Kumradhi Mh Zitto Kabwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumradhi Mh Zitto Kabwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masatu, Oct 14, 2009.

 1. M

  Masatu JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mh Zitto, nianze kwa kukiri mimi nilikuwa miongoni mwa wana JF wengi tuliokuzonga kwa kejeri, shutma, kashfa na dhihaka kadha wa kadha kuhusiana na msimamo wako kwenye suala zima la ununuzi wa mitambo ya Dowans.

  Mheshimiwa, ulikuwa sahihi kwa kusimamia kile unachoamini ni sahihi. Hii ndio sifa adimu ya kiongozi. Naamini hata wewe mwenyewe ulijua toka mwanzo kuwa uamuzi wako wa kutetea ununuzi wa mitambo ile hautakuwa popular na pengine ni kitanzi cha kisiasa. Lakini kwa ujasiri usiomithilika uliendelea kujenga hoja na wengi tulitia pamba masikioni mwetu na kukuita majina mabaya lukuki. Binafsi nilikwenda mbali zaidi na kukuita fisadi. Hili ndilo limenisukuma kuandika waraka huu mfupi ili kukuomba msamaha kwa maandishi yote machafu juu yako. Naamini tupo wengi wa aina hii lakini wenzangu wanakosa uthubutu wa kukiri na wanajichimbia kwenye keyboard zao.

  Taifa leo lipo latika kiza, kwa sababu ya watu wachache waliokataa ushauri wa wataalam. Wale "wapiganaji" wanaona soni nyuso zimewashuka wanatapatapa kutafuta justification ya uamuzi wao mbovu ambao umeligharimu na utaendelea kuligharimu taifa kwa hasara kubwa.

  Mheshimiwa watani zangu wazaramo wana msemo ufuatao "akutukanae kilabu cha pombe usisubiri kesho yake na wewe mrudishie matusi yake huko huko kilabu cha pombe" Kwa kuwa kashfa nilizitoa hapa JF nalazimika kuomba msamaha hapa hapa JF na ni matumaini yangu utanisamehe.

  Nimalizie kwa kukiri na kusema kuwa Mh, wewe ni hazina ya taifa hili. Kama kiongozi vision yako ni kubwa kuliko umri wako. Pamoja na kuwa wanasiasa wanaepuka sana kujiingiza katika masuala tata kwa kuchelea kushusha credibility zao wewe umeweka utanzania wako mbele bila kuogopa kupoteza umaarufu wako wa kisiasa and spot on, you got it right.

  Bravo Mh Zitto na endelea na misimamo yako thabithi yenye manufaa kwa taifa letu.

  Mheshimiwa naomba kuwasilisha
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  The World of Paranormal Experience is rife!!
   
 3. A

  August JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  wataalamu hawakushauri tununue mitambo ya wizi, walio toa uamuzi wa kununua mitambo ya wizi ni idrisa akisaidiwa na baadhi ya wapambe ambao wengine hatujajua nini ili kuwa interest yao. walicho sema wataalamu ni kununua mitambo in general, specific ilikuja kwa watawala au viongozi, ku-source hiyo mitambo ya wezi, ambao mpaka leo hii aliyekuwa analipwa hizo hela hatuambiwe, kwanini? kama hakuna kitu cha ajabu?
   
 4. M

  Masatu JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  spinning....
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Masatu,
  CCM ndivyo mlivyo.
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  How about this:
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Is Zitto CCM? je wewe chama gani homeboy?
   
 8. A

  August JF-Expert Member

  #8
  Oct 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,511
  Likes Received: 724
  Trophy Points: 280
  jibu specific, na sio sweeping statement ambayo ina beba mazuri na uchafu, je aliye lipwa hela richmond aka dowans ni nani? na hii hela ya mitambo tutampa nani?
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Oct 14, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  kwi!kwi!kwi!
  Mimi mtoto yatima.
   
 10. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Jasusi huyu ni Masatu kweli ama kuna nguvu nyuma ya Masatu ? Huge U turn indeed
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Masatu,
  Mkuu wangu labda wewe omba radhi kwa sababu unachobishana hapa JF ni ubishi tu usiozingatia umuhimu wa hoja nzima ya mahitaji yetu.
  Zitto na viongozi wengine wote wanafikiria kama wewe, yaani kutatua tatizo ndio mpango yakinifu wa maendeleo yetu..kwa njia hiyo hatuwezi kuwa wabunifu hata kidogo..Hatuwezi kujenga mipango bora ya ujenzi wa taifa letu changa na maskini ikiwa tunafikiria kutatua marttatizo kama vile maskini mwenye njaa anayetafuta mlo wa siku..
  Mawazo ya Zitto yaweza kuwa mazuri kwa sasahivi kwa sababu tu tuna njaa, lakini ktatizo mloshindwa kuliona ni kuuza mwili wetu kwa sababu ya mlo wa siku. Kesho tutaendelea kuuza mwili na mwisho wake kuzoea umalaya wa kuuza mwili, jambo ambalo Zitto, Lipumba na viongozi wengine wameshindwa kuliona.
  Mkuu wangu kama serikali imeshindwa kutekeleza hata mradi mmoja wa ufaji umeme kama tulivyoahidiwa, Zitto alitakiwa kusimama upande wa pili kama kiongozi wa Upinzani ambaye analitakia mema Taifa letu badala yake amejiunga na mpango wa kutatua matatizo tuliyokuwa nayo kwa njia ya Umalaya.

  Well wewe unaweza kuomba samahani lakini navuyojua mimi njaa hiyo ya siku mbili tatu, hatujafa bado.. kweli tuna shida lakini hatuwezimkuuza mwili wetu kwa sababu Zitto kasema.
  As a fact mimi naunga sana mpango wake wa kuachana na siasa kutogombea Ubunge arudi kazini akafanye kazi alosemea..I thought he stand with us kama wapinzani wa utawala huu unapofikia maswala mazito kama haya lakini anapounga mkono upotoshaji huu kwa sababu tu matokeo yake yamepangwa kuwa hivyo... nasikitika kusema kachuuzika! He is a Lost boy kisiasa!
   
 12. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Hahahahah,

  Yaani Zitto atakuwa mtu wa ajabu kusikiliza porojo kama hizo. Hata nikibaki peke yangu, sitasita kusema kuwa Zitto hakuwa sahihi katika ushauri wake kwamba tumwage pesa nyingine kuwalipa wezi (DOWANS a.k.a Richmond). Na kama ni kulipa fadhira basi aendelee na kampeni zake! Dowans ni wizi hata ikibidi kukaa gizani hadi JK aondoke madarakani ni poa tu! Wasitufanye wajinga. Ipo siku siri iliyojificha ya Zitto kuwa kipenzi cha watawala na CCM kwenye hili suala la Dowans itafichuka. Nitabki Tomaso milele!
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Dark City,
  Mkuu wangu umesema kweli.. wakati wa Mkapa tulikaa kizani karibu mwaka mzima..Sikumsikia Zitto wala machizi wengine wakizungumza lolote kana kwamba wananchi tumeshasahu hali ile...Yote hii Zitto anacheza ili Kigoma wapate generator ambayo kaahidiwa kama Tanesco watachukua mtambo huu.... hakuna zaidi, ni mchezo wa CCM...
  Janja yao kwisha gundua!
   
 14. Nzokanhyilu

  Nzokanhyilu JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 19, 2007
  Messages: 1,087
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Duh, hii fresh. Ndio maana nimeuliza kule hivi watu bado wanamsikiliza? Stand yake ilionyesha yeye ni kiongozi asiyeona mbali na ana mawazo ya kuziba ufa kuliko kujenga ukuta.
  Sometimes one needs to suffer, go through hard times, so that they can say....damn am never gonna go through that again. Sasa hii ishu ya umeme ndio inatakiwa watu wa experience tu, ila kama Dowans itanunuliwa itaonyesha jinsi waafrika tulivyo wajinga.
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Poa Mkuu, nimekupata.

  Ila kama huyu kijana angekuwa mjanja basi angekaa kimya. Sasa si unaona anataka kutuletea uchuro? Naamini ataanza kusuta watu kama alivyowahi kutoa maneno ya jeuri na kejeli hapa JF? Alitakiwa kujua kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliompa Dr Rashid jeuri hadi akaacha kununua mitambo ya maani ili tuingie gizani. Kwa hiyo wote wako kundi moja na mafisadi wengine ambao ni "enemies of the people" katika hili na hatakiwi hata kusema kitu! Ila kwa kiburi chake utasikia atakayoyasema kesho!
   
 16. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  utani wa wazaramo na kina masatu lazima afe mtu
   
 17. m

  matambo JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  kma ni kweli ulipost thred y kumtukan mhe.zito nkupongeza kwa uungwana wako wako wa kumuomba radhi kupitia jukwaa hilihili ulilomtumia,
  nchi yetu hivi sasa ipo taabuni shauri ya wajinga wachache wasioona mbali ni kweli yawezekana mitambo ile ni ya kifisadi lakini by that time we had no option lakini watu wakaona labda kama vile kuna watu fulani watamake kwelikweli,huo haukuwa uamuzi mzuri,
  inafsi ni mfuatiliaji mzyri wa television series ya kimarekani ya 24,kuna seasons zingine mfano season 3 au season 7 jack bauer analazimika kufanya mahusiano na magaidi just ili apate anachokitaka na kwa kwetu tulichokitaka ni nchi kuwa kwenye umeme ili shughuli za uzalishaji mali zisisimamae,leo hii nani anaweza kutueleza ni mamiliono mngapi yanapotea kutokana na viwanda au ofisi mbalimbali kuwa hazifanyi kazi?au ghrarama ambazo zinakuwa incurred kwa ajili ya majenereta?
  BANIANI MBAYA LAKINI KIATU CHAKE DAWA
   
 18. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Huu wote ni ukosefu wa principles tu, hamna geni!

  Tuwafungulie kutoka jela walawiti, wauaji, majambazi, n.k. kwa vile nchi yetu haina pesa za kutosha?!!

  Watu wengine mnaonekana mko tayari kulala (kimapenzi) na wazazi wenu eti kwa vile tu jambazi limewashikia mtutu kichwani!! Let's suffer na vibatari vyetu, lakini Dowans na nduguye Richmond nasema NO!!!
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu, yaani sina la kuongeza... Nafikiri, Tanzania we need Jesus! ni wakati wa ukombozi wa kiroho!
   
 20. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Masatu unamuomba msamaha Zitto kwa sababu zipi endelevu?Mkuu Masatu barua yako hii haina hoja za msingi,ukiachilia kilio chako cha kuomba msamaha kwa watu ambao wapo tayari kuona katiba inavunjwa kwa maslahi yao na wenzao wachache!

  Kwanza,Katiba ya TZ inakataza kabisa kwa serikali kununua mitambo chakavu,na Zitto kabwe alisimama kidete kupigania ivunjwe katiba ili mitambo hiyo chakavu ya DOWANS inunuliwe,ina maana Masatu unamuomba masamaha mtu aliyetaka hadi katiba ivunjwe?

  Pili,TANESCO haiwezi kushauriwa na kamati ya akina Zitto njia mbadala ya kupata umeme wa uhakika mbali na hii mitambo ya DOWANS?Je kama tungenunua mitambo ya DOWANS ndiyo ingekuwa suluhisho la kudumu la umeme kwa waTZ?unamuomba msamaha mtu aliyeshindwa kuishauri vyema serikali baada ya kukataa wazo lake la kununua mitambo yenye mgogoro ya DOWANS?

  Masatu your too low for this kaka,na ingawaje Zitto alifanya kazi kubwa sana kuibua baadhi ya ufisadi hapa TZ lkn kwa hili alichemsha na katu nasisitiza tena siwezi muomba msamaha na naamini alikosea!
   
Loading...