Kumekucha Nzega! Selelii azomewa mwanzo mwisho! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumekucha Nzega! Selelii azomewa mwanzo mwisho!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Diwani, Jul 23, 2010.

 1. D

  Diwani Member

  #1
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinyang'anyilo cha uchaguzi wa kura za maoni mwaka huu katika jimbo la Nzega kimeanza kwa vibweka baada ya mbunge wa jimbo anayemalizia muda wake Lucas L selelii kuzomewa mwanzo hadi mwisho alipopewa nafasi ya kujieleza huku wananchi wakimzomea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mkutano huku wakipaza sauti Asulubiwe! Asulubiwe! hatumtaki hali ilyopelekea hatari ya mkutano kuharibika . kibaya zaidi ni pale alipopanda Husen Bashe yeye alishangiliwa kiasi cha kushindwa kujieleza kwani kelele za wananchi zilikuwa kubwa mno na baadae wananchi wakakumbusha enzi za mrema kwa kulisukuma gari la Bashe hadi pale vyombo vya usalama vilipoingilia kati kwa kuuzuia umati huo wa watu
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tupe chanzo cha habari. Au wewe mwenyewe ulikuwepo pale?
   
 3. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mpambe wa Bashe huyooo
   
 4. D

  Diwani Member

  #4
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoja na upambe nilikuwepo kwenye mkutano, ni kata ya Ndala baada ya kutoka Budushi na sasa hivi tumefika kata ya puge kata aliyozaliwa selelii watu wamelizunguka gari la Bashe kila mtu anataka kumpa mkono, hadi sasa selelii bado hajashuka ndani ya Gari nadhani anaongea na simu
   
 5. a

  atina Member

  #5
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 29, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata manabii walikataliwa kwao!!!!
   
 6. w

  wamlaga Member

  #6
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa hana uhakika kwani mimi nipo nzega na hali hiyo haipo acheni uongo
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Ngoja ahamie CHADEMA baada ya sakakasi zenu muone......
   
 8. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Kama hawamtaki kuna siku ya kupiga kura..zomea ya nini?
  Seleli nae asome alama za nyakati atakiwi tena huko..tafuta tumaini jipya..
  Achana na hao wasiotaka kukosolewa hata 'wanapokula wakasahau kunawa'...
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mbinu za EL na RA?
   
 10. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,993
  Likes Received: 1,047
  Trophy Points: 280
  Hiyo inajulikana wazi kwani, huyo EL huwa anakuja hapa mara kwa mara na kufanya vikao vya siri kwa lengo la kummaliza Selelii,
  hivyo sintomshangaa huyu ajiitaye Diwani kwa kauli yake hiyo. Tunajua ni mwaka wa uchaguzi tutaona/sikia mengi, kuanzia:
  Same Mashariki hadi Kyela, Nzega hadi Urambo, Kahama hadi Sikonge, Vunjo hadi Kwa Dr. Slaa n.k n.k kisa tu Waheshimiwa hawa walikuwa against Richmond, EL, RA, n.k.

  Hatuhitaji hekaya za Abunuwasi hapa yatupasa kusubiri kura za maoni. Vp wewe Diwani kwa upande wako Huzomewiiiii!:shut-mouth:
   
 11. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #11
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,263
  Trophy Points: 280
  Mhnnn!!Mwaka huu lazima pachimbike siutani hii ndo itatupa pcha halisi ya 2015 patakuwaje sbiri wachache warudi idodomya!!subiri!!:blah:
   
 12. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Asijali, ajipange tu maana wengi wamepangwa kuwaangusha wapiganaji wa ufisadi . CCM wang'oeni mapema tuwapeleke kwa Dr wa Demokrasia na Maendeleo ya kweli SLAA
   
 13. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #13
  Jul 23, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hivi inawezekana ehe?
   
 14. Kamaka

  Kamaka JF-Expert Member

  #14
  Jul 23, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 565
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hii kali
   
 15. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Diwani usitake kuanza kuaminisha watu kuwa selelii hatakiwi jimboni, si tusubiri kura za maoni! umesema watu awalikumbusha enzi za mrema kwa kulisukuma gari la Bashe, je unakumbuka pia pamoja na mrema kusukumwa ni mkapa ndie aliyeshinda! kusukumwa gari si hoja, huenda Bashe na kundi lake walikodi watu kufanya hivyo ili kum frustrate Selelii, angalia sana Diwani na Bashe wako msije zimia baada ya kura za maoni! kumbuka " ajidhanie amesimama aangalie asije akaanguka"
   
 16. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #16
  Jul 23, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,024
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hii siyo kali tegemea zaidi. Hadi Octoba!
   
 17. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #17
  Jul 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  pesa kiasi gani za ufisadi zimetumika hapo .. kikao chenu na RA kitakuwa saa ngapi?
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #18
  Jul 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,663
  Likes Received: 21,887
  Trophy Points: 280
  Nimefatilia post zake zote yeye ni sifa kwa Bashe na shutuma kwa Seleli. Watu wa aina hii hawatufai hapa JF maana wanatupotezea muda wetu kwa habari za kishabiki kwa makundi yao. Naye anapoteza muda kwenye keyboard, akasukume gari la Bashe roho yake ipate burudani.
   
 19. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #19
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Story kama ghost kushabikia ufisadi
   
 20. D

  Diwani Member

  #20
  Jul 23, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hatupaswi kuwa na hasira hapa bali nimepost kuwapa taarifa no matter nimetumwa au la! the issue is ni lichokisema ni kweli au nimetoa wrong habari? niwape habari zaidi ni kuwa baada ya selelii kuzomewa sana jana katika kikao cha tathmini jioni selelii amelalamika kwa viongozi juu ya hali hiyo hivyo yakatoka maamuzi kuwa ni marufuku kwa wananchi kumshangilia mgombea mmoja na yametoka maamuzi kuwa kuanzia leo mikutano isifanyike sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu, kwa maana hiyo mkutano wa kwanza wa leo umefanyika kata ya puge lakini nje kabisa ya kitongoji cha puge japo haijasaidia kwani watu wamekodi baiskeli( gana gana) kuufuata mkutano na hali iliyojitokeza jana imejitokeza leo pia japo kidogo imedhibitiwa na viongozi wa msafara kwa kumfanya Bashe awe mzungumzaji wa mwisho. huyo aliyesema yupo Nzega sina hakika sana na taarifa zake kwani kwa sasa tuna malizia mkutano wa Mwisho kata ya Magengati inayopakana na wilaya ya Uyui na watu wamemshangilia sana Bashe nipo kwenye msafara! mwenye swali aulize
   
Loading...