Mkuu pengine sijasoma post zako zote, ushauri wako ni nini katika wakati kama huu? we all know long term strategies, na zimesemwa tangu JK akiwa huko huko, tukarogwa akapewa urais.
Kuhusu Tanesco tunajua hamna kitu pale, unaweza ukamchukua mtoto wa darasa la nne akaongoza Tanesco.
However, Poor innocent people are dying out there what is the solution NOW!
Your contribution on this matter at hand will be greatly appreciated
Mkuu kwa haraka sana unanikumbusha mshikaji wangu mmoja ambaye tulimkanya kutotembea na msichana jina kapuni ambaye alisadikika ni mgonjwa wa Ukimwi. Majibu yake yalikuwa mazito sana na yenye kuumiza mara tatu.. alibwabwaja kama vile tumemshika mkono..
'Ohhh! kwani nyie mna hakika gani kama mimi ni mzima?.. hata hivyo mnataka niwakanyage nyie au?..Wanaume wazima badala ya kuja na ushauri wa maana mnaanza kusema watu wengine wakati afya zenu wenyewe matatani..Mwenye kiu mimi, mwenye kupenda mimi nyie yanawahusu kitu gani kwani Ukimwi nini sii ugonjwa tu kama maradhi mengine!..Sote tutakufa khakuna atakaye ishi milele..Kama ni cost za mazishi nikifa acheni nife nitazikwa na city!'
Tukifikia hapa mkuu wangu nadhani ipo haja yetu sisi kukaa pembeni na kuitazama picha nzima ya Dowans!..
Hata hivyo nitamalizia kwa kukukumbusha vitu vichache sana! ni kweli mwenye kusikia uchungu wa maumivu leo hii ni wewe uliyepo on the ground, lakini kumbuka tu haya yafuatayo..
Wananchi tulipokea hotuba ya waziri Ngereja tarahe 11 December mwaka 2008 pia hotuba ya Mh. rais wetu Jakaya Kikwete ktk kuufunga mwaka 2008 ambao wote walitamka kwamba seriikali haitanunua mitambo ya Dowans hivyo wanajiandaa na ununuzi wa mitambo mipya iki ni pamoja na kuboresha mabwawa yetu ili yaweze kuzalisha umeme wa ziada (short term strategy)..
Hawa ni viongozi wa juu ktk utawala wetu na wasemapo hawa sidhani kama kuna hoja tena au mjadala wa Tanesco au Dowans...na bila shaka walifikia maamuzi hayo kwa kushauriwa na wataalam maanake yaonyesha watu mnafikiria tu kwamba Dr. Idrisa ndiye mwenye wataalam..Wakatuondoa wasiwasi uliofuatia maneno ya Idrisa kwamba taifa litakapo ingia kizani tusimlaumu yeye.
Kufuatia maneno hayo, Mzee Mwanakijiji kama nakumbuka vizuri alimshauri rais wetu JK kuwasimamisha kazi Dr.Rashid na waziri Ngereja mara moja kwa sababu hawa ndio walikuwa kiini cha mchezo huo mchafu wa vitisho kwa wananchi wakati nafasi ya kufanya ufumbuzi ipo na ilikuwepo kwa muda..Hata hivyo, matokeo yake Serikali haikufanya kitu!
Hivyo basi Ushauri wetu wakati tupo kizani, ni kuwa huu ndio wakati wetu sote Watanzania kuonyesha kutoridhika na Utawala uliopo. Kutoridhika na mikakati mibovu ambayo inaturudisha nyuma kimaendeleo badala ya kulalama na mitambo ya Dowans ambayo haiwezi kuondoa tatizo la Umeme nchi ila ni kipozeo cha upungufu uliotokea.
Nitarudia kusema mtambo wa Dowans ni Kibatari ambacho hatukihitaji.. kwa afya ya uchumi wetu na usiri uliojengeka nyuma ya mitambo hiyo ni sawa na taifa zima tumekubali kupokea Rushwa, kinyume cha kiapo cha imani ya kila Mtanzania. Mkuu wakati Dar mnaingia katika mgao wa Umeme kuna wilaya na vijiji huko bara vimeanza kupata umeme kwa mara ya kwanza huo umeme unatoka wapi?.
Aidha, rais Kikwete a step down kwa sababu kashindwa kutimiza ahadi yake kwa wananchi (rejea hotuba yake ya kufunga mwaka 2008, au Dr. Rashid na Ngereja wachukuliwe hatua kali na mipango mipya na yenye uhakika inafuatwa.
Leo tutanunua mitambo ya Dowans na itakuja haribika kama mitambo mingine ambayo hadi leo hii imesimama haifanyi kazi..ni mchezo ule ule wa TRA kuwa na vichwa ambavyo vimesimama na vinatakiwa ukarabati lakini serikali imeshindwa kuwawezesha engineer wetu.
Je, unafahamu kwamba leo hii kwa zaidi ya miaka 20 tunazalisha umeme chini ya kiwango au uwezo wa mitambo tuliyokuwa nayo kwa asilimia 40 au zaidi?.. Tutaendeshaje uchumi wa nchi ikiwa sehemu kubwa ya nguvu za Umeme wetu haifanyi kazi leo tunakuja tegemea Dowans kuwa mkombozi..