Elections 2010 Kumekucha Nzega! Selelii azomewa mwanzo mwisho!

Jamani hatupaswi kuwa na hasira hapa bali nimepost kuwapa taarifa no matter nimetumwa au la! the issue is ni lichokisema ni kweli au nimetoa wrong habari? niwape habari zaidi ni kuwa baada ya selelii kuzomewa sana jana katika kikao cha tathmini jioni selelii amelalamika kwa viongozi juu ya hali hiyo hivyo yakatoka maamuzi kuwa ni marufuku kwa wananchi kumshangilia mgombea mmoja na yametoka maamuzi kuwa kuanzia leo mikutano isifanyike sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu, kwa maana hiyo mkutano wa kwanza wa leo umefanyika kata ya puge lakini nje kabisa ya kitongoji cha puge japo haijasaidia kwani watu wamekodi baiskeli( gana gana) kuufuata mkutano na hali iliyojitokeza jana imejitokeza leo pia japo kidogo imedhibitiwa na viongozi wa msafara kwa kumfanya Bashe awe mzungumzaji wa mwisho. huyo aliyesema yupo Nzega sina hakika sana na taarifa zake kwani kwa sasa tuna malizia mkutano wa Mwisho kata ya Mirambo Itobo inayopakana na wilaya ya Uyui na watu wamemshangilia sana Bashe nipo kwenye msafara! mwenye swali aulize

Na vipi kama hao washangiliaji wamekodiwa kwa kazi hiyo? umefuatilia, Je hao ni wapiga Kura kweli? mbona wanakodi Baiskeli kufuatilia mikutano? nina wasiwasi. Fisadis at work
 
Heshima kwako Diwani,

Inawezakana unatoa taharifa za kweli lakini napata shaka kidogo baada ya kufuatilia post zako za nyuma inaonekana unapenda ushabiki kitu amabacho si kizuri ndani ya jamvi la JF.Uzuri wa hili jamvi ukileta ushabiki utajulikana tu utafanyeje pengine tungepata taarifa kutoka chanzo kingine ingeweza kusaidia sana.
 
Jamani hatupaswi kuwa na hasira hapa bali nimepost kuwapa taarifa no matter nimetumwa au la! the issue is ni lichokisema ni kweli au nimetoa wrong habari? niwape habari zaidi ni kuwa baada ya selelii kuzomewa sana jana katika kikao cha tathmini jioni selelii amelalamika kwa viongozi juu ya hali hiyo hivyo yakatoka maamuzi kuwa ni marufuku kwa wananchi kumshangilia mgombea mmoja na yametoka maamuzi kuwa kuanzia leo mikutano isifanyike sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu, kwa maana hiyo mkutano wa kwanza wa leo umefanyika kata ya puge lakini nje kabisa ya kitongoji cha puge japo haijasaidia kwani watu wamekodi baiskeli( gana gana) kuufuata mkutano na hali iliyojitokeza jana imejitokeza leo pia japo kidogo imedhibitiwa na viongozi wa msafara kwa kumfanya Bashe awe mzungumzaji wa mwisho. huyo aliyesema yupo Nzega sina hakika sana na taarifa zake kwani kwa sasa tuna malizia mkutano wa Mwisho kata ya Magengati inayopakana na wilaya ya Uyui na watu wamemshangilia sana Bashe nipo kwenye msafara! mwenye swali aulize

kwa sababu wewe ni mpambe wa bashi kwa hiyo habari yako inachukuliwa kuwa ni ya kipambe tu.
 
Heshima mbele wakuu!
inawezekana kabisa mimi ni shabiki wa Bashe, inawezekana kabisa nimetumwa na RA/EL and what ever haki yangu ya kushabikia mtu au kitu haipokonywi na mtu au kitu chochote kama vile watu ambao wangependa leo CCM isambaratike na ife kabisa wakati wengine tukikesha tukisali kuomba CCM itawale milele!
 
Huyu Bashe si ni pandikizi la fisadi Rostum? Vipi watu wa Nzega wasilijue hili?
 
pamoja na upambe nilikuwepo kwenye mkutano, ni kata ya Ndala baada ya kutoka Budushi na sasa hivi tumefika kata ya puge kata aliyozaliwa selelii watu wamelizunguka gari la Bashe kila mtu anataka kumpa mkono, hadi sasa selelii bado hajashuka ndani ya Gari nadhani anaongea na simu
Kwa hiyo kazi yako ni kumpamba huyo jamaa huku JF?
 
Diwani,
Hivi Bashe atakaposhindwa kupata Ubunge utakuja kwa mbwembwe tena kutujulisha?
 
Heshima mbele wakuu!
inawezekana kabisa mimi ni shabiki wa Bashe, inawezekana kabisa nimetumwa na RA/EL and what ever haki yangu ya kushabikia mtu au kitu haipokonywi na mtu au kitu chochote kama vile watu ambao wangependa leo CCM isambaratike na ife kabisa wakati wengine tukikesha tukisali kuomba CCM itawale milele!
Sawa kabisa, ila nakushauri ushabikie kwa kumsifu unayempenda, siyo kwa kumsemea uongo au kuudanganya uma juu unayemchukia!
We sema tu huyo jamaa yako ni kidume cha mbegu, au mwanaume wa shoka kama wasemavyo akina Sophia Simba tutakuelewa!
 
Mimi nataka hawa wabunge wa SISI EMU wote washindwe na hao watakaoshinda kura za maoni washindwe katka uchaguzi, i hate CCM!!!
 
Huyu Bashe si ni pandikizi la fisadi Rostum? Vipi watu wa Nzega wasilijue hili?

umaskini wenu ndio angamizo lenu....huna hela huna sauti katika nji hii..kelele zitapigwa na hao mnaoita mafisadi watapeta kama kawa
 
Wewe ndugu usinilazimishe nikukabili wewe binafsi kwani ninawasiwasi na uwezo wako wa kueleza haya. Jifunze namna njema ya kutoa propaganda. Ninachokiona kwako unashindwa kueleza maeneo ambayo Bashe hakubaliki unajihalibia bure hatra hiyo kazi uliyo pewa itakushinda na watakuona haufa hiza pesa za richmond Nzega hazitafua dafu tupo tayari kum pa kura Dr. Kigwangala kuliko kumpa kura mtu asiyeaaminika. Nzega inawenyewe na chuki yenu kwa Selelii inazidi kumuongezea umaarufu. Njoo hapa Nata, lussu ambapo makao makuu nyake ni Mwaluzwilo, nenda Wel;a, Mbogwe , Mwanhala kote huko richmond inafahamika. hampati kitu zaidi ya kum uongezea umaarufu selelii. bado unamashaka na mimi niliye nzega vijijini?
 
umaskini wenu ndio angamizo lenu....huna hela huna sauti katika nji hii..kelele zitapigwa na hao mnaoita mafisadi watapeta kama kawa

Inasikitisha, lakini ndiyo ukweli. Mafisadi wameshika nchi, na wanamiliki almost everything in this country. Everybody need to stand-up and be counted; NOW!!
 
Kinyang'anyilo cha uchaguzi wa kura za maoni mwaka huu katika jimbo la Nzega kimeanza kwa vibweka baada ya mbunge wa jimbo anayemalizia muda wake Lucas L selelii kuzomewa mwanzo hadi mwisho alipopewa nafasi ya kujieleza huku wananchi wakimzomea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mkutano huku wakipaza sauti Asulubiwe! Asulubiwe! hatumtaki hali ilyopelekea hatari ya mkutano kuharibika . kibaya zaidi ni pale alipopanda Husen Bashe yeye alishangiliwa kiasi cha kushindwa kujieleza kwani kelele za wananchi zilikuwa kubwa mno na baadae wananchi wakakumbusha enzi za mrema kwa kulisukuma gari la Bashe hadi pale vyombo vya usalama vilipoingilia kati kwa kuuzuia umati huo wa watu

Diwani naomba nikuulize swali moja, Seleli kazomewa kwa kosa gani hasa alilolifanya? na Bashe kashangiliwa sana kwa kipi alichowafanyia wananchi wa Nzega? Maoni yangu kwako, next time naomba utuchukulie clips ya hivyo vitendo kwenye video au hata kwenye simu yako unayotumia kukutumia hizi information.
 
PHP:
Jamani hatupaswi kuwa na hasira hapa bali nimepost kuwapa taarifa no matter nimetumwa au la! the issue is ni lichokisema ni kweli au nimetoa wrong habari? niwape habari zaidi ni kuwa baada ya selelii kuzomewa sana jana katika kikao cha tathmini jioni selelii amelalamika kwa viongozi juu ya hali hiyo hivyo yakatoka maamuzi kuwa ni marufuku kwa wananchi kumshangilia mgombea mmoja na yametoka maamuzi kuwa kuanzia leo mikutano isifanyike sehemu zenye mikusanyiko mikubwa ya watu, kwa maana hiyo mkutano wa kwanza wa leo umefanyika kata ya puge lakini nje kabisa ya kitongoji cha puge japo haijasaidia kwani watu wamekodi baiskeli( gana gana) kuufuata mkutano na hali iliyojitokeza jana imejitokeza leo pia japo kidogo imedhibitiwa na viongozi wa msafara kwa kumfanya Bashe awe mzungumzaji wa mwisho. huyo aliyesema yupo Nzega sina hakika sana na taarifa zake kwani kwa sasa tuna malizia mkutano wa Mwisho kata ya Magengati inayopakana na wilaya ya Uyui na watu wamemshangilia sana Bashe nipo kwenye msafara! mwenye swali aulize

Asalaam aleikum waungwana wote. Mimi nakiri ugeni katika forum hii mahiri.
Naamini anayotujuza Diwani kuwa yanatokea na yataendelea kutokea.
Swali kwetu sote ni kuwa yanatokea kwa sababu wanaNzega hawamtaki Selelii au kwa kuwa watu fulani wanamwogopa sana Selelii hivyo hawataki arudi Bungeni?
Kwa nini sisi Watanzania tunakubali wachuuzi wa chumvi na pembe za ng'ombe watupangie wabunge wetu?
Watanzania tunajua kuwa huo unaoitwa utajiri uliokithiri wa hao wanaowapinga wazalendo kama Selelii, wamepata utajiri kupitia jasho la Watanzania kwa njia za kifisadi?
Mwana Forum Diwani anaandika kwa namna ya kushangilia kuwa Selelii kazomewa; hivi hata Watanzania wachache wenye angalau mwanga kidogo wa elimu wanaweza kushabikia kuzomewa kwa mpiganaji mahiri dhidi ya ufisadi?
Tanzania ni nchi tajiri sana. Kwa nini Watanzania tunaridhika kuendelea kuwa masikini huku tukishabikia utajiri wa mafisadi?
Wale tulio na mwanga kidogo tunao wajibu wa kuwaelimisha wale waliojinyima ili sisi tuelimike maana bila kujali mahali tuliposomea, mchango wa Watanzania masikini ni mkubwa sana kwetu sote.
Wana Nzega waelimishwe kuwa kuchagua vibaraka wa mafisadi kutawagharimu sana mbele ya safari
 
waache wafu wawaziki waffu wenzao kazi tanzania ipo kweli kweli.enyi wafanyakazi wana JF tuko wapi kuwaelimisha hawa wanaohongwa kanga na fulana nchi iteketee
 
BASHE ANAANGUKA KWA KISHINDO KWANI HAPA LUSSU YAANI9 MWALUZWILO WATU WANADAI NI BORA APITE KIGWANGALA Dr. kuliko huyu wa richmond
 
Back
Top Bottom