Huku Kwetu Kuna MwanaCCM mmoja alikuwa ni mwathirika wa UKIMWI kwa muda Mrefu na alikuwa akifuata dawa za kuongeza siku za kuishi makao makuu ya Wilaya ambapo kutoka kijijini kwetu hadi wilayani(Hospitali ya wilaya) nauli ya BUS ni Tsh 10,000/= kwenda na kurudi.Sasa baada ya kumalizika uchaguzi kukatokea utengano wa kiwango cha juu sana, na kwa vile jamaa alikuwa anachangiwa nauli na marafiki zake ambao ni wana CDM wakakata huo mrija na ndugu yetu huyo akawa ameshindwa kuendelea na dozi kwa kukosa nauli ya kwenda kuchukua dawa, Jamaa AFYA yake ikawa mbaya sana na kupelekea kufariki.Bad enough baada ya kufariki watu waligoma kumzika pale kijijini kwa sababu hakuwa na eneo la ardhi yoyote, ilibidi wananzengo watoe taarifa police ndo waliokuja kuuchukua mwili wake na kwenda kuuzika wanakojua wao.
Jamani hili Tamko cyo la kupuuzia hata kidogo kwa sababu baadhi ya watu hasa wana CCM ndo wahanga wakubwa sana wa hili tamko.Kwa MTU asiyejua kinachoendelea sehemu nyingi hapa Tz hasa vijijini anaweza akasema ccm inapendwa lkn ukijitambulisha kuwa wewe ni mwanachama au mshabiki tu wa ccm, watu wanakuona kama vile ni shetani flani hivi.
CCM hili tamko ni baya sana kwa usitawi wa watu wenu I mean wanachama wenu.Kuweni makini.