Bwana YESU asifiwe!
Aina ya kwanza ya ndoa ni:
1.Ndoa ya kutungua
> Hii ni ile ndoa ambapo watu wanakutana tu na kupendana na hapohapo wanaanza mahusiano kwenda guest. Huyu anasema "nimekuzimia" na huyu anasema "na mimi nimekuzimia" kisha wanakwenda kuzimika pamoja guest. Ndoa hii inafananishwa na nguo dukani umeona unataka,ukiona nyngne nzr unataka kwa iyo unatungua tu.
Aina ya pili:
2.Ndoa ya mashono
> Hii ni ndoa inayofananishwa na nguo kushona kwa fundi. Hapa kuna utaratibu vipimo lazima vifanyike vzr kuona kama inakutosha. Hii ndipo taratibu za kikanisa zinafuatwa bila hata ya kukutana kimwili.
>Ndoa hii pia ina baraka kwa kuwekewa mikono na wachungaji.
> Ninawaombea MUNGU awape NEEMA ya kufunga ndoa ya mashono katika jina la YESU KRISTO.
AMEN