Kuna aliyewahi kuingiza gari kutoka Japan?

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,495
2,250
Kama kuna mtu amewahi kulipitia hili, iligharimu kiasi gani kulitoa bandarini? Tax,agent fees etc.
 
Kama kuna mtu amewahi kulipitia hili, iligharimu kiasi gani kulitoa bandarini? Tax,agent fees etc.
Ok,

Ni 95% ya CIF price kama ni gari la 1999-2005 (mwaka wa kutengenezwa gari) na hiyo ni endapo utakuwa umepitishia Dar.
 
Ok,

Ni 95% ya CIF price kama ni gari la 1999-2005 (mwaka wa kutengenezwa gari) na hiyo ni endapo utakuwa umepitishia Dar.

Pia ikiwa TRA wataikubali hiyo CIF price ktk risiti yako, vinginevyo wanatumia bei yao kwa vigezo vyao - wanaita "uplift (?)". Lakini kama ilivyo mambo mengi Bongo, ni ukadiriaji unaotoa "kula" sana kwa assessors wa TRA kwani hawana formula maalum na ya uhakika kuh kiwango cha kulipa. Na Sijui kama wenzangu mna habari ya utata uliopo juu ya "Year of Manufacture" ambao hata AUTOREC wamemwona TRA Commissioner bila ufumbuzi!!

Gharama za Wakala zinategemea aina ya gari (saloon, mini-bus, bus/truck, p/u) na hata kujuana. Mimi nililipa laki moja na nusu kwa HIACE na akaniambia gari dogo (saloon) ni laki moja.

_______________________________________________________

KIATU CHANGU KIPANA LAKINI KINANIBANA!!
 
Mr Kang, a Rule-of-Thumb ,ukinunua gari dola 3000 basi tegemea gharama zakulitoa(Ushuru,clearing& fowarding) kuwa roughly fedha hiyo hiyo in Tshs(kwa gari ndogo)
 
Nilinunua gari Suzuki Alto ya mwaka 2000 toka itccars.com kwa dola 300 na kusafirisha kwa dola 700. Jumla C&F Dar ikafika kama dola 1500. TRA wakanigomea kata kata pamoja na kuwaonyesha website lakini wapi. Wakauplift mpaka dola 2000. Wakapiga hesabu ya ushuru ikaja milioni 3 na. Nililisusa gari bandarini mpaka akatokea clearing agent mmoja akasema nimpe 1.5 alete gari mpaka mlangoni. Nikampa within a week, gari liko mlangoni. Mpaka sasa ngoma ni usajili maana jamaa kacheza deal front paperwork imemgomea. Hivyo kuwa makini sana na hawa wacheza deal, rahisi isije kuwa ghali.
 
Ukitaka ujue nchi yetu imeoza agiza gari Nje, then uanze harakati za kulitoa bandarini...Utajuta kunnua...Wengi wameyasusa magari yao!!!...Huwa natamani niwatukane watu wa TRA...watu ambao umesoma nao, wana kila aina ya vitu vya ufahari..wakati wewe umekomaa unatafuta vya HALALI, wenzako kula HARAMU ishakuwa jambo la kawaida...

The whole TAX system BONGO ipo Hovyo, inatoa mianya ya Rushwa sana....

Hakuna mtu anaekataa kulipa TAX kwa maendeleo ya nchi...wao wanaweka hesabu za Ajabu ajabu mno...Waweke tu TAX 100%, hizo breakdown wazifanye wao maofisini...pia wakuliane na real price ya uliponunua...

Ma-Evaluator sijui wana nongwa gani...hawa ma-evaluator hebu wafike soko la magari Japan, UK au Dubai , Hongkong, waone bei za magari...wao evaluation wanatoa wapi? wao ndio wametengeneza?...ktk sytle kama hii Rushwa ndio inapokomaa....na watu kama hawa wakiamishwa tu ofisi....basi huwa wanajiua!!!! they cann't survive...na Mishahara yao!!!

Nawashauri wadau wote mlete magari yenu ZNZ....hakuna usumbufu sana. One day gari umetoa.!!!..na Agent bei yake kama 50,000. na Nimesikia siku hizi Namba za usajili the same Bongo na ZNZ...

Kutoa gari znz kuja bara takriban 350-500,000 kutegemea na size of the car...

mwenye data zaid aseme....
 
Hiyo ni sawa sawa, Ila number bado mgogoro. Lazima ubadilishe. Pitishia gari lako Znz kabla hawajastuka. Maana nahisi mwaka huu wanaweza kuweka pin baada ya watu wengi sana kupitishia kule kwa wakati huu.
 
CIF VALUE X CURRENT XRATE
X 25% IMPORT DUTY
X 20% VAT..
Hiyo ndo standard kama gari YOM si not older than ten years and cubic capacity has not exceed 1000..if so, then the computation has to be like this:
CIF X XRATE
X 25% IMPORT DUTY
X 5% ECISE DUTY IF CC >1500 BUT NOT EXCEEDING 2500
X 10% EXCISE DUTY IF CC >2500 AND ABOVE +
X 20% IF OLDER THAN 10 YEARS.
X 20% VAT

natumai nimeeleweka...
 
Ukiritimba wa hii bandari yetu DSM umezidi mpaka unakera.
Kwa gari ya CC less or eqaual to 2000 cumulative tax ni 50 % while kwa CC beyond that am told ni 65%.
Ngoma ipo kwenye evaluation ya gari apo TRA sijui huwa wanatumia formular gani.
Yangu iko njiani ndo najipanga ila kuna mshikaji mzoefu kasema haina kwele.
Ni toyota CAMI YA 2000 nimeinua kwa dola 6000 CIF DSM nimeambiwa kodi ni kati ya 2.5m -3m
 
__________________
happylandin n drive safe
 
MLISHAKUMBANA NA ISSUE YA MIKANDAAAAAAA
kuna upumbavu wa kuangalia mikanda eti ndiyo inaonyesha manufacture date ya gari. hii ni njia ya ulaji ya jamaa wa TRA. Ukiuliza hata japan wanakwambia kuwa mikanda inatengenezwa na viwanda vingine na hununuliwa kama item nyingine na haina uhusiano na gari imetengenezwa lini.
 
Watanzania bado hatujajuana tu? kwamba kila anaepata wadhfa na madaraka kidogo hutumia manyanyaso na kero kwa anaowahudumia, ili iwe chanzo cha yeye huyo Afisa ati aonekane wa maana, anyenyekewe, na kuogopewa na wale wajuu zaidi kujidhania Miungu! hiyo ndio mbinu kuu ya Mla Rushwa. Akishakudhalilisha unamtafutia Hongo unampa tena ukiamini unampa Haki ya Wajibu wake. Wengine bado wana mawazo Lala kuwa Gari ni chombo cha anasa cha kufanyia starehe, hivyo ukiweza kumiliki basi utajiri na unapaswa kukomolewa. kumbukeni nchi inakotoka hata Simu na Friji vilihesabiwa anasa TV ndio hungethubutu kuitaja, leo yamepita. Tunaingia 2009 na haya mambo ya kitu kidogo bado yanakaza kamba, wapi mwisho wake? na wapi mwisho wetu? GARI LA KAWAIDA SI ANASA NI NYENZO MUHIMU KWA SHUHULI ZA MAENDELEO hivyo mletaji ,mtumiji aangaliwe vema na utaratibu.
 
Mimi nilinunua gari aina ya Toyota Surf '96 model C & F Dar $8000 kutoka Dubai nimelipa 12million ilikuwa mwaka wa jana 2007. Jirani yangu naye aliagiza kama hilo la kwangu muda huo huo tena la kwake engine ilikuwa na cc kubwa yeye amelipishwa 6million. Kwa hiyo kweli jamaa hawana formula inayo eleweka.
 
Na vipi kuhusu tax exemption kwa waajiriwa wa serikali (civil servants)? Yaani katika
VAT, IMPORT TAX, EXCISE DUTY na kodi nyinginezo ni zipi hasa huwa exempted?
 
Hata matrekta ushuru wake ni kama magari mengine? Nilidhani yana unafuu wa kodi. Naomba kueleweshwa.
 
Wafanyakazi wanasamehewa VAT (20%) tu, lakini shida utakayopata kujaza na kusainiwa hizo fomu hata huo msamaha hauna maana, kodi zilizobaki wanalipia. Hata matrekta halikadhalika.
Note:
1. Cars/trucks used less that 10 yrs:Kodi zake ni, 25% import duty, 20% VAT, 5%or 10% (depending of the engine size), so taxes ni 50% or 55% of CIF value. Plus, port charges.

2. Kama imetumika zaidi ya miaka 10, then ongeza 25% tax (scrap tax) on top of 50% or 55%. Jumla 75 - 80% of CIF.

Ukitaka kufuata utaratibu huna haja ya kuhonga mtu. Ila ukitaka kodi zipungue kidogo hapo ndio akili mumtwi.
 
Shughuli ya kuingiza gari ni noma! Ni mwezi uliopita tu nimeimaliza hiyo...mmmh kidogo miliache majembe waje walishughulikie....TRA is crap!
Kwa yule anayeta kuingiza gari ni bora akaonana na moja wa importers pale dar, watakuchaji kiasi lakini usumbufu wote unakuwa wao na ni wazoefu wa kudeal (kuhonga?) na manyang'au wa TRA.
 
...Kwa maana hiyo, mwisho wa yote ni afadhali uende pale tawi la Autorec uwaonyeshe gari unalotaka halafu uwaachie wao ndio wakuletee, si ndio??
 
...Kwa maana hiyo, mwisho wa yote ni afadhali uende pale tawi la Autorec uwaonyeshe gari unalotaka halafu uwaachie wao ndio wakuletee, si ndio??

Kama hauna haraka waachie kila kitu hawa ila kama una haraka hawa jamaa hawafai, mi niliagiza gari july 2007 nikalipata february 2008, nitaka ku cancel transaction wakaniambia wanakata 20% ya CIF niliyolipia yaani ilikuwa nuksi. Ila magari yao ni quality sana hawa jamaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom