Bashe, Kigwangalla vita kali Nzega. Bashe amsasambua Mh. Kigwangalla | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bashe, Kigwangalla vita kali Nzega. Bashe amsasambua Mh. Kigwangalla

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kapotolo, Jun 9, 2011.

 1. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hii iko wanabidii, sijui kama ilishakuja humu, mimi sijapata kuiona, nimeiweka hapa ili muangalie mnyukano huu wa Siasa za Nzega. Haya ni majibu ya Bashe kwa Kigwangalla.

  Ili kuweza kuisoma na kuielewa kwa undani unashauriwa kusoma hii pia: Nzega: Said Nassor Bogoile ndiye Hamis Andrea Kigwangalla?

  BASHE ANAANZA HIVI:

  SALAAM
  ,

  Sikuwahi kuwa member wa hii forum lakini nimeguswa na kuvutiwa kutokana na mjadala ambao umemhusisha Mbunge wangu MH HAMIS ANDREA KIGWANGALA (SAIDI NASSOR BAGAILE) sikutaka kujadili jambo lolote lakini kilichonileta hapa kuchangia ni mambo makubwa mawili ambayo nitayataja hapa chini, leo nimefahamu kwanini Mh Kigwangala tulipokutana mara ya mwisho pale MOVENPICK Ijumaa katika kujadili baadhi ya mambo na umuhimu wa social network nikamwambia nataka nijiunge na wana bidii, alinishauri NISIJIUNGE WANABIDII KWAKUWA NI SEHEMU ISYOFAA WATU WANAPINGA KILA KITU, nimefahamu sababu kumbe hakutaka nifahamu kuwa mbunge wagu yupo huku akipotosha taarifa nyingi sana. Sikupenda kujibu hoja zake imenibidi,hizi chini ni sababu kuu zilizonisukuma kujibu.

  (1) Mbunge wangu amenitaja kwa jina katika baadhi ya mambo.

  (2) Kuweka rikodi sawa sawa juu ya baadhi maswala ya Msingi.

  Hizo ni sababu kubwa zilizonifanya niingie na kujibu baadhi ya mambo,nimesoma hoja za Mbunge ameongelea maeneo makuu yafuatayo, (1) UHALALI WA JINA LAKE (2) URAIA WA BASHE (MIMI BINAFSI) (3) AMESEMA HAKUBEBWA ( 4) AMONGELEA USHINDI WANGU (5) AMEONGELEA SWALA LA WAMA ( 6) AMEONGELEA KUWA ALIRUDISHA UNITY KTK CHAMA (7) ASILI YAKE. Haya ni maeneo makuu niliyoweza kuyaona katika majibu yake alotoa hapa.


  Nianze kwa kusema HAKUNA JAMBO BORA DUNIANI KAMA KUFAHAMU MAPUNGUFU YAKO, KUYAKUBALI NA KUKUBALI KUYAFANYIA KAZI, PIA HAKUNA JAMBO BORA KAMA KUMSHUKURU MUNGU KWA JAMBO LOLOTE UNALOKUTANA NALO kama nilivoshukuru mimi tar 2 august 2010 baada ya kuapata ushindi wa kura za maoni, na kushukuru pia baada ya kutoteuliwa na chama vyote nilimshukuru mungu.


  Nimesema haya maneno kutokana na mbunge wangu kutokuwa mtu wakushsukuru mungu kwa bahati alopata ambayo imetokana na tabia na mila za watu kumalizana kutokana na kuwa na misimamo,mitazamo,fikra,na maoni tofauti tofauti juu ya baadhi ya mambo.SAIDI be a Gentleman kubali ubunge wa jimbo la Nzega haukuwa wako hukuwa na political Vission, Mission, wala strategy ya kupata ubunge ule,bcs of CCM politics Mimi na Lucas selelii hatukuteuliwa and you KNOW it.


  NIANZE NA UHALALI WA JINA:

  Usipotoshe watu jina la Hamis Andrea si jina lako kijana mwenye jina hili yupo Nzega unafahamu na baada ya Wewe KUTEULIWA Chama na Wana CCM kilikushauri uende mahakamani kuapa kupata kiapo cha mahakama kubadili jina na kulichukua rasmi jina la Hamis Andrea na ulifanya hivo, jina la hamis andrea umelichukua Rasmi baada ya KUTEULIWA na kabla ya kuchukwa Form na kuhisi utawekewa Pingamizi, lakini deep in your heart uanafahamu wewe na mimi tumesoma same primary school na mimi na wewe hatukufaulu DARASA LA SABA KITONGO PRIMARY SCHOOL.

  Baada ya hapo kutumia nafasi ya mama yako ambae wakati huo alikua ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega ulienda mwanzoli ukachukua jina la HAMIS ANDREA na kuanza kulitumia kijana huyu alifaulu yeye na watoto wa MZEE MTANGA WAKIKE AMBAO NI TWINS kwakuwa hakuwa na taarifa mapema na kwa kuwa kijana huyu baada ya kumaliza pale mwanzoli alienda kuishi KITANGILI baada ya mitihani taarifa za ufaulu wake zilichelewa kumfikia kijana huyu, ulichukua nafasi yake na wewe kwenda KIGOMA SEKONDARI.

  Ni kweli kama ulivosema kwamba wewe nimjukuu wa mzee KIGWANGALLAH,huu ni ukoo wa mama yako na si BABA yako,na tulipokuwa tunasoma Primary ulikuwa unaitwa Jina la SAIDI NASSORO BAGAILE, nayo haya majina ( nassoro bagaile) ni ya ukoo wa mama yako tumekuwa wote hatumjui BABA YAKO na hakuna mtu wa Nzega ambae anamfahamu baba yako na siku zote imekuwa HIVYO until utakapo prove otherwise ( tunaweza kuchanga fedha hapa wanabidii watafute team ya watu wakafanye uchunguzi walete ripoti hapa tujue nani mkweli). Wanabidii mkiangalia HOJA ya kuhalalisha na U TANZANIA WA KIGWANGALA SIKU ZOTE ATAELEZA KWA KIREFU HISTORIA YA UPANDE WA MAMA YAKE UPANDE WA BABA UTABAKI UNCLEAR HATA MAELEZO YAKE HAPA YANAONYESHA HIVO,ingawa haikuwa strategy yangu kum disqualify SAIDI baada ya kuteuliwa katika uchaguzi kwa HOJA YA UIRAI bcs mimi si MUUMINI WA UKABURU HUO.


  URAIA WA BASHE:


  Nimesema mara Nyingi na leo nasema Tena URAIA WANGU HAUNA MASHAKA hata kidogo, labda nitoe maelezo mafupi hapa, Kutokana na sheria yetu ya UHAMIAJI KUNA AINA MBILI WATU kuna watanzania ambao wanaomba uraia kwakuwa hawajazaliwa TANZANIA inabidi baada ya muda wakaiishi kwa kutumia HATI MAALUM (PARMIT) Ambayo inakuwa re newable wataomba na watatangazwa katika magazeti na hawa wanatakiwa waishi si chini ya miaka 10.


  Kundi la pili ni Mtanzania ambae anazaliwa Tanzania na ambae mzazi wake hasa wa kiume wakati mtoto huyo anazaliwa HAKUWA RAIA wa Tanzania,now Commenting on my setuation, BABU MZAA BABA alihamia Tanzania 1949, akiwa na baba yangu waliishi mkoa wa Tabora wilaya ya Tabora mjini,BABU MZAA MAMA aliahamia Tanzania 1902 akiwa na BABA yake aliishi maeneo ya SUMBAWANGA NA BAADAE ENEO LINALOITWA LAHELA NA ALIKUWA AKIJULIKANA KAMA MZEE ABDI ALI WAJINGA, BIBI MZAA MAMA ALIZALIWA BOMA NG"OMBE MOSHI Mwaka 1920, mama yangu mzazi alizaliwa Tabora mjini mtaa wa Mwanza Road.


  Ukitazama that background utaona mzazi ambae alihamia Tanzania ni BABA yangu, kwa wanaofahamu historia ya Nchii hii watakumbuka 1957 wakati waingereza wanaandaa mazingira ya kukabidhi uhuru wa TANGANYIKA waliita all MINIORITY SOCIETY ambao walikuwa chini ya British Ambrella, na kuwaambia wana uhuru wakuchagua kubaki na URAIA wanchi walizotoka.

  Na wakati huo babu zangu wote walikua na BRITISH PASPORT KWA SABABU WALIKUA WAMETOKA ENEO LA KASKAZINI LA SOMALIA LILIKUA CHINI YA BRITSH COLONY LILIKUA LINAITWA SOMALILAND, ama wachukue UHURU WA TANGANYIKA.

  Babu zangu waliamua kuacha URAIA wanchi walizotoka na kuchukua uraia wa TANGANYIKA.


  Waliasiliwa na kuandikishwa kama RAIA wa Tanganyika na kukabidhi HATI za uingereza na wao kutambulika kama WATANGANYIKA hiyo ilikua 1957.Hi unaweza kwenda RITA katika Registry za 1957 utakuta ukoo wa babu mzaa mama na babu mzaa baba .kwa mantiki hii wazazi wangu wote ni RAIA wa Tanganyika toka 1957 mpaka 1964 wakawa Raia wa Tanzania. Kwahiyo hoja ya urai wangu haina la kujadili

  Ukiangalia 1959 TANU branch office ya Nzega ambayo kwa sasa ni ofisi ya CCM kata, alieitoa na kumkabidhi ofisi ile MAMA AMINA MAUFI wakati huo akiwa ni Mwenyekiti wa Tanu Branch na katibu wake ni Mwl shija ambae sasa ni mkiti wa CCM wilaya ya Nzega alikuwa Marehemu Babu yangu.

  Chumba kile lilikuwa DUKA lake nay eye aliwapa ili ofisi ya Tanu ifunguliwe pale,hii ni memory iliyonifanya 2008 nilikarabati Jengo lile liweze kutumika mpaka leo.


  NINI KILITOKEA BAADA YA HAPO:

  Wazazi wangu walioana baadae na kuzaa watoto sita mm nikiwa mmoja wao,kilichotokea ni kwamba 1986 /7 mzee anaeitwa MZEE RASHID NYEMBO( marehemu) ambae alikuwa Rafiki mkubwa wa Mzee wangu walikuwa na Safari ya Maswala ya kidini mzee wangu hakuwa na Hati ya Kusafiria wakati huo na u can imagine wakati huo hakuona umuhimu wa swala hilo.

  Alitakiwa kupata hati alifata utaratibu lakini AFISA uhamiaji wilaya ya Nzega alikuwa anaitwa MR MALONGO na wakati huo kulikuwa na opartion za kukamata wahamiaji na kila wakija watu kutoka makao makuu ama mkoani walikuwa wanamsumbua na kumtaka atoe maelezo ya WHO IS HE.

  Alishauriwa ni vizuri aombe UARAI KWA UTARATIBU WA MTU ALIEHAMIA TANZANIA, mzee wangu alifata utaratibu na kupewa HATI YA URAIA CERTIFICATE OF NATURALISATION 1987 na alipata hati na mambo mengine.

  Tukumbuke Sheria yetu inatambua MZAZI WA KIUME,kwakuwa niliamua kuingia katika SIASA na ninafahamu hata leo ukipata msichana unaempenda PROTECTION ni MUHIMU basi 2008. Niliamua kwenda mahakamani kukana UARAI WA BABA (si kwasababu sina sifa bali kujilinda kama mtu anapoamua kutumia kondom ni katika kujilinda na un forseen events) lakini bcs kutokana na DOCUMENTATION mzazi wangu wa kiume alipewa HATI ya URAIA 1987.


  Na mimi kwa kuwa najua in politics anything can HAPPEN hasa pale linapotakiwa jambo flani kufanyika basi wakati nagombea UENYEKITI WA UVCCM TAIFA NILIAMUA KUWA NA HATI YA KIAPO INCASE OF ANYTHING na hilo likaja kujitokeza likakosa nguvu nikatoa kiapo hoja ikafa, pamoja na kuwaeleza URAIA wangu haukuwa na shaka yoyote lakini pia nilisema nimeisha timiza sharti la kwenda mahakamani nikaitumia.

  Na 2009 niliamua kutaka IDARA YA UHAMIAJI INIPATIE CERTIFICATE OF CITIZENSHIP ambayo utaratibu wake nitofauti na ule wa mtu anepewa CERTIFICATE OF NATURALIZATION, 2009 nilipatiwa hati hiyo ambayo mpaka leo ninayo .

  Kwahiyo MH MASHA hakupotosha ,mkurugenzi wa UHAMIAJI HAKUPOTOSHA, wala mkurugenzi mkuu wa RITA hakupotosha pale alipotoa ushuhuda wa kimaandishi juu ya uhalali wa wazazi wangu kuwa katika registry ya mkoloni ya 1957 na wote hawa walikiandikia chama BARUA kuthibitisha tena baada ya mimi kutoteuliwa na mimi kuwaandikia Barua ni kitaka kauli yao juu ya upotoshaji uliofanyika,nakala ya Barua hizo ninazo mpaka leo, NIMSHAURI mbunge wangu usiongelee usilolifahamu usiwe mmoja wa wale wanaofumbia macho ukweli kujipa maliwazo ya MOYO.  USHINDI WANGU 2010


  Mh Saidi/kigwangala amekuwa mara nyingi akitaka kupotosha ukweli juu ya ushindi wangu labda watu wengi wajue historia ya mimi na wewe katika siasa za JIMBO LA NZEGA,2005 wote tukiwa tumetoka mashuleni na ajira zetu za mwanzo tuligombea ubunge jimbo la nzega wewe ukitumia Gari aina ya Mark 11 na mimi Suzuki vitara ukiwa na mkeo mimi single ukipita kuwaambia wananzega wakuchague kwakuwa wewe ni msomi, kijana na una mke.

  Huku mimi nikipita na kuwaambia wanichague kwa kuwa mimi ni kijana wao wamenisomesha na sasa nina taka kusimamia yale ambayo waliotangulia walishindwa kuyafanya.

  Wana CCM wajimbo la Nzega walinipa kura 109 na wewe kura 24 chini ya 25% ndicho ulichopata ukifananisha ushindi wangu na wako, wakati huo kaka yetu LUCAS SELELII akipata ushindi wakura zaidi ya 300.


  Baada ya hapo wewe ulikimbia jimbo hukushiriki jambo lolote wakati mimi nikiendelea kutekeleza yake niliyoahidi kwa wapiga kura kama ninavyofanya sasa, 2007 ulifanyika uchaguzi wa chama nikapa kura 1947 kati ya kura 1982 zilizopigwa na mimi kuchaguliwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM TAIFA.

  Then katika mktano mkuu wa mkao wa Tabora nilipata kura 487 kati ya kura 550 zilizopigwa na kuchaguliwa Mjumbe wa Halmshauri kuu ya CCM mkoa wa Tabora, chaguzi hiz wewe hukishiriki nilishinda huku nikipingwa na watu wote wenye Nguvu katika MKOA namaanisha WOTE. Na hapa nilizuia wizi wkura na GAZETI LA MWANANCHI LILIANDIKA STORY CCM WAONYESHA NAMNA YA KUIBA KURA.  2010 KATIKA UCHAGUZI

  Katika uchaguzi huu nilishinda kihalali katika vitua 152 wewe uliongoza vituo 3,ambavyo nata CENTRE ulinizidi kura 7,isanzu centre,na shila,wakati kaka yetu SELELII alishinda vituo Viwili ambavyo ni SILIMUKA akinizidi kura 52,na ITILO akinizidi kura 17 kama sikosei.

  LAKINI VITUO HIVO SI KATA KIKATA MIMI NILISHINDA KATA ZOTE 21, na wewe unalifahamu hili tulikua na Vituo 152 katika kata 21,vituo vyote tuliweka mawakala wote sisi wagombea wakuu 3 katika uchaguzi huo na matokea yakawa Bashe 14,420,SELELII 2500 KIGWANGALA(SAIDI)1530 kama sijakosea ukitazama kura hizo ni sawa ni 11 to 12% ya kra nilizopata.

  Wana Bidii hata leo tukirudia Uchaguzi JIMBO LA NZEGA NITASHINDA KWA KURA NYINGI SANA na ikiwezekana tuakaandikishane tukafanye kampeni nauhakika nitamshinda lakini UBUNGE aendelee nao hili sina shaka juu yake.


  Utakumbuka wakati wa kura za maoni niliwaahidi kuwashinda kwakuwa nilikuwa nafahamu kuna njama hizi nilikuambia wewe na wengine ,ninafahamu mpango wa kunikata jina lakini nitahakikisha ninawashinda kwa kura nyingi sana ili hatamtakaponikata watanzania na wananzega watapiga kelele kwa niaba yangu na historia itakuwa imeandikwa na hili lilitokea.

  Wapo wanahabari waliokuwa wananieleza juu ya mipango hii mliokuwa mnaifanya na ilifahamika mapema ,but I said to my self sijajiunga CCM kwa ajili ya UBUNGE tu nitagombea nitashindwa nitakatwa lakini nitabaki ndani ya CCM kutimiza wajibu wangu,na unafahamu hili kwa 2015 u will face me again if god wish,politically u have never been threat to me jimbo la nzega ninafahamu mtu pekee ambae ninaamini ni threat kwangu ni LUCAS LUMAMBO SELELII not you.  HOJA YA WAMA


  Sipendi kuliongelea sana hili lakini ni AJABU unapokana kuwa HUKUWAHI KUFANYA KAZI NA WAMA ni kama mimi nije katika PUBLIC nisema siajawahi kuajiriwa na ROSTAM AZIZ ni kukana ukweli ulio wazi binafsi sina uhakika kama uteuzi wako una mahusiano na kazi zako WAMA.

  Bali nina uhakika umefanya kazi za WAMA kama MUWEZESHAJI na MTOA mafunzo yapo maeneo ambayo uliwahikutoa TRAINING ambayo mimi nafahamu,mfano KANDA YA ZIWA umewahi kufanya maeneo kama shinynga ,BARAZA KUU LA UVCCM ambalo mimi nilikuwepo DODOMA 2008 feb uliletwa na WAMA why useme UONGO jambo baya sana najisikia AIBU MBUNGE WANGU ANAPO DANGANYA.inawezekana mpaka leo tunasubiri maandamano ya kufunga mgodi hakuna umetudanganya naanza kupata mashaka na wewe.

  USHINDI WA JIMBO LA NZEGA

  Be honest huweza kufanya mkutano wa HADHARA hata mmoja mpaka ALIPOKUJA MH RAIS na sote tuliahidi kukusaidia,mimi ni mmoja wa watu ambao waligombana na MARAFIKI zangu kuja kukuombea KURA ni utamaduni mwema mtu kushukuru unafahumu deep inside in ur heart hukuwa na team ya kampeni aliekuwa kampeni meneja wako MR RWANGISA ndie aliekuwa kampeni MENEJA WA KAKA YETU SELELII,leo unasema HUKUBEBWA ULIBEBWA NA CCM na wana nzega walichagua chama kilichotuokoa NZEGA kama chama ni UPINZANI kugawanyika CUF na CHADEMA ur un popular katika JIMBO NA HILI UNALIFAHAMU.


  UNITY KATIKA CHAMA

  SAIDI/KIGWANGALA wana ccm waliungana kukisaidia chama chetu nah ii haikuwa jitihada yako binafsi wala jitihada ya mtu mwingine wewe si ulieleta umoja katika chama bali itikadi z wana ccm ndizo zilizo waunganisha watu wa nzega na ukiangalia katika historia yetu ya jimbo this time ni mwaka ambao watu walijitokeza kidogo kuliko waliojiandikisha,hukupata hata kura za wanachama wa ccm walipiga kura wote,utakumbuka binafsi nilipita maeneo yote ambayo wewe ulishindwa kuyafikia ulienda maeneo hayo baada ya mimi kuwa nimepita na kueleza why wachague CCM na sikuwahi kutumia JINA lako kuombea kura chama BCS nilijua the only instrument ya kuwafanya wana Nzega wakuchague ni kutumia CCM.

  HITIMISHO

  Wana bidii mara nyingi MH mbunge wangu amekuwa akitaka tuamini kwamba yeye A kumbe ni B its good kusimama kwa RANGI yako sikupanga kuyaongea haya lakini imenilazimu kufanya hivo baada ya kuwa mara zote nikiangalia mkuu wangu akipotosha ukweli juu ya mambo mengi.

  Jambo la msingi kubali hukushinda nzega ,hukuwa chaguo la wana nzega,umefaidika na migogoro ya kisiasa ndani ya mkoa na Taifa hili,leo usilazimishe watu wakaanza kufanya kazi kuangalia CREDIBILLITY ya hata ELIMU YAKO NI QUESTIONABLE, ukiangalia unaongela umesoma MASTERS ya Bsness Administration, KAROLINSKA institute a lot of questions with no answer.

  Tutaangalia credibility ya Degree yako ya Muhimbili,tutaangalia uhalali wa wewe kuchukua kiapo cha kubadili jina siku tatu kabla ya kujaza fomu,usilazimishe tujadili ambayo si sawa kuyajadili wewe ni kiongozi sasa acha siasa za uongo,upotoshaji,simamia unachokiamini na si wanachokiamini wengine.

  Tutahoji moral authority juu ya mambo mengi unayoongea wakati wewe ni mmoja wa walio benefit na STIMULUS package 2009/10 ambazo hazikuwafaidisha wakulima zaidi ya kujinufaisha wewe binafsi kununua ma Range mjini na kuja kugombea ubunge Nzega kwa Fedha za walipa Kodi kupitia kampuni ya MSK ambayo wananchi wa Nzega hiuta jina la Ambalo unalifahamu,,tutakuhoji uadilifu wako wakati wewe ni mtu alilazimisha wananchi wa nzega waache kulima mazao ya chakula walime PAMBA kujinufaisha wewe binafsi na biashara yako na kushindwa kuwapa pembejeo matokea yake PAMBA wakose na chakula wakose.

  Na sasa wanakabiliwa na njaa ukitumia nafasi yako ya ubunge kuhamasisha kilimo cha pamba na matokeo yake kuwatia watu umasikini na sasa wana nzega wanakabiliwa na njaa,

  Umefika wakati wa wewe kusimamia ahadi ulizotupa jimboni Tunasubiri maandamano siku 21 zimeisha,na hapa nilikushangaa lakini nikakubali kujifunza kitu kipya Mgodi ule upo pale kisheria,ni ilani ya chama uliyoinadi,leo unaandaa maandamano kuondoa?

  Nikasema labda new approach ktk siasa zetu,Umetuahuahidi mikopo kina mama nzega umechukua viingilio vyetu hujatoa mkopo mpaka leo ni either urudishe 6000 ulizochukua ama uwape mikopo,sio kupita na kuchinja Ng"ombe na pilau vijijini ndio maendeleo tuliotaka wana nzega.


  Sikutaka kujakutoa maelezo marefu hapa,kama nilivokushauri juzi wakati tunachangia mfuko wa maendeleo wa mkoa wa TABORA Yule kijana unajua unatumia jina lake unajisikiaje anabeba mizigo sokoni na GANAGANA,msaidie mtafutie mtaji akafanye biashara hata nje ya Nzega kwa Mungu utaoneka umeshukuru,bila ya Jina lake leo may be usingekuwa hapo ulipo una RESPONSIBILITY YA KIBINAADAMU KUMSAIDIA YULE BWANA HAMIS.

  Mwisho kuwa mkweli ukweli utakuweka HURU
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bashe ni Kichwa kumbe!
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,403
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Barua ndefu kama hii...
   
 4. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ukisoma saana, Hamisi anatakiwa kuvuliwa ubunge, na mama yake anatakiwa kufikishwa mahakamni kwa kuiba haki ya kijana wa watu kwenda sekondari. Hii makala inaweza kusaidia wanasheria kuanza kuandaa mashitaka.

  Na wanatakiwa wamlipe kijana kwa kuua maisha yake, hatuwezi kuendekeza ujinga huu, angekuwa ametumia jina na kushinda mtihani hapo tunaweza kumsamee, lakini kijana kashinda mtihani then unampeleka mwanao?

  Kwa jina la mwingine no no no, hata huyu hakimu/au mwanasheria aliyemwapisha kwa jina hili bila kufanya uchunguzi naye anatakiwa afungwe tu
   
 5. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hahaha... nakumbuka kuna mdau alisema members wengi wa JF ambao ni wavivu kusoma hawawezi mada za kutoka wanabidii ... kule hoja hujibiwa na hoja ..
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ukijua huu wenzako wanajua ule... kazi ipo
   
 7. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  Ni kweli baba Mchungaji, ni makala yake ya pili hii naisoma ikiwa na mashiko.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nilianza kusoma nikajikuta nimesoma yote!
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa ukweli na kukiri kutamuweka huru!!amsaidie yule kijana alieiba jina lake sababu labda ya uwezo!!!!!!
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Duh, apa ngoma inogile lino!! Hizi sarakasi za wanaCCM zinafurahisha sana. Yetu macho tu. Mtajimaliza wenyewe, wala hamuhitaji CHADEMA iwamalize.
   
 11. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  huwezi kuacha, nilitaka kusummarize nikaona kila ninachoondoa ni point.
   
 12. k

  kbhoke Member

  #12
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Du, mambo hayo!!!!!
   
 13. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa ni kichwa. First time nilimsikia akiongea baada ya kuambiwa sio raia, still he was very composed na aliongea bila kinyongo. He is very humble, na busara nyingi. Namheshimu ingawa yuko chama cha magamba.
   
 14. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ashitakiwe!!! Asulubiwe!!
   
 15. L

  Luiz JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bashe umenena tatizo chama magamba ni fitina na chuki kama wamekuchukia lazima waseme wewe sio mtanzania.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wanajamii sikilizeni kwa makini, haya yamekuja baada ya Hamis kuuliza swali la umeme ambalo Rostam, Bashe na Lowassa ndio Prime member................

  Haya yote CCM waliyajua hata kabla ya uchaguzi, alas they didnt realise kwamba Hamis was fighting from within.

  Hii yote ni ile vita ya mafisadi na ccm safi

  Mtasikia mengi sana, ila kama mnaipenda Tanzania mtanielewa

  Hamis amegusa mslahi ya wakubwa wa mafisadi and Bashe is their korokoroni
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hamis kamgusa tanesco na ufisadi wa symbion, epa na richmond, usiwe kipofu
   
 18. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Ehee hiyo vita ni kali, vipi wanamaghamba mmeamua kuparulana? Hiyo Nzega sasa haikaliki ni moto, Mhs Mbunge vipi unajibu au vipi?

  Wacha nikapumzike bwana
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.... ati tunakubali Bashe leo msafi, kesho atakuwa Lowassa keshokutwa Rostam

  tusiwe black and stupid

  tunatumiwa na hamis atakua mbuzi wa kafara kuhoji umeme kwenye swali kwa wizara yao

  kesho mtasikia zaidi ila mwenye uzalendo atajua na kumlinda hamisis


  acheni ujinga wa kutumiwa na wezi wa rasilimali zetu
   
 20. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  u might be right, lakini hii haiondoi ukweli kwamba Mh Kigwa ana kesi ya kujibu
   
Loading...