Kuna anayewafahamu vizuri ForePlan Clinic ya Dr. Mwaka?

Kuna anayewafahamu vizuri ForePlan Clinic ya Dr. Mwaka?

Mganga mkuu mfawidhi wa clinic ya mitishamba😀😀😀😀
 
Mjanja mjanja flani hivi kuibia watu kwa kuaminiwa......Naye atapotea kama Dr.Ndodi.
 
Nami natamani kufahamu CV ya huyu bwana. Dr. Kwa Kuwa anatibu kama Matunge au ni real MD?
 
Mjini ujanja mwingi tuu.tumia bongo yako town.
 
Mganga wa kina mama na anawala sana wagonjwa wake Hana lolote
Nahesgumu
Naheshimu tu sheria za nchi ningefunguka mpaka mwisho. Ngoja lowassa aingie madarakani tutanyooshana tu nchi hii
 
Mganga wa kina mama na anawala sana wagonjwa wake Hana lolote
Nahesgumu
Naheshimu tu sheria za nchi ningefunguka mpaka mwisho. Ngoja lowassa aingie madarakani tutanyooshana tu nchi hii

Mkuu wee Mwaga tu hapa
 
Kama huna ujuacho juu ya mtu huyu ni vema ukanyamaza, watu wanauliza kwasababu ana tiririka, kwa hiyo wanataka kujiridhisha. kwa hiyo kama hujui juu yake ni vizuri ukanyamaza na amini atakuja mwenyewe hapa uwanjani na kujieleza. aweze kwa TV ashindwe hapa jamvini!
 
Binadamu hawana jema,

Acheni kumchafua mtu, wamama wengi tu wamesaidiwa kimatibabu, Tiba mbadala inaruhusiwa.

Usiseme kitu kama huna ushahidi.
 
Niliwahi kuambiwa alikuwa daktari pale Muhimbili akaacha ndo akafungua hosp yake hii ya tiba mbadala. Wenye kujua zaidi watujuze.
 
Siku nilimtest nina shida fulani nikaambiwa nitume laki 300000/=
 
Mimi nimewahi kipata dawa hapo. Zilinishinda sababu nilitibua vidonda vya tumbo niliporudi akasema kwanini hukusema.
Nikapoteza imani kwake sababu hata dawa zingize nilizopewa nesi alishindwa kunipa maelekezo vizuri.
Kama hiyo dawa iliyonishinda ikimwagika chini sakafu inapauka na hairudi kwenye hali yake kama zamani.
Nilipoteza imani na tayali nililipa pesa kibao na dawa nikamwaga.
 
Mpaka sasa sijapata CV yake! Kwann serikali inaachia dhana ya ujasiriamali hadi kwenye afya za watu?au ndio kusema watanzania hawahitaji kupatiwa huduma bora za afya na serikali?
 
Back
Top Bottom