Kumekucha CCM vs UKAWA

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
MAMBO yanazidi kwenda mrama kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), anaandika Dani Tibason. Msimamo uliotolewa na Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) unaakisi mwanzo mpya wa msuguano wa kisiasa nchini.

Tayari BAVICHA wametangaza msimamo wa kutoshirikiana na vijana wa CCM katika tukio la aina yoyote. Mbali na kutangaza msimamo huo pia wametangaza kuzuia mikutano yote ambayo itaandaliwa na CCM kama inavyozuiwa ya CHADEMA.

Msimamo huo umetolewa leo na Julius Mwita, Katibu Mkuu wa BAVICHA wakati akizungumza na waandishi wa habari Dodoma.
Mwita amesema, kutokana na kitendo cha Serikali ya CCM kushirikiana na Jeshi la Polisi kuzuia mikutano ya Chadema kinaonesha wazi kuwa, serikali ina mpango wa kuhakikisha inaua upinzani jambo ambalo haliwezi kukubalika.

Amesema, kutokana na hali hiyo kwa sasa BAVICHA wametangaza kutoshirikiana na vijana wa CCM katika mazingira yoyote ikiwa ni pamoja na katika masomo, nyumba walizopanga, misiba na katika majamga mengine mbalimbali.

“Kutokana na kuwepo kwa vitendo vya kikatili vinavyofanywa na Serikali ya CCM vya kuzuia mikutano ya upinzani, sasa tunatangaza sisi vijana wa Bavicha hatutashirikiana na wanachama wa CCM kwa njia yoyote ya kijamii wala kimaendeleo.

“Natangaza kwa vijana wote wa CHADEMA hatutashiriki katika mazizi, hatutashiriki kusoma nao wale waliopo katika vyuo, hatutashiriki sherehe mbalimbali zinazowahusu wao wala hatutashiriki katika jambo lolote la kimaendeleo, na hii ni msimamo wetu.

“Pia tunawapongeza wabunge wetu kwa kususia shughuli zote za ambazo zinafanywa na CCM kwani kwa kufanya hivyo inaonesha kuwa sasa tumechoka na uongozi wa kiimla,” amesema Mwita.

Hata hivyo amedai, Rais John Magufuli ni muoga kuliko marais wote kwa kuwa ni rais ambaye hapendi kukosolewa na kuambiwa ukweli pale ambao amekuwa akikosea jambo ambalo anatakiwa kujitafakari na kujikosoa.

“Sasa vijana vijana tumejipanga kuhakikisha Jeshi la Polisi linazuia mikutano au mikusanyiko ambayo inafanywa na CCM na ikumbukwe kuwa, 23 Julai mwaka huu CCM watakuwa na vikao vya kumkabidhi rais Magufuli kuwa mwenyekiti wa CCM.

“Sasa tunataka Jeshi la Polisi kuzuia mkusanyiko huo na kama haitawezekana vijana wa CHADEMA na UKAWA watazui mikutano hiyo.

“Haiwezekani mikutano ya CHADEMA ikawa ndiyo inayozuiliwa wakati mikutano na mikusanyiko ya CCM inaendelea kufanyika, jambo hili kamwe haiwezi kukubalika na tunasema sasa imefika mwisho wa uvumilivu,” amesema Mwita.

Edward Simbeye, Katibu Mwenezi BAVICHA amesema, yeye ndiye mratibu wa mahafali za wanafunzi wa CHADEMA vyuo vikuu (Chaso) nchini hivyo polisi walipaswa kumkamate yeye na si kuzuia mahafali hayo.
 
Duu mbona mambo yanazidi kuharibika. Tunapoelekea mambo yatazidi kuharibika. Raisi kama ni msikivu aliangalie hili kwa jicho la tatu.
 
UZURI ni kwamba WATANZANIA hatujafikia level hii ya kufanya MAIGIZO mnayotaka tufanye..afu MKAE MJUE vyama vya SIASA SI DINI ZETU wala MAKABILA YETU kiasi kwamba inaweza tenganisha umoja wetu.....NA KATIKA HILI MNAJIDANGANYA maana CDM haina ushawishi wowote kwa WATANZANIA kwa kipindi hichi ambacho WATANZANIA wote tunamuona MAGUFULI NDIO MKOMBOZI WETU.....kuthibitisha hili tuone kama mtafanikiwa mnachotaka kukifanya.....
AFU na nyie BAVICHA ebu mtuambie TOKEA huu mwaka umeanza mmeisha toa matamko mangapi juu ya SERIKALI HII na JE MAFANIKIO yenu juu ya HAYA MATAMKO ni yepi???...EBU TUPENI MREJESHO ili tuwasapoti katika hili....MAANA TUMEISHA WACHOKA NA MATAMKO YENU YA SIYO KUA NA KICHWA WALA MIGUU
 
ukisikia mbwembwe ndo hizi,wanafikiri bara ni sawa na zanzibar??kama wao wanajitenga wajitenge tu,waanze na kuwatenga na mama zao na baba zao maana baadhi yao ni wanaccm,hawatoamini na macho yao hayo wanayoyaongea yataishia hapohapo........
 
UZURI ni kwamba WATANZANIA hatujafikia level hii ya kufanya MAIGIZO mnayotaka tufanye..afu MKAE MJUE vyama vya SIASA SI DINI ZETU wala MAKABILA YETU kiasi kwamba inaweza tenganisha umoja wetu.....NA KATIKA HILI MNAJIDANGANYA maana CDM haina ushawishi wowote kwa WATANZANIA kwa kipindi hichi ambacho WATANZANIA wote tunamuona MAGUFULI NDIO MKOMBOZI WETU.....kuthibitisha hili tuone kama mtafanikiwa mnachotaka kukifanya.....
AFU na nyie BAVICHA ebu mtuambie TOKEA huu mwaka umeanza mmeisha toa matamko mangapi juu ya SERIKALI HII na JE MAFANIKIO yenu juu ya HAYA MATAMKO ni yepi???...EBU TUPENI MREJESHO ili tuwasapoti katika hili....MAANA TUMEISHA WACHOKA NA MATAMKO YENU YA SIYO KUA NA KICHWA WALA MIGUU

Mbuyu huanza kama mchicha. Huku tunakoelekea na ugumu huu wa maisha usishangae kupata support kubwa ya watu.

Mpaka sasa bado Magufuli hajafanya kile watanzania walichotarajia zaidi ya hadithi ya majipu. Sasa hivi ukimsifia Magu huoni watu wengi wakisupport kama ilivyokuwa miezi mitatu ya mwanzo, sasa hivi ni kama watu wamepoteana wanangoja tu mawazo mbadala ili rasmi wamtoe maanani.

Kama ugali mezani unakuja kwa shida hata utoe ahadi gani itakuwa ngumu kuungwa mkono, sana sana wananchi wataingiwa tu na hofu dhidi ya dola ila sio kukufurahia. Fanya utafiti wa kutosha, wanaosifia wamebaki wanaccm tena kwa unafiki lakini kwa ugumu huu wa maisha hata hiyo pumzi ya kusifia inaanza kukata.
 
Dah, maridhiano kwenye siasa ni jambo la busara sana, lakin siku zote ubabe una demand ukatili na kibri

Dawa ya Dharau kibri, wenye hekima na busara nchi hii mbona wapo wengi?
Dr Tulia, inteligence never trumps wisdom, source imeanzia huko bungeni,hakuna anegeuza shingo, let it happen that if we cant live like brothers, let us perish like fools
 
UZURI ni kwamba WATANZANIA hatujafikia level hii ya kufanya MAIGIZO mnayotaka tufanye..afu MKAE MJUE vyama vya SIASA SI DINI ZETU wala MAKABILA YETU kiasi kwamba inaweza tenganisha umoja wetu.....NA KATIKA HILI MNAJIDANGANYA maana CDM haina ushawishi wowote kwa WATANZANIA kwa kipindi hichi ambacho WATANZANIA wote tunamuona MAGUFULI NDIO MKOMBOZI WETU.....kuthibitisha hili tuone kama mtafanikiwa mnachotaka kukifanya.....
AFU na nyie BAVICHA ebu mtuambie TOKEA huu mwaka umeanza mmeisha toa matamko mangapi juu ya SERIKALI HII na JE MAFANIKIO yenu juu ya HAYA MATAMKO ni yepi???...EBU TUPENI MREJESHO ili tuwasapoti katika hili....MAANA TUMEISHA WACHOKA NA MATAMKO YENU YA SIYO KUA NA KICHWA WALA MIGUU
Huo ndio msimamo wa bavicha, upende husipende na watu tupo tayari kujiunga na ushauri wao, we nani hadi unawasemea watanzania?
 
Back
Top Bottom