Kuna namna mbili za kumsaidia mtu
Mpe msaada wa mahitaji yake kila siku kama vile mlemavu, siku ukiondoka na yeye arudi kwenye hali yake ya shida
Au muwezeshe kwa mbinu kusudi ajitegemee kwa muda mrefu ata usipokuwepo bado atazimudu changamoto
Magufuli ataiongoza Tanzania kwa miaka kumi, hata kama mtu alikuwa si shabiki wa ndege zipo na zishanunuliwa busara ni kuona wanapata faida, same applies to TTCL anayotaka kuiewezesha na yenyewe aliikuta na ataondoka ataicha.
Raisi anaweza fanya anavyoweza kwa jitihada zake kuyasaidia mashirika ya umma lakini kama yenyewe hayana mbinu za biashara akitoka hali yao itarudi kuwa vile vile.
Kama watanzania tunataka kuona haya mashirika yanapata faida na wanakuwa washindani sokoni bila ya Magu ni lazima wawe wabunifu kama washidani wao walivyo.
Wenzao wanaelewa mafanikio kwenye soko la ushindani ni kujua gap ilipo ya wateja, kuelewa consumer expectations kwenye huduma zao, kuzindua huduma kutokana na ushahidi, kushindana kwa value na wengine na kutoa huduma yenye kiwango.
Ngoja nikupe mfano miaka mitatu/minne nyuma kupitia humu humu JF Halotel ilivyofunguliwa walikuja na clever entry strategy na ilikuwa kila ukifungua kule jukwaa la habari kuna thread halotel mkombozi sijui bei zake nafuu, hatolel sijui package fulani ni bora kushinda Voda in short habari ya mjini ilikuwa Halotel. Aikuchukua muda thread zikaanza kubadilika hawa Halotel wameanza kuwa wezi etc with malalamiko ya watanzania.
Plan hapo ilikuwa ni kuvutia wateja kwanza walipopata wa kutosha taratibu wakawarudisha kwenye uhalisia wa gharama za kuzalisha huduma na kuanza kutoza kwa bei za uhalisia kwa kuzingatia value competition leo wanawateja 10 million wakati TTCL ina laki tano.
Point yangu ni kwamba haya mashirika ya serikari hawana jitihada za kupata wateja na awajali kuona washindani wao wanafanya nini kusudi watengeneze competitive edge sokoni.
Matokeo yake results zao ni mbovu wote, sasa awawezi endelea na kuwa watoa gawio wazuri mbeleni kwa kupewa kila kitu. Magu akitoka na wao wanarudi kule kule ni bora kuwapa ukweli kama tunataka kuona wanakuwa na sustainable businesses sio kuendelea kuona wanalelewa vibaya na mlezi aliepo wanakuwa kama spoilt brats who cant fend for themselves wote iwe Posta, TTCL, ATCL, TANAPA. Airport Authorities, Bandari etc wote ni below the capacity of their potential na hawana pressure kwa sababu sisi wenyewe atutoi kasoro zao.