Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,772
- 35,770
Last edited by a moderator:
Wanabodi,
Nimefuatilia mkutano wa hadhara wa CUF kutoka uwanja wa Mnazi Mmoja Zanzibar, kupitia Star TV, CUF wametangaza wazi kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ndiye atakaye apishwa kuwa rais wa Zanzibar, Novembar 1, mwaka 2015!.
Kwa vile uchaguzi wowote ni ushindani, japo kauli hiyo ya CUF inaweza kuwa ni kauli tuu ya kujipa matumaini, ila pia kwa siasa za Zanzibar, ni kweli kuna uwezekano wa CCM kushindwa Zanzibar.
Kwa vile Zanzibar inatawaliwa na SUK, mshindi wa urais ndiye Rais na mshindwa huwa Makamo wa kwanza wa rais, kwa kuzingatia uwezekano wa CCM kushindwa Zanzibar, hivyo kama watamsimamisha tena Dr. Shein, na CCM ikashindwa, hii inamaanisha Dr. Shein atakuwa demoted kutoka rais hadi kuwa Makamo wa Rais!, hii itakuwa ni aibu kwa Dr. Shein!.
Hivyo nashauri, hata kama CCM inajua kuwa ni lazima itashinda uchaguzi wa Zanzibar kwa kutumbia mbunu zile zile!, ila sio vibaya kuweka akiba ya uwezekano wa mbinu hizo kushindwa this time, ili kumtunzia heshima, nawashauri wasimsimamishe tena Dr. Shein kugombea urais wa Zanzibar, ili kumuepushia na aibu ya kushindwa, bora Dr. Shein achagizwe kugombea urais wa Muungano ambako huku atashinda straight forward!.
Huu ni ushauri tuu wa bure, sio lazima ufuatwe!.
Jee CCM Zanzibar iendelee kumsimamisha Dr. Shein au imuepushie na aibu ya kushindwa?!
Pasco
Nasubiria kutimia kwa maneno ya unabii huu!.
Pasco
Pasco aka nabii aka mtabiri kwenye ubora wake
UR Right!. Pole!.Prejudice. Nilidhani wewe ni mwandishi wa habari. Sorry buddy
Mimi naona.Dr Shein aachie kiungwana then,CCM Ipendekeze mtu mtu mwingine awe makamu wa rais kama katiba ya Zanzibar inaruhusu
Naam Pasco. Ulinena aisee.Na Seif kawashika "pabaya".Ukiamka nchare,ukikaa nchare,ukikimbia nchare'. Mbaya zaidi hata international media zimemsikia.Akiongea "FACTS"..Je ZEC watatangaza matokeo halisi ya vituoni au watapika yao...Let's wait.
Pia natamani huku ng'ambo napo unabii wako utimie.