Kumekucha CCM vs UKAWA

Kumekucha CCM vs UKAWA

Daahh ni muda sasa ffu hawajawa bize sasa wamepata kazi
 
Huyo mtoto wa Mura hajui wala hana mamlaka na hicho anachokiongea. Labda kwao tu Tarime jambo hilo kwa kiasi wanaweza kujaribu kulifanya wakiwa na huto tupanga twao na wataipata fresh.

Mimi nina watoto kadhaa wakubwa kuliko huyo Mura, nusu ni wana CCM na nusu ni wana UKAWA, na tunaishi pamoja kama familia. Inawezekanaje eti wasishirikiane kwa sababu eti kuna Mura mmoja aliyeajiriwa BAVICHA katoa tamko. This is more than ridiculous!
 
Kuona watu anataka comments mana kwamba wako choking. No kweli kwamba hayo mahafali alikuwa ya kaskazini? Hii nchi mnaipeleka wapi? Nawashauri viongozi wenzangu tumlilie Mungu ashuke mwenyewe sasa maana busara na hekima ya binadamu imeshindwa kufanya kazi. Anayeweza sasa ni Yeye mwenyewe tu
 
Inanisikitisha sana kuskia upuuz kama huu, yaani mmekaa mkafiria sasa twende tukawatenge wananchi kwa itikadi zenu kipuuzi puuzi tuu, kwa taarifa yenu muishie huko huko mtengane hukohuko, watu wafarakane kwa kutetea matumbo ya watu wachache, sio siri huku ndio mnako force tuelekee
haya mambo usiyadharau sana.
 
Hatari sana ,, yaaani vyama vifanye tushindwe hata kuzikana ??
 
Kama ndugu yako ni ccm na amefariki utafanya nn na wewe cdm
 
Nimetafakari kwa kina sana na nimefikia maamuzi ya kuunga mkono maamuzi ya BAVICHA , lengo langu kuu likiwa ni kuepusha shari zaidi , waendelee na yao na sisi tubaki na yetu , kujiepusha na hatari ni njia bora zaidi ya kubaki salama .
 
UZURI ni kwamba WATANZANIA hatujafikia level hii ya kufanya MAIGIZO mnayotaka tufanye..afu MKAE MJUE vyama vya SIASA SI DINI ZETU wala MAKABILA YETU kiasi kwamba inaweza tenganisha umoja wetu.....NA KATIKA HILI MNAJIDANGANYA maana CDM haina ushawishi wowote kwa WATANZANIA kwa kipindi hichi ambacho WATANZANIA wote tunamuona MAGUFULI NDIO MKOMBOZI WETU.....kuthibitisha hili tuone kama mtafanikiwa mnachotaka kukifanya.....
AFU na nyie BAVICHA ebu mtuambie TOKEA huu mwaka umeanza mmeisha toa matamko mangapi juu ya SERIKALI HII na JE MAFANIKIO yenu juu ya HAYA MATAMKO ni yepi???...EBU TUPENI MREJESHO ili tuwasapoti katika hili....MAANA TUMEISHA WACHOKA NA MATAMKO YENU YA SIYO KUA NA KICHWA WALA MIGUU
Tatizo wewe mwenyewe siasa umeigeuza kuwa dini!
 
Kama ndugu yako ni ccm na amefariki utafanya nn na wewe cdm
Tamko la vijana limezingatia yote haya , aliyetamka naye anao ndugu waliosalia gizani , bali ameona hali halisi , kama unaye ndugu ambaye ni sehemu ya wanaokunyanyasa unaogopa nini kuachana naye ? Undugu ni lazima uwe wa pande mbili .
 
Hao Bavicha bangi tu hawawezi kuharibu umoja aliotujengea mwasisi wa Taifa Hayati Baba wa Taifa. Mie nyumbani mdogo wangu CHADEMA, mjomba wangu UDP, Mama yangu CCM sasa mama yangu akipata tatizo mdogo wangu asimsaidie kisa CCM? Nadhani hizo zitakua ni akili za kushikiliwa na DJ Mbowe
 
Inanisikitisha sana kuskia upuuz kama huu, yaani mmekaa mkafiria sasa twende tukawatenge wananchi kwa itikadi zenu kipuuzi puuzi tuu, kwa taarifa yenu muishie huko huko mtengane hukohuko, watu wafarakane kwa kutetea matumbo ya watu wachache, sio siri huku ndio mnako force tuelekee

Dini zenyewe zimeshindwa kututenganisha sembuse upuuzi wa vyama vya siasa.
 
Mie mbona nimeshaanza kutoshirikiana nao mwana JF yeyote wa CCM ninayemjua akianzisha thread sichangii.
ha ha haaaa.
 
Back
Top Bottom