Kumekucha TTCL wateja sasa bwerere!

Kumekucha TTCL wateja sasa bwerere!

Wote.Serikali haiwezi kukupa ajira halafu uwe kinyume nayo,ni wajibu wako kum-support mwajiri wako.
Hayo yote ni kazi bure, Umeme, maji, barabara vyote hivo tunasapoti mwajiri bila shuruti vp kuna jipya au la ajabu.
 
Ni hatari sana.
Kuweka mikakati ya kufufua kampuni moja linalopewa mtaji na serikali na kuua makampuni zaidi ya matano yenye mitaji yao ni jambo la ajabu kabisa.

Watanzania hawajawahi kulalamika kuwa wanakosa mtandao wa kujiunga nao.
Kwa nini tunatumia kodi za wananchi kuhangaika na huduma ambazo zipo za kumwaga na kulazimisha kuziua badala ya kuziimarisha ili tupate kodi.

Watanzania tunaibiwa na kidhulumiwa sana na mifumo ya watawala mana Mfanyakazi anakatwa kodi.
Kodi hiyo inaenda kuanzisha kampuni kama TTCL halafu mfanyakazi huyo huyo aliyelipa kodi anakatwa tena kodi kwenye vocha anayonunua kwenye kampuni aliyoipa mtaji.
Ni unyonyaji mkubwa sana wa serikali kwa wananchi wanyonge wenye vipato vidogo kwa lengo la kuwaneemesha miungu watu wanaotawala.

Bila tulitegemea nchi iwe na makampuni makubwa yasiyopungua 50,000. Makampuni makubwa ndiyo yanayoweza kubusti Uchumi wa nchi mana nchi ina maskini wengi sana ambao hawana uwezo wa kutumia pesa kwenye mahitaji ya ziada ili wakuze soko. Na nje ya nchi hatuweze kabisa kushindana kama mbinu yenyewe ni hiyo ya vitisho na kuuana kwa kutishiwa njaa ili watu wajiunge.
Hatari sana.
Tumekosea sana na tutakosea zaidi kuipa CCM nguvu kubwa ya wabunge ambao hawana tija kwa taifa zaidi ya maslahi yao.
 
Usichanganye mambo ya biashara na ajira.
TTCL ni biashara, mtu ana uhuru wa kuwa mteja wako au la. Ujinga huu uliwahi kuibeba NMB.

Ajira ina sheria, haki na wajibu wake kwa mwajiri na mwajiriwa.

Mkataba unamtaka mwajiri kuongeza mshahara kila mwaka mpya wa fedha. Hili sio ombi wala hisani, ni sheria. Lkn kwa sababu nchi hii ni mazwazwa, hatuwezi kuhoji.

Kwa hiyo, mtumishi wa umma ana haki ya kuchagua mtandao anaoupenda.

Nilitaka kununua line ya TTCL lkn kwa ubabe huu sinunui nione mwajiri atanifanyaje.
Hawa wafanyikazi mufilisi kabisa,kwanza kama wangekuwa wanajitambua kusingekuwa na haja hata ya kulazimishwa.Hii inaonyesha wazi kwamba in one way or the other they are aganst the government.Uko kinyume na serikali halafu bila aibu unaomba nyongeza ya mshahara!Aibu sana.
 
Usipotumia miezi 3 hadi 6...
Yaani hawana database yakujua watu wenye laini au la.Mimi ninachojua makampuni yana database ya majina au wenye namba za simu na usipotumia kwa muda wa mwaka mmoja wanampa mtu mwingine sasa TTCL wanataka majina ya nini sasa ai
 
Safi sana Siasa ya ujamaa na kujitegemea!
Ni hatari sana.
Kuweka mikakati ya kufufua kampuni moja linalopewa mtaji na serikali na kuua makampuni zaidi ya matano yenye mitaji yao ni jambo la ajabu kabisa.

Watanzania hawajawahi kulalamika kuwa wanakosa mtandao wa kujiunga nao.
Kwa nini tunatumia kodi za wananchi kuhangaika na huduma ambazo zipo za kumwaga na kulazimisha kuziua badala ya kuziimarisha ili tupate kodi.

Watanzania tunaibiwa na kidhulumiwa sana na mifumo ya watawala mana Mfanyakazi anakatwa kodi.
Kodi hiyo inaenda kuanzisha kampuni kama TTCL halafu mfanyakazi huyo huyo aliyelipa kodi anakatwa tena kodi kwenye vocha anayonunua kwenye kampuni aliyoipa mtaji.
Ni unyonyaji mkubwa sana wa serikali kwa wananchi wanyonge wenye vipato vidogo kwa lengo la kuwaneemesha miungu watu wanaotawala.

Bila tulitegemea nchi iwe na makampuni makubwa yasiyopungua 50,000. Makampuni makubwa ndiyo yanayoweza kubusti Uchumi wa nchi mana nchi ina maskini wengi sana ambao hawana uwezo wa kutumia pesa kwenye mahitaji ya ziada ili wakuze soko. Na nje ya nchi hatuweze kabisa kushindana kama mbinu yenyewe ni hiyo ya vitisho na kuuana kwa kutishiwa njaa ili watu wajiunge.
Hatari sana.
Tumekosea sana na tutakosea zaidi kuipa CCM nguvu kubwa ya wabunge ambao hawana tija kwa taifa zaidi ya maslahi yao.

Biashara za kujufunzia ukubwani, sekta binafsi ndio injini ya uchumi
 
Punda utampeleka mtoni, je utamlazimisha kunywa maji. Hawa wafanyakazi watanunua hizo line, jee watalazimishwa kuzitumia kwa mawasiliano yao binafsi?
 
Ok TTCL hapo wana changamoto ya kuhakikisha vocha zao zinapatikana Hadi kwa shemeji yangu nyasa vijijini waliko mabwana shamba na mabibi shamba na watendaji wa vijiji na kata na walimu wa shule za msingi za porini waajiriwa wa serikali.Vocha za TTCL Ni changamoto.
Tumia TTCL PESA kuongeza salio!
 
Mawakala wa TPesa vijijini na wilayani mikoani unajua waliko au wewe uko dar es salaam na siyo dar nje ya jiji? Nje ya Jiji la dar ulishawahi waona hao mawakala wa TPesa sura zao wanafananaje? Unakaa ofisini ulishatoka nje ya Jiji ukaona hao TPesa wakala?
Kila ofisi ya Wilaya ya TTCL kuna Wakala, TTCL Pesa ni wapya coverage yao siyo kubwa, nakukumbusha "mbuyu ulianza kama mchicha".
 
Watanzania wenye simu za mkononi wanafikia 43,621,000 na kati ya hao TTCL ina subscribers 711,411 (1.6%). Serikali ina jumla ya wfanyakazi 800,000. Hata kama wote hawa waki-subscribe kwa TTCL watafikia 1,511,411 (3.4%). TTCL isitegemee itatoboa kwa kubebwa bebwa. Badala yake iandae marketing strategy itakayowawezesha kuongeza market share ili angalau ifikie 20% ndani ya miaka 3 ijayo.
Kwa nini Mfanyakazi wa TiGo kuwa na line ya tiGo, Vodacom kuwa na laini ya Vodacom, AirTel kuwa na line ya Airtele , Zantel kuwa na line ya Zantel (mwajiri) , nk siyo issue, ila Mfanya kazi wa Serikali kuwa na line ya mwajiri (Shirika la Mawasiliano la Taifa (TTCL) inaonekana ni issue?! Naomba kujua.
 
Wenzao wanatafuta wateja kwa mikakati wao wanasubiri serikari halafu kumbe wanakomalia issue pembeni, watetezi wa huu uzembe watakwambia hawana network za kufikia wateja.

Maajabu wakiletewa wateja bure huko mikoani mara tu network zao zinawafikia watu hao hao ambao walishindwa kuwapata kwa marketing ploys.

Only possible kwenye mashirika ya serikari ya Tanzania
 
Hawa wafanyikazi mufilisi kabisa,kwanza kama wangekuwa wanajitambua kusingekuwa na haja hata ya kulazimishwa.Hii inaonyesha wazi kwamba in one way or the other they are aganst the government.Uko kinyume na serikali halafu bila aibu unaomba nyongeza ya mshahara!Aibu sana.
Aisee, leo mbona uko chini hivi?
Mfanya kazi awe wa serikali au la, anapeleka pesa yake palipo na huduma nzuri. Zungumzia TTCL watoe huduma nzuri badala ya kukazia mfanya kazi apeleke uteja wake huko hata kama huduma ni mbovu.
 
Mbona kama umeyumba mkuu tatzo si vocha je network ipo credit unapata kupitia njia mbadala
Ok TTCL hapo wana changamoto ya kuhakikisha vocha zao zinapatikana Hadi kwa shemeji yangu nyasa vijijini waliko mabwana shamba na mabibi shamba na watendaji wa vijiji na kata na walimu wa shule za msingi za porini waajiriwa wa serikali.Vocha za TTCL Ni changamoto.
 
Kwa nini Mfanyakazi wa TiGo kuwa na line ya tiGo, Vodacom kuwa na laini ya Vodacom, AirTel kuwa na line ya Airtele , Zantel kuwa na line ya Zantel (mwajiri) , nk siyo issue, ila Mfanya kazi wa Serikali kuwa na line ya mwajiri (Shirika la Mawasiliano la Taifa (TTCL) inaonekana ni issue?! Naomba kujua.
Kwa sababu TTCL siyo mwajiri wa watumishi wa serikali!
 
Back
Top Bottom