Kumekucha TTCL wateja sasa bwerere!

Kumekucha TTCL wateja sasa bwerere!

Kwani nyongeza ya mshahara hutolewa kama matokeo ya kuiunga serikali mkono au hutolewa kama matokeo ya kazi unayoifanya pamoja na kupanda kwa gharama za maisha?!
Nyongeza ya mshahara au kupandishwa cheo sio automatic,inategemea utendaji wako wa kazi na vigezo vingine kama mwajiri wako atakavyo ona fit.Let us be serious,mtumishi huko tayari kum-support mwajiri wako kwenye endevours zake za kuwaendeleza wananchi including yourself,endevour ambayo itamsaidia kupata fedha za kukulipa hata mshahara!Jamani bado unategemea mwajiri huyo huyo akuongezee mshahara?!Kama unataka mwajiri wako awe nawe,be with him in times of need.
 
Ok mishahara na marupurupu iongezwe SI sahihi kupandisha cost za simu za kazi anazotumia mwajiriwa at the expense ya mfanyakazi.Uzalendo Ni two way traffic not one way.Huu mzigo wa charges za mwajiriwa kuwa na simu mbili ya Tigo pesa au Mpesa ili atumie kununua vocha za TTCL waajiri waubebe au TTCL ibebe vinginevyo TTCL ijipange ifikishe vocha kila Kona ya nchi na hizo huduma zake za TTCL pesa.Wasikwepe majukumu na kusukumizia waajiriwa wakatafute line za tigo pesa au mpesa ili waihudumie TTCL kwa charges at the expense of employee.No.
Hivi unsjua kwamba TTCL iki-perform vizuri itatoa gawio kubwa serikalini,gawio ambalo litasaidia kukulipa hata wewe mshahara?Usione kama TTCL ni kitu cha mbaali,no it is so close to you.
 
Aisee, leo mbona uko chini hivi?
Mfanya kazi awe wa serikali au la, anapeleka pesa yake palipo na huduma nzuri. Zungumzia TTCL watoe huduma nzuri badala ya kukazia mfanya kazi apeleke uteja wake huko hata kama huduma ni mbovu.
Wewe ni sehemu ya TTCL,usijione kama uko mbali sana na TTCL.Kumbuka kwamba ukii-support TTCL unaisaidia serikali kupata fedha kupitia gawio,na hivyo indirectly unaisaidia serikali kukulipa wewe mshahara.Usione kama TTCL iko mbali sana na wewe no.Jitafakari.
 
Kwa sababu TTCL siyo mwajiri wa watumishi wa serikali!
Mkuu Ileje, heshima kwako.
Naona unapanua goli badala ya kujibu hoja.
Binafsi ningependa kufahamu.
Suala Wafanyakazi wa TiGo wana line za tiGo, Wafanyakazi wa Vodacom wana laini za Vodacom, wafanya kazi wa AirTel kuwa na line za Airtelel , wafanyakazi wa Zantel wana line ya Zantel, wafanyakzai wa halotel nk wote wana line ambazo sina nasaba na mwajiri wao wala jamii haioni kama hilo ni tatizo. Namanisha hata mashirika yasiyo ya mawasiliano wanazo Kampuni rafiki za mawasiliano ambazo wanazitumia kwahuduma hizo ikiwemo CUG. Je kwa nini mfanyakazi wa Serikali kuwa na line zenye nasaba na mwajiri (Shirika la Mawasiliano la Taifa (TTCL) inaonekana ni tatizo?!?! Naomba kujua.
 
Usichanganye mambo ya biashara na ajira.
TTCL ni biashara, mtu ana uhuru wa kuwa mteja wako au la. Ujinga huu uliwahi kuibeba NMB.

Ajira ina sheria, haki na wajibu wake kwa mwajiri na mwajiriwa.

Mkataba unamtaka mwajiri kuongeza mshahara kila mwaka mpya wa fedha. Hili sio ombi wala hisani, ni sheria. Lkn kwa sababu nchi hii ni mazwazwa, hatuwezi kuhoji.

Kwa hiyo, mtumishi wa umma ana haki ya kuchagua mtandao anaoupenda.

Nilitaka kununua line ya TTCL lkn kwa ubabe huu sinunui nione mwajiri atanifanyaje.
Nilitegemea mfanyakazi aone mbali kwa kuwa ana elimu,kumbe elimu haijasaidia.Hivi unaona kwamba TTCL ni biashara per se,no.Kumbuka kwamba TTCL iki-perform vizuri through your support,itatoa gawio kubwa zaidi na hivyo utaiwezesha kukulipa wewe mshahara.Funguka kijana.
 
Mkuu Ileje, heshima kwako.
Naona unapanua goli badala ya kujibu hoja.
Binafsi ningependa kufahamu.
Suala Wafanyakazi wa TiGo wana line za tiGo, Wafanyakazi wa Vodacom wana laini za Vodacom, wafanya kazi wa AirTel kuwa na line za Airtelel , wafanyakazi wa Zantel wana line ya Zantel, wafanyakzai wa halotel nk wote wana line ambazo sina nasaba na mwajiri wao wala jamii haioni kama hilo ni tatizo. Namanisha hata mashirika yasiyo ya mawasiliano wanazo Kampuni rafiki za mawasiliano ambazo wanazitumia kwahuduma hizo ikiwemo CUG. Je kwa nini mfanyakazi wa Serikali kuwa na line zenye nasaba na mwajiri (Shirika la Mawasiliano la Taifa (TTCL) inaonekana ni tatizo?!?! Naomba kujua.
Mawasilino katika ofisi za serikali hafanyika kwa simu za mezani ambazo ni za TTCL! Hivyo kwa mawasilino yote ya kiofisi wafanyakazi wa serikali wanatumia TTCL ambalo ni shirika la serikali!

Kwa mawasilino binafsi mtumishi anatumia mtandao alionao na ambao ni nafuu kwake na hauna shida ya network!
 
Wewe ni sehemu ya TTCL,usijione kama uko mbali sana na TTCL.Kumbuka kwamba ukii-support TTCL unaisaidia serikali kupata fedha kupitia gawio,na hivyo indirectly unaisaidia serikali kukulipa wewe mshahara.Usione kama TTCL iko mbali sana na wewe no.Jitafakari.
Ninakubaliana sana na wewe katika ulichoandika isipokuwa hayo maneno uliyoweka mwisho "

unaisaidia serikali kukulipa wewe mshahara.Usione kama TTCL iko mbali sana na wewe no.Jitafakari.
Sio wajibu wangu ku'support' kama huduma ni mbovu.
 
Ninakubaliana sana na wewe katika ulichoandika isipokuwa hayo maneno uliyoweka mwisho "

Sio wajibu wangu ku'support' kama huduma ni mbovu.
Wewe ni mmoja wa wale ambao unaweza kuchangia huduma ya TTCL ikawa nzuri,kama utajitambua.P'se come onboard.
 
Namanisha hata mashirika yasiyo ya mawasiliano wanazo Kampuni rafiki za mawasiliano ambazo wanazitumia kwahuduma hizo ikiwemo CUG. Je kwa nini mfanyakazi wa Serikali kuwa na line zenye nasaba na mwajiri (Shirika la Mawasiliano la Taifa (TTCL) inaonekana ni tatizo?!?! Naomba kujua.
Umeandika "Kampuni rafiki za mawasiliano ambazo wanazitumia"..., lakini hujasema 'wanalazimishwa wazitumie'. Maana yake hapa ni kwamba wanao utashi wa kuzitumia au la. Hii ina maana kubwa ukiifikiria na ni tofauti na matakwa ya kujiunga kwa lazima kwa mtu binafsi; hata awe mwajiriwa wa serikali. Ndio, ni jambo jema linalotakiwa kufanywa na wananchi wote kuyaunga mkono mashirika yetu. Kitu mhimu hapa ni kuweka mkazo mashirika haya yafanye kazi kwa ufanisi. Yakifanya hivyo, hakuna atakayetaka kulazimishwa kujiunga nayo.

Tutakapotoka kwa wafanyakazi serikalini, mwisho wetu utakuwa wapi? Raia wote ambao ni waTanzania lazima wajiunge na mtandao huo? Kwa maana wanaotoa amri hizi ndio serikali, na ni serikali ya raia wote.
 
Awamu ya tano ni mfano wa kuigwa barani africa,jamaa ana akili sana kwa kweli,haitakaa itokee
 
Waje Tu,Hii mitandao ya sasa imekuwa majambazi,inatuibia mchana kweupeee! labda inaweza kuwa nafuu sasa...
 
mtumishi wa umma asietumia line ya TTCL afukuzwe kazi, serikali haiwezi kukupa mshahara mtumishi wa umma, halafu unaenda kununua vocha ya tigo au vodacon, huko ni kukosa uzalendo!
 
Nimesema "kama utajitambua,"usichukue neno moja out of context.
Kuna namna mbili za kumsaidia mtu

Mpe msaada wa mahitaji yake kila siku kama vile mlemavu, siku ukiondoka na yeye arudi kwenye hali yake ya shida

Au muwezeshe kwa mbinu kusudi ajitegemee kwa muda mrefu ata usipokuwepo bado atazimudu changamoto

Magufuli ataiongoza Tanzania kwa miaka kumi, hata kama mtu alikuwa si shabiki wa ndege zipo na zishanunuliwa busara ni kuona wanapata faida, same applies to TTCL anayotaka kuiewezesha na yenyewe aliikuta na ataondoka ataicha.

Raisi anaweza fanya anavyoweza kwa jitihada zake kuyasaidia mashirika ya umma lakini kama yenyewe hayana mbinu za biashara akitoka hali yao itarudi kuwa vile vile.

Kama watanzania tunataka kuona haya mashirika yanapata faida na wanakuwa washindani sokoni bila ya Magu ni lazima wawe wabunifu kama washidani wao walivyo.

Wenzao wanaelewa mafanikio kwenye soko la ushindani ni kujua gap ilipo ya wateja, kuelewa consumer expectations kwenye huduma zao, kuzindua huduma kutokana na ushahidi, kushindana kwa value na wengine na kutoa huduma yenye kiwango.

Ngoja nikupe mfano miaka mitatu/minne nyuma kupitia humu humu JF Halotel ilivyofunguliwa walikuja na clever entry strategy na ilikuwa kila ukifungua kule jukwaa la habari kuna thread halotel mkombozi sijui bei zake nafuu, hatolel sijui package fulani ni bora kushinda Voda in short habari ya mjini ilikuwa Halotel. Aikuchukua muda thread zikaanza kubadilika hawa Halotel wameanza kuwa wezi etc with malalamiko ya watanzania.

Plan hapo ilikuwa ni kuvutia wateja kwanza walipopata wa kutosha taratibu wakawarudisha kwenye uhalisia wa gharama za kuzalisha huduma na kuanza kutoza kwa bei za uhalisia kwa kuzingatia value competition leo wanawateja 10 million wakati TTCL ina laki tano.

Point yangu ni kwamba haya mashirika ya serikari hawana jitihada za kupata wateja na awajali kuona washindani wao wanafanya nini kusudi watengeneze competitive edge sokoni.

Matokeo yake results zao ni mbovu wote, sasa awawezi endelea na kuwa watoa gawio wazuri mbeleni kwa kupewa kila kitu. Magu akitoka na wao wanarudi kule kule ni bora kuwapa ukweli kama tunataka kuona wanakuwa na sustainable businesses sio kuendelea kuona wanalelewa vibaya na mlezi aliepo wanakuwa kama spoilt brats who cant fend for themselves wote iwe Posta, TTCL, ATCL, TANAPA. Airport Authorities, Bandari etc wote ni below the capacity of their potential na hawana pressure kwa sababu sisi wenyewe atutoi kasoro zao.
 
Nyongeza ya mshahara au kupandishwa cheo sio automatic,inategemea utendaji wako wa kazi na vigezo vingine kama mwajiri wako atakavyo ona fit.Let us be serious,mtumishi huko tayari kum-support mwajiri wako kwenye endevours zake za kuwaendeleza wananchi including yourself,endevour ambayo itamsaidia kupata fedha za kukulipa hata mshahara!Jamani bado unategemea mwajiri huyo huyo akuongezee mshahara?!Kama unataka mwajiri wako awe nawe,be with him in times of need.
Ndio maana nimekuambia inategemea kazi unayoifanya pamoja na kupanda kwa gharama za maisha. Sasa kama kazi unafanya, sio kwamba umekaa tu, tena unafanya kitaalam na si kisiasa, na bado gharama za maisha zimepanda, ni haki kuongezwa mshahara. Tatizo uungwaji mkono mnaoutaka ni wa kisiasa na hapo ndipo tatizo linapokuja. Ni rahisi sana kusema maendeleo hayana chama lakini bado tunaweka uchama na siasa kwenye shughuli za maendeleo. Shida kubwa hapa Africa ni kuwa viongozi hawajaweza kabisa kutenganisha siasa na masuala mengine ya utaalam, maendeleo na uwajibikaji.
 
Nilitegemea mfanyakazi aone mbali kwa kuwa ana elimu,kumbe elimu haijasaidia.Hivi unaona kwamba TTCL ni biashara per se,no.Kumbuka kwamba TTCL iki-perform vizuri through your support,itatoa gawio kubwa zaidi na hivyo utaiwezesha kukulipa wewe mshahara.Funguka kijana.
Asante kwa kutambua kuwa elimu yangu haijanisaidia.

TTCL wakiwa wabunifu na huduma zikiwaridhisha watu, wateja watakuja tu bila kutumia nguvu na kejeli kama hizi.

Madhara ya kutegemea watumishi wa umma ni shirika kubweteka then kushindwa ktk soko.

Ukiamua kufanya biashara, fanya biashara. Usitafute huruma za wazalendo.

Niliwahi kuwa na TTCL line nikaitupa kule. Hela yangu halafu nipate shida ya huduma kisa nini?
 
Jamani Economists hebu Toeni ushauri wenye mantiki mana Biashara na siasa ni kama mafuta na maji vitajitenga tu hata uchanganye..Mi naona Goverment iwekeze zaidi ktk kuhakikisha ttcl anatoa service za ukweli wateja tuta join tu kuliko uku kulazimishana
 
Back
Top Bottom