Kumiliki simu ya TECNO kuna raha zake bwana!

Kumiliki simu ya TECNO kuna raha zake bwana!

Kiukweli haya mambo nayasomaga tu, nina mwaka wa NNE naumia h6 na sijawahi pata hizo shida
H6 ndio revolution ya smartphone za tecno, sijawah penda tecno ila hii naweza isifia, camera yake ilikua natural na high quality, specs zake nying zilikua real achana na haya mafamba ya skuhz,
 
waz

Wazee wa kuweka launchers za ku-download huwa mnajulikana kirahisi sana.

😎😎
Mzee mzee... ulitaka nisiwe nayo ili upate faida gani .....
Screenshot_20181021-074214.png
 
Mimi ninachoipendea haijawahi kugoma kuingiza salio za Tigo pesa au kumtumia mtu salio kwa bahati mbaya. Raha ya simu salio sio unajisifu una iPhone kuingia JF bando la bure mnaita free nini sijui!
Freebasics
 
- Mara una type message characters zinajiongeza zenyewe!

- Unaongea mtu, ukikata simu haikati mpaka ung'oe betrii!

- Unafungua screen, inagoma kufunguka hadi uzime uwashe!

- Unasave namba ya mtu, siku unakuta mara imepotea.

- Muziki wake utadhani una suboufer!

- Mafundi wake na spare zake vimejaa kedekede kila kona!

- Zinatuunganisha haswa, kila unayekutana nae anayo!

Hongera TECNO.
huo ni UMAMA kujifanya unadharau tecno mtanzania umaskini umekujaa mpaka wap sijui...
kamtindo ka kudharau tecno wakati ndo katu transform 90% ya waafrica hasa east africa kutoka gizani mpaka hapa tulipo na kuzijua samsung...
hata kama situmii tecno lakin mtu akiidharau huwa namuona limbukeni sana..
 
E mail nasoma, natuma ,document zangu naandaa vizuri nikiamua kuprint na print, camera ipo vizuri picha napiga, nikiwa na uhitaji wa documentary au habari yoyote you tube naingia, vizuri, nikiamua kupitia mitandao ya kijamii sipati tatizo kwanini sasa nikomae kununua simu ya laki name au saba wakati ipo simu ya laki tatu inaweza kufanya yote hayo tena kwa ufanisi,

Vijana ngojeni mmalize masomo ndio mtajua kumbe TEKNO na iPhone zote simu tofauti majina, ukiwa unakula bure unalala bure huwezi kujua thamani ya pesa kitu cha million moja utaona kawaida tu kuwanacho sababu pesa yako haina uhitaji, mkikua mtaacha huu ubishi was kitoto
 
Nilikutana na Demu flani kwa Hiace nikamuomba simu nijibip ili nipate no. Yake akakubali nashangaa mbona simu haiiti wala kusema haipatikani coz niliicha gheto, ila nikajipa moyo kuwa itafika ni mtandao tu, daadeki nafika geto ninafuraha nikijua nitakuta missed call nakuta simu iko fait Mode. Shenz sana hii tecno
 
Back
Top Bottom