Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,426
Reaction score
133,821
Wanabodi,

Nimefuatilia mkutano wa hadhara wa CUF kutoka uwanja wa Mnazi Mmoja Zanzibar, kupitia Star TV, CUF wametangaza wazi kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ndiye atakaye apishwa kuwa rais wa Zanzibar, Novembar 1, mwaka 2015!.

Kwa vile uchaguzi wowote ni ushindani, japo kauli hiyo ya CUF inaweza kuwa ni kauli tuu ya kujipa matumaini, ila pia kwa siasa za Zanzibar, ni kweli kuna uwezekano wa CCM kushindwa Zanzibar.

Kwa vile Zanzibar inatawaliwa na SUK, mshindi wa urais ndiye Rais na mshindwa huwa Makamo wa kwanza wa rais, kwa kuzingatia uwezekano wa CCM kushindwa Zanzibar, hivyo kama watamsimamisha tena Dr. Shein, na CCM ikashindwa, hii inamaanisha Dr. Shein atakuwa demoted kutoka rais hadi kuwa Makamo wa Rais!, hii itakuwa ni aibu kwa Dr. Shein!.

Hivyo nashauri, hata kama CCM inajua kuwa ni lazima itashinda uchaguzi wa Zanzibar kwa kutumia mbunu zile zile!, inazotumia katika chaguzi zote za Zanzibar na kushinda kirahisi, sio vibaya kuweka akiba ya uwezekano wa mbinu hizo kushindwa this time, kufuatia kuongezeka kwa tansparency kwenye uchaguzi, sasa ili kumtunzia heshima rais wa sasa, nawashauri CCM Zanzibar, wasimsimamishe tena Dr. Ali Mohamed Shein kuwa Mgombea wake wa urais wa Zanzibar, ili kumuepushia na aibu ya kushindwa, bora CCM, wamlete Dr. Shein kugombea urais wa Muungano ambako huku hakuna any credible opposition, mgombea yoyote atakayesimamishwa na CCM, hata awe ni kiazi vipi, ndiye atashinda straight forward na kuwa rais wa JMT, lakini Zanzibar, kuna kazi!.

Huu ni ushauri tuu wa bure, sio lazima ufuatwe!,sababu za kwanini Dr Shein atashindwa Zanzibar, nazijua lakini naomba nisizitaje!.

Jee CCM Zanzibar iendelee kumsimamisha Dr. Shein na kukubali aibu ya kushindwa, au imuepushie na aibu ya kushindwa, au mambo yatakuwa kama ile kawaida yao ya Zanzibar, ashinde asishinde, nchi ya Mapinduzi haiwezi kukabidhiwa kwa waliopinduliwa kwa kipande cha karatasi, hivyo ZEC watafanya mambo kama kawa?.

Pasco

Update
Hili lilikuja kutokea ila ili kumuepushia aibu hii, uchaguzi ulifutwa Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda
P
 
yaani pasco hata mkutano haujaisha kuona watu wanapinga katiba pendekezwa umeogopa au unapima upepo?
 
Wanabodi,

Nimefuatilia mkutano wa hadhara wa CUF kutoka uwanja wa Mnazi Mmoja Zanzibar, kupitia Star TV, CUF wametangaza wazi kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ndiye atakaye apishwa kuwa rais wa Zanzibar, Novembar 1, mwaka 2015!.

Kwa vile uchaguzi wowote ni ushindani, japo kauli hiyo ya CUF inaweza kuwa ni kauli tuu ya kujipa matumaini, ila pia kwa siasa za Zanzibar, ni kweli kuna uwezekano wa CCM kushindwa Zanzibar.

Kwa vile Zanzibar inatawaliwa na SUK, mshindi wa urais ndiye Rais na mshindwa huwa Makamo wa kwanza wa rais, kwa kuzingatia uwezekano wa CCM kushindwa Zanzibar, hivyo kama watamsimamisha tena Dr. Shein, na CCM ikashindwa, hii inamaanisha Dr. Shein atakuwa demoted kutoka rais hadi kuwa Makamo wa Rais!, hii itakuwa ni aibu kwa Dr. Shein!.

Hivyo nashauri, hata kama CCM inajua kuwa ni lazima itashinda uchaguzi wa Zanzibar kwa kutumbia mbunu zile zile!, ila sio vibaya kuweka akiba ya uwezekano wa mbinu hizo kushindwa this time, ili kumtunzia heshima, nawashauri wasimsimamishe tena Dr. Shein kugombea urais wa Zanzibar, ili kumuepushia na aibu ya kushindwa, bora Dr. Shein achagizwe kugombea urais wa Muungano ambako huku atashinda straight forward!.

Huu ni ushauri tuu wa bure, sio lazima ufuatwe!.

Jee CCM Zanzibar iendelee kumsimamisha Dr. Shein au imuepushie na aibu ya kushindwa?!

Pasco

Miaka yote ktk chaguz cuf huwa wanashinda ila wanaminywa hilo sio geni mkuu ndi mana waliamua kumpa kacheo maalim seif kuogopa machafuko ili watulie saiv wakipita cuf tena cjui kama watakubali.
 
Nhnnn...ya Zanzibar si mepesi mwaka huu. Kama ccm ikitaka kutumia mbinu zilezile za zamani wajue kuna cha-moto toka pande zote. Waamue kusuka au kunyoa. Walitegemea sana serikali wakati huo....na Maalim akiwa nje ya mfumo huo...leo yuko ndani. Nayaona ya Sudani Kusini Nov 2015 unless.....
 
Pasco, Mbona yule mwingine alikuwa Waziri Mkuu akapigwa chini akabakiwa na Ubunge mbona hukusema ni demotion imtamuaibisha?
Mkuu, ile ni ajali tuu ya kisiasa!, ndio maana alijikalia kimya amejikunyata, sasa ndio anataka kuamkamka na kupanda kule kileleni akamalizie majukumu yake!.

Sasa kwa taarifa yako tu Shein atakuja kugombea huku, kule anaachiwa kijana wangu Nahodha. Yule jamaa yetu kile kigezo cha afya kimesha haribu fomesheni...
 
Kitakacho washangaza WaTanganyika ni kwamba Dr. Shein atasimamishwa kugombea kwa tiketi ya CCM serikali ya muungano, na kuna kwa makadirio ya karibu, atashinda, halafu kule Zenji upinzani wanaelekea kuchukua madaraka kwa kushinda uchaguzi wa Visiwani. Hivyo Rais wa kule mwenye mwelekeo wa kuvunja au kubadili mfumo wa muungano ataendelea kufanya vitu vyake huku Watanganyika wakijikuta wanatawaliwa na kiongozi Mzenji wakati muungano unaoeleweka hautakuwepo tena!! Hii ndio itawazindua macho Watanganyika waliolala usingizi wa kisiasa!! Watatambua maana ya usemi, "changu ni changu na chako ni chetu". Subiri tu, yengu macho!!
 
Mkuu Mike, kama huwa wanashinda na hawapewi, nini kitakachofanya safari hii wapewe?!.Pasco
 
Ukiona hivi ujue matarajio ya PASCO yako ....kwenye kona yani watu wamekaba mpaka penati....sasa lililopo ni kubamiza tu ata vile vinyongo vinyongo vilivyobakiki baada ya malaria iliyokaa tumboni uwenda vikaibua kutabika na kuutibua Mwili kutoka kwenye hali fulani iliyotulia kuhamia kwenye homa ya nyongo.

Anyway Pasco unajua jambo lako hili unalolijadili hapa lilikuwa kwenye rasimu ya Warioba, Wazanzibar hao hao kupitia Bunge la Katiba wakalibomoa, na kupitia hapo ndio lilikuwa lipate suluhu. Kwa kuwa enzi za Mwalimu kulikuwa na Serikali Mbili Nchi moja na sio za sasa hivi Nchi Mbili Serikali Mbili....Ukiijua sentensi hiiyo basi UHALALI wa Wazanzibar kuomba Rais wa 2015 Tanzania atoke kwao ushapoteza maana toka walipoamua kuwa na Katiba yao na nyimbo zao.Ndio maana hata wao wenyewe unawaona wapole wana hawana munkariii ....sema jingine Pasco.
Re: Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano, 2015 Si Zamu ya Zanzibar?

Kamchezo hako kaishie huko huko Zenj!!cause i know where are you heading too...ile ya kusema tukose wote haipo brother Tanzania Bara ni Bara tuuu...hakuna zile za dakika ya mwisho speaker anatakiwa wa jinsia ya kike, huku waliochukua form wako wanaume...mmmhh.
 
Mkuu Mike, kama huwa wanashinda na hawapewi, nini kitakachofanya safari hii wapewe?!.Pasco

Kuna allowable threshold ya kuchakachua matokeo. Lakini MARGIN ya ushindi inapokuwa kubwa huwezi kuchakachua tena matokeo. Tumeona huku bara kwenye Ubunge.

Hivyo AVALANCHE ya UKAWA itampa ushindi mkubwa Maalim Seif ambao hauwezi KUCHAKACHULIKA!

Tanzania ni nchi ya maajabu, ina muungano wa kipekee ambao haupo dunia popote! Lakini ajabu hakuna nchi yeyote duniani iliyowahi kuuiga.

Na kwa maajabu hayo tusubiri kushuhudia AJABU jingine la karne ya 21, aliyekuwa RAIS anakuwa MAKAMU WA KWANZA wa RAIS na aliyekuwa MAKAMU WA KWANZA WA RAIS wa rais anakuwa RAIS.
 
nadhani kama uchaguzi znz ungekuwa fair shein hatagombea znz, lakini kwavile wenyewe wanajua wanachofanya shein atagombea kama kawaida
 
Wanabodi,

Nimefuatilia mkutano wa hadhara wa CUF kutoka uwanja wa Mnazi Mmoja Zanzibar, kupitia Star TV, CUF wametangaza wazi kuwa Maalim Seif Sharif Hamad ndiye atakaye apishwa kuwa rais wa Zanzibar, Novembar 1, mwaka 2015!.

Kwa vile uchaguzi wowote ni ushindani, japo kauli hiyo ya CUF inaweza kuwa ni kauli tuu ya kujipa matumaini, ila pia kwa siasa za Zanzibar, ni kweli kuna uwezekano wa CCM kushindwa Zanzibar.

Kwa vile Zanzibar inatawaliwa na SUK, mshindi wa urais ndiye Rais na mshindwa huwa Makamo wa kwanza wa rais, kwa kuzingatia uwezekano wa CCM kushindwa Zanzibar, hivyo kama watamsimamisha tena Dr. Shein, na CCM ikashindwa, hii inamaanisha Dr. Shein atakuwa demoted kutoka rais hadi kuwa Makamo wa Rais!, hii itakuwa ni aibu kwa Dr. Shein!.

Hivyo nashauri, hata kama CCM inajua kuwa ni lazima itashinda uchaguzi wa Zanzibar kwa kutumbia mbunu zile zile!, ila sio vibaya kuweka akiba ya uwezekano wa mbinu hizo kushindwa this time, ili kumtunzia heshima, nawashauri wasimsimamishe tena Dr. Shein kugombea urais wa Zanzibar, ili kumuepushia na aibu ya kushindwa, bora Dr. Shein achagizwe kugombea urais wa Muungano ambako huku atashinda straight forward!.

Huu ni ushauri tuu wa bure, sio lazima ufuatwe!.

Jee CCM Zanzibar iendelee kumsimamisha Dr. Shein au imuepushie na aibu ya kushindwa?!

Pasco
Nasubiria kutimia kwa maneno ya unabii huu!.

Naam Pasco. Ulinena aisee.Na Seif kawashika "pabaya".Ukiamka nchare,ukikaa nchare,ukikimbia nchare'. Mbaya zaidi hata international media zimemsikia.Akiongea "FACTS"..Je ZEC watatangaza matokeo halisi ya vituoni au watapika yao...Let's wait.
Pia natamani huku ng'ambo napo unabii wako utimie.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom