ule wa Chile, ila ulitokea kwenye eneo dogo tu la mji wa Port Au Prince.wakati lile la Chile halikuwa na nguvu kama zile za Haiti lakini lilitokea katika eneo kubwa sana tena ndani ya maji.
   
 13. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 827
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Haiti's earth quake ilitokea saa 5pm, wakati wa rush hr , halafu watu wengi wamekufa , mbona ina nishangaza , wakati huo si wengi watakua barabarani wakielekea nyumbani na wengi ambao hawana kazi watakua mtaani wakizurura au kupanga kuibia wasafiri, inakuaje watu wengi walikufa au ni ndio kuongeza idadi ili michango ije ,wachache wale? , mana ile nchi rushwa na ufisadi ni no 1.
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,233
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  Shule murua kabisa hapo juu asanteni sana wakuu
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Mafuriko kilosa tu yametushinda, hadi blogger wa JF akaanza kuhamasisha watu kuchangia wahanga. Usafi wa mji wa Dar es saalaam umetushinda kabisa, ambai hauhitaji teknolojia wala msaada kutoka nje. Unayozungumzia ni madogo sana na huenda yapo kwenye makaratasi yetu, lakini utekelezaji wake ni kama haupo.

  Chile is by far advance than most countries in Americas, na maendeleo yao yantokana na kufuata taratibu zilizowekwa, ikiwa ni pamoja na kwenye miundo mbinu na makazi. They do not have unofficial cities likeHaiti, and the enforce the rules they have.

  Na kuna uwezekano kuwa baada ya tetemeko kama kuna jengo likigundulika kuwa lilijengwa bila kufuata standards basi hatua zinachukuliwa. We can leran this one as well.
   
 16. Companero

  Companero Platinum Member

  #16
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,491
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Nyani Ngabu, tofauti ya Wachile na Wahaiti ni nini?
   
 17. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,717
  Trophy Points: 280
  Hofu yangu ni haya maghorofa ya Dar es salaam, hivi kweli Kariakoo itapona? hata yakitokea yale madogomadogo ya mikoani ?
   
 18. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hii ndo hali halisi huko Chile[​IMG]c

  Majengo pia yalianguka


  [​IMG]

  Madaraja yamevunjika.

  [​IMG]

  magari yametumbukia....

  So la kujifunza,ni wataalam wetu kujua kuwa haya majanga yanaweza kutokea,kutokana na jiografia ya nchi yetu,na yanaweza kuwa na madhara kiasi gani.Hii inahitaji research za mara kwa mara na za kina...ili hivi vikwangua anga vinavyomea katika miji yetu visijegeuka majeneza yetu baadae.Designers lazima wafikirie maswala haya yote ili kuepusha madhara makubwa ya baadae...
   
 19. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 784
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Haya matetemeko hayapashwi kabisa kulinganishwa, La Haiti limetokea nchi kavu wakati la Chile Baharini. halafu population kubwa ya WaChile haiishi pwani ndo pona yao.
   
 20. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nyani,
  Kwa nini unahangaika kushauri tujifunze toka kwa wengine wakati tulishaambiwa kuwa Mtu Mweusi hakuna analoweza kutenda?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...