Kumpiga mkeo sio poa kabisa

Kumpiga mkeo sio poa kabisa

Bado hujasema hujawajua wanawake bado niulize mimi niliyebahatikaga kuishi na mmakonde fulani mwenye kaasili cha umwera..mdomondomo na matusi ndo maana nakwambia oa utasema
Ukiachana na madhila ya huyo! Tupe uzoefu wa kuzichakata pisi za huko, yanayosemwa ni kweli kwamba ni mafundi sana kunako
 
Namaanisha kumpiga mkeo mangumi ama kipigo kama cha mbwa mwizi ama paka shume sio poa kabisa

Huwa ninasoma mabandko mengi hapa ambapo baadhi ya wanaume hujitapa jinsi walivyowatwanga wake zao na kuwatusi, na leo nina ujumbe kwa wote wenye tabia ya kupiga wake zao.

Ndugu yangu mpendwa, tumia mikono yako kumkumbatia, kumbembeleza na kumkanda mkeo.

Mungu alikupa misuli ya kuweza kumpelekea moto mkeo mkiwa faragha, kumwinua na kumlinda mkeo na hatari zote. Mkeo anapaswa kujisikia salama na salama zaidi mikononi mwako.

Rafiki yangu mpendwa, tumia ulimi wako kumbusu na kumbariki mkeo.

Ikiwa una matatizo huko kazini kwako Usimwagie hasira zako kwa mkeo, hata ukiwa na matatizo ya kifedha usipeleke hasira zako kwa mkeo.

Maneno ya kinywa chako yanapaswa kujaa sifa, pongezi na kutia moyo.

Ni woga ndio unaomfanya mtu kumpiga mkewe. Kwa kawaida waoga hujificha nyuma ya vurugu ili kuepuka uwajibikaji.

Jifanye kuwa bora kuliko kuwa muoga .

Kamata hii..... "mke mzuri ndiye anayekusaidia kukua na kuimarika kimwili (kiakili) na kiroho". Hivyo jionyeshe kuwa umekua na una akili kwa kutatua maswala yote kwa uangalifu.

Ubarikiwe
Hakuna kupigana ni twa twa twaaatwaaa. Mchezo umeisha
 
Hoja yako ni kumpiga mwanamke au kumpiga kipigo Cha mbwa koko maana sijawai ona mwanaume anayejisifia humu kumpiga mkewe kipigo Cha mbwa koko ila Kama kumpiga tu nina wasiwasi na uwezo wako wa kifikra...Mosi.

Pili, ukiona mtu kapigwa maanayake Kuna contractions zisizoweza vumilika zimetokea mfano dharau za Hali ya juu sasa wewe badala ulete solution au alternative inayoeleweka badala yake unasema sijui umbusu, ukandekande na kumpetipeti yaani mkeo kaktukana then mpetipeti



Tena wengine hadi kumpiga makofi mume wake, Je hapo napo Mwanaume uendelee kubembeleza mkeo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom