Kuna aina 2 za ndoa. Je, yako ni ipi?

Kuna aina 2 za ndoa. Je, yako ni ipi?

Mwinjilist mtume nabii

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2015
Posts
2,437
Reaction score
1,100
Bwana YESU asifiwe!

Aina ya kwanza ya ndoa ni:

1.Ndoa ya kutungua
> Hii ni ile ndoa ambapo watu wanakutana tu na kupendana na hapohapo wanaanza mahusiano kwenda guest. Huyu anasema "nimekuzimia" na huyu anasema "na mimi nimekuzimia" kisha wanakwenda kuzimika pamoja guest. Ndoa hii inafananishwa na nguo dukani umeona unataka,ukiona nyngne nzr unataka kwa iyo unatungua tu.

Aina ya pili:

2.Ndoa ya mashono

> Hii ni ndoa inayofananishwa na nguo kushona kwa fundi. Hapa kuna utaratibu vipimo lazima vifanyike vzr kuona kama inakutosha. Hii ndipo taratibu za kikanisa zinafuatwa bila hata ya kukutana kimwili.

>Ndoa hii pia ina baraka kwa kuwekewa mikono na wachungaji.

> Ninawaombea MUNGU awape NEEMA ya kufunga ndoa ya mashono katika jina la YESU KRISTO.

AMEN
 
Maduka ya nguo za kutungua au ready made yanakuwa na vyumba chenye kioo kwa ajili ya kujaribisha hizo ngu kabla ya kununua. Na watu wengine wanajua size zao hivyo husoma tu kwenye label na kununua. Halafu hiyo ya mashono lazima kupima sehemu zote kabla ya kushona.
 
Bwana YESU asifiwe!

Aina ya kwanza ya ndoa ni:

1.Ndoa ya kutungua
>Ndoa hii inafananishwa na nguo dukani umeona unataka,ukiona nyngne nzr unataka kwa iyo unatungua tu.

Aina ya pili:

2.Ndoa ya mashono

> Hii ni ndoa inayofananishwa na nguo kushona kwa fundi. Hapa kuna utaratibu vipimo lazima vifanyike vzr kuona kama inakutosha. Hii ndipo taratibu za kikanisa zinafuatwa bila hata ya kukutana kimwili.

>Ndoa hii pia ina baraka kwa kuwekewa mikono na wachungaji.

> Ninawaombea MUNGU awape NEEMA ya kufunga ndoa ya mashono katika jina la YESU KRISTO.

AMEN

Umesahau aina ya tatu ya ndoa ambayo ni NDOA YA MTUMBA (USED) Aina hii ya ndoa ni ile ambayo unakutana na mke/mme ambaye alishaachika na mnazimikiana mnaamua kulianzisha. Aina hii ya ndoa inadumu kuliko hiyo ya kupima. Si unajua sifa ya nguo za mtumba zinadumu sana.
 
Duh...umetisha!
 
Zipo nyingine ni za kushona lakini zimekaa kama za kutungua, wahusika hawana furaha ndani ya ndoa yao wala amani ya Moyo ktk maisha yao
 
Back
Top Bottom