Kumpiga mkeo sio poa kabisa

Kambi ya Fisi

JF-Expert Member
Feb 3, 2018
13,525
22,019
Namaanisha kumpiga mkeo mangumi ama kipigo kama cha mbwa mwizi ama paka shume sio poa kabisa

Huwa ninasoma mabandko mengi hapa ambapo baadhi ya wanaume hujitapa jinsi walivyowatwanga wake zao na kuwatusi, na leo nina ujumbe kwa wote wenye tabia ya kupiga wake zao.

Ndugu yangu mpendwa, tumia mikono yako kumkumbatia, kumbembeleza na kumkanda mkeo.

Mungu alikupa misuli ya kuweza kumpelekea moto mkeo mkiwa faragha, kumwinua na kumlinda mkeo na hatari zote. Mkeo anapaswa kujisikia salama na salama zaidi mikononi mwako.

Rafiki yangu mpendwa, tumia ulimi wako kumbusu na kumbariki mkeo.

Ikiwa una matatizo huko kazini kwako Usimwagie hasira zako kwa mkeo, hata ukiwa na matatizo ya kifedha usipeleke hasira zako kwa mkeo.

Maneno ya kinywa chako yanapaswa kujaa sifa, pongezi na kutia moyo.

Ni woga ndio unaomfanya mtu kumpiga mkewe. Kwa kawaida waoga hujificha nyuma ya vurugu ili kuepuka uwajibikaji.

Jifanye kuwa bora kuliko kuwa muoga .

Kamata hii..... "mke mzuri ndiye anayekusaidia kukua na kuimarika kimwili (kiakili) na kiroho". Hivyo jionyeshe kuwa umekua na una akili kwa kutatua maswala yote kwa uangalifu.

Ubarikiwe
 
Ndoa ni photocopy jinsi wazazi walivyoishi.Mtoto kama alishuhudia mama yake akipigwa bezwa mbele yake nae atahitaji Mwanaume type ya baba yake.
Akimpata muungwana na mstaarabu atamchokoa hadi apigwe ili ajaze Lile gap la hisia lililochwa na makovu ya yake aliyokuwa alishuhudia mama yake akipigwa
 
Mfano wanawake wa mkoa wa... wanapenda Mwanaume mpigaji ndio uamini ni uanaume.
Ukiwa mvulana haishauriwi kuoa huko utanyanyasika sana,wengi wao ni wababe ni madikteta kwa waume zao,Sasa waume zao uwanyoosha kwa kipigo.
Wao utii huja kwa kipigo.
Ni ishu ya spirit ni kitu Cha asili
 
Ndoa ni photocopy jinsi wazazi walivyoishi.Mtoto kama alishuhudia mama yake akipigwa bezwa mbele yake nae atahitaji Mwanaume type ya baba yake.
Akimpata muungwana na mstaarabu atamchokoa hadi apigwe ili ajaze Lile gap la hisia lililochwa na makovu ya yake aliyokuwa alishuhudia mama yake akipigwa
Sidhani kama kuna ukweli kwa hili
 
Namaanisha kumpiga mkeo mangumi ama kipigo kama cha mbwa mwizi ama paka shume sio poa kabisa

Huwa ninasoma mabandko mengi hapa ambapo baadhi ya wanaume hujitapa jinsi walivyowatwanga wake zao na kuwatus

Ubarikiwe
Ni kweli wanaume wasio jiamini ndio wanapiga wake zao na kuwatukana matusi ya nguoni, lakin wakumbuke kuwa hao ni binadam sio wanyama kuna njia nyingi za kutatua migogora hata kawa ameekuudhi lakini sio kupiga huko ni kukosa hekima.
 
Hoja yako ni kumpiga mwanamke au kumpiga kipigo Cha mbwa koko maana sijawai ona mwanaume anayejisifia humu kumpiga mkewe kipigo Cha mbwa koko ila Kama kumpiga tu nina wasiwasi na uwezo wako wa kifikra...Mosi.

Pili, ukiona mtu kapigwa maanayake Kuna contractions zisizoweza vumilika zimetokea mfano dharau za Hali ya juu sasa wewe badala ulete solution au alternative inayoeleweka badala yake unasema sijui umbusu, ukandekande na kumpetipeti yaani mkeo kaktukana then mpetipeti
 
Back
Top Bottom