Elections 2010 Kumekucha Nzega! Selelii azomewa mwanzo mwisho!

Jamani hatupaswi kuwa na hasira hapa bali nimepost kuwapa taarifa no matter nimetumwa au la! the issue is ni lichokisema ni kweli au nimetoa wrong habari? niwape habari zaidi ni kuwa baada ya selelii kuzomewa sana jana katika kikao cha tathmini jioni selelii amelalamika kwa viongozi juu ya hali hiyo hivyo yakatoka maamuzi kuwa ni marufuku kwa wananchi kumshangilia mgombea mmoja na yametoka maamuzi kuwa kuanzia leo mikutano isifanyike sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu, kwa maana hiyo mkutano wa kwanza wa leo umefanyika kata ya puge lakini nje kabisa ya kitongoji cha puge japo haijasaidia kwani watu wamekodi baiskeli( gana gana) kuufuata mkutano na hali iliyojitokeza jana imejitokeza leo pia japo kidogo imedhibitiwa na viongozi wa msafara kwa kumfanya Bashe awe mzungumzaji wa mwisho. huyo aliyesema yupo Nzega sina hakika sana na taarifa zake kwani kwa sasa tuna malizia mkutano wa Mwisho kata ya Magengati inayopakana na wilaya ya Uyui na watu wamemshangilia sana Bashe nipo kwenye msafara! mwenye swali aulize

By definition, mkutano ni mkusanyiko wa watu wengi. Sasa wanakwepa mikusanyiko mikubwa ya watu ili iweje? Hapa kuna doubts za kutosha kuhusu hizi taarifa unazozitoa.

Tamko kama hilo sidhani kama ni sahihi. Lengo la mikutano hiyo ni kumwaga sera kwa wapiga kura, sasa ukipeleka mkutano huo nje ya makazi/kitongoji unakwenda kuhutubia miti? Sometimes unapopika stori tumia basi akili kidogo maana siyo kila mtu atakubaliana na stori ambayo inaonekana ina elements za uongo/uzushi.
 
kazi unayo diwani! hivi bashe ana wake wangapi vile? naomba unijibu maana umesema mwenye swali akuulize. jitahidi maana huyo mwislamu bwana anaruhusiwa kuongeza. nadhani wakubwa mmenielewa
 
Hii mitu bana kutukana inapenda lakini utashangaa KIBONDE anakuwa Mbunge wa Kawe.Hivi watu wanafikiri wanaowaita Mafisadi watatoka kwa kupigiwa kelele..Go go Bashe
 
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Nzega ni kweli kuwa Seleli alifanyiwa vurugu wakati wa mikutano kule kata ya Puge. Naambiwa Bashe alikodisha/amekodisha wahuni kwa ajili ya kufanya hizi vurugu na kile kinachoitwa ''kusukuma gari lake''. Mbaya zaidi Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya wamelifumbia macho hili sababu inasemekana wako kwenye kambi ya Bashe. Sidhani kama hili litamsaidia badala yake litampa publicity mbaya!
 
Mpambe wa Bashe huyooo
Acheni unazi na tuchambue hoja. Haisaidii kumbandika jina hii ni JF.
Ukweli wa mambo ndiyo huo na mkitaka kujua zaidi tafuteni walioko jimboni wakupeni hali halisi.
Utashi wetu siyo lazima uwe utashi wa wananchi na kwa bahati nzuri hata wazee walitufundisha kwa methali kuwa 'wengi wape'
 
Selelii kuzomewa ni dalili kuwa wana Nzega wanapangiwa vipaa umbele vya maendeleo yao na watu wengine. Unapozomea mwanzo mpaka mwisho au ukashangilia mwanzo mpaka mwisho, yote ni makelele tu. Wale wanaolipwa kupiga kelele kwa kushangilia au kuzomea hawaitakii mema nchi yetu. Haiwezekani KELELE ikawa ndiyo kipaaumbele maendeleo cha wananchi wa jimbo la Nzega
 
Kinyang'anyilo cha uchaguzi wa kura za maoni mwaka huu katika jimbo la Nzega kimeanza kwa vibweka baada ya mbunge wa jimbo anayemalizia muda wake Lucas L selelii kuzomewa mwanzo hadi mwisho alipopewa nafasi ya kujieleza huku wananchi wakimzomea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mkutano huku wakipaza sauti Asulubiwe! Asulubiwe! hatumtaki hali ilyopelekea hatari ya mkutano kuharibika . kibaya zaidi ni pale alipopanda Husen Bashe yeye alishangiliwa kiasi cha kushindwa kujieleza kwani kelele za wananchi zilikuwa kubwa mno na baadae wananchi wakakumbusha enzi za mrema kwa kulisukuma gari la Bashe hadi pale vyombo vya usalama vilipoingilia kati kwa kuuzuia umati huo wa watu

Na kweli alisulubiwa... sasa sijui na yeye atafufuka kutoka wafu??!!
 
Well inajulikana wazi kuwa Bashe ni pandikizi la Lowassa na RA. Vijana walitumwa huko miezi miwili iliyopita kununua kura za wanachama.
 
Back
Top Bottom